JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kununua jezi halisi (original) za timu ya Simba SC, akitoa rai kwa wapenda soka wote kuepuka jezi bandia (feki).
Dkt. Mwigulu ameunga mkono kampeni ya kuhamasisha mashabiki kukataa jezi feki na kununua orijino kwa kununua jezi 200.
Ameyasema hayo nyumbani kwake Misigiri Iramba Mkoani Singida, alipotembelewa na ugeni wa timu ya mauzo ya simba ukiongozwa na Msemaji wa Timu hiyo Ahmed Ally.