TANZIA Dkt. Muhammed Seif Khatib afariki dunia

chrome

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
401
425
Dkt. Muhammed Seif Khatibu ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa siku nyingi Serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi amefariki dunia. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Uzini kisiwani Zanzibar.

Nyadhifa alizowahi kushika Dkt. Khatib
  • Mwenyekiti wa UVCCM kutoka 1978 hadi 1983.
  • Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kutoka 1978 hadi 2002.
  • Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Habari.
  • Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo
  • Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Masuala ya Muungano

Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.

Khatib.JPG


Dkt. Mohamed Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kupata shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha Dodoma

Baada ya kuongea nae kwa kina, nikawa najiuliza sijui nianze na hili jina la Daktari ambalo alilipata rasmi mnamo Novemba 25, 2011 pale alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.

“Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Ni bahati ilioje mimi kuipata Shahada hii ya juu kitaaluma”-Dkt Seif Khatib

=====

Assallam allaykum,
Uongozi wa Zanzibar Media Coporation Ltd unasikitika kutangaza kifo cha Mkurugenzi mtendaji wake Dr. Muhammed Seif Khatib kilichotokea hii leo asubuhi, taratibu za mazishi zitatolewa na familia yake baadae hii leo. Seif Khatib (70), amefariki dunia leo Februari 15, 2021 asubuhi mjini Unguja.

Amewahi kuhudumu serikalini kwa nafasi mbalimbali kama waziri wa muungano/habari pia amewahi kuhudumu km Mkuu wa organizesheni wa ccm Taifa wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la uzini, hadi umauti unamkuta alikuwa akimiliki vyombo vya habari vya zenj fm/zenj tv pamoja na gazeti la Nipe habari

Ramadhan Sendah
Meneja mkuu.


--
Dkt. Khatib amewahi kushika nyadhifa nyingi na kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (1978-82), Katibu Mkuu Umoja huo (1982 - 88) ambapo hapo kwa vijana amekuwa kiongozi kwa miaka 10.

Amekuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na awamu ya Tatu ya Mhe. Mkapa na ya nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (1988-2010), safari hiyo akianzia toka akiwa mbunge wa viti vya Vijana na baadaye wa Jimbo la Uzini tokea mwaka 1988 hadi alipostaafu mwaka 2015.

Vile vile amekuwa Mjumbe wa NEC ya CCM tokea 1978 hadi 2017, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (1995-2017), na baadaye Katibu wake wa Oganaizesheni 2012-2017.

Licha ya kuwa mwanasiasa mwenye nyadhifa mbalimbali, Dkt. Khatib katika muda wake wa ziada alikuwa mwandishi wa makala za michezo katika gazeti la Serikali la Daily News, gazeti la chama Uhuru na katika Mzalendo akiwika na makala yake mashuhuri KIPANGA.

Na hakuishia magazetini pekee. Huyu bwana pia ni Mwandishi mashuhuri wa vitabu vikiwemo “Fungate ya Uhuru”, “Wasakatonge”, “Chanjo”, “Vifaru Weusi”, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar” na “Taarab Zanzibar”.
 
Back
Top Bottom