Zanzibar 2020 Dkt. Magufuli: Nitapata tabu ya kumpata Waziri wa Ulinzi nikichaguliwa kuwa Rais

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombea urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Unafiki wa Magufuli ni wa kiwango cha Shetani !!

Kwanza sisi hatukuchagui tena. Acha kujitoa ufahamu...
 
Inasikitisha sana tena sana kauli kama hizi, ni hatari sana kwa kweli ni lazima zikemewe haijalishi chama gani. Haya mambo Tz hatuna na wala hatujawahi kuongea huu upuuzi piga kampeni lakini kauli hizi hatari sana. Kwanza waziri hawezi moja na zaidi mkuu wa majeshi ana report kwa Rais ambaye ni mkuu wao wote na kupinduliwa nchi nyingi za africa mapinduzi yamefanywa na watu wa kawaida sana jeshini wala sio wakuu wa majeshi lakini haya sio muhimu. Rais lazima akemewe na hizi kauli zake na CCM viongozi wamwambie mzee hapa hapana umeteleza...
Ndani ya CCM nani aweza mkemea Magufuli? Kama JK, aliwahi ambiwa ana washwawashwa. Je, nani mwingine mwenye uwezo huo?

Ndo maana suluhisho la upuuzi wa mpuuzi huyu ni kumkataa kwenye sanduku la KURA Oktoba 28 ili jambo letu litimie....
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombea urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Kwa hali hii kweli atachaguliwa tena?
 
Mhhh kazi kweli kweli!
 
Kuna watu ni wazito sana kuelewa mambo,

Rais alitoa kauli hiyo akilenga kuonesha ubora wa Mgombea kwa nafasi ya Urais Zanzibar , Hussein Mwinyi na sio zaidi ya hapo.
Nilidhani una uelewa mkubwa wa mambo kumbe hakuna kitu. Niambie nchi ngapi uliskia Waziri wa Ulinzi ( ambaye sio mwanajeshi) alipindua Serikali.

Huyo Mwinyi, JPM kamkuta hapo na kamuacha hapo kwa sababu alikuwa anaandaliwa na CCM
 
Kama ni kweli kayasema hayo, basi nampa ushauri huu - Ajiteue mwenyewe kuwa waziri wa ulinzi; yaani awe rais na amir jeshi mkuu na waziri wa ulinzi!
 
Sio kweli ni ufinyu wako qa kufikiri tu.
Swala la kuchagua viongozi kwenye sekta nyeti inahitaji umakini wa hali ya juu na sio kukurupuka.
Jiwe anatakiwa kudhibitiwa haraka sana, vinginevyo atatupeleke shimoni huyu kiumbe, kauli nyingine si vyema zikatolewa na kiongozi kama yeye

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Lissu akisema atashinda ni kosa, huyu mbwiga mpaka keshaanza kupata shida wa kumteua inaonekana ni sawa, ndio maana hata jirani zetu wanatucheka huu sio uchaguzi ni takataka.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombea urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Hata haiingii akilini, kampeni ya kiwango cha chini sana hii.
 
Back
Top Bottom