Zanzibar 2020 Dkt. Magufuli: Nitapata tabu ya kumpata Waziri wa Ulinzi nikichaguliwa kuwa Rais

Inasikitisha sana tena sana kauli kama hizi, ni hatari sana kwa kweli ni lazima zikemewe haijalishi chama gani. Haya mambo Tz hatuna na wala hatujawahi kuongea huu upuuzi piga kampeni lakini kauli hizi hatari sana. Kwanza waziri hawezi moja na zaidi mkuu wa majeshi ana report kwa Rais ambaye ni mkuu wao wote na kupinduliwa nchi nyingi za africa mapinduzi yamefanywa na watu wa kawaida sana jeshini wala sio wakuu wa majeshi lakini haya sio muhimu. Rais lazima akemewe na hizi kauli zake na CCM viongozi wamwambie mzee hapa hapana umeteleza...
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombe urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Kwani huko CCM kumejaa viazi?
 
Labda wanataka kupindua matakwa ya wapiga kura bara na visiwani. Hali wameshaiona ni ngumu sana kwao
 
Yani JPM keshapita sasa anaanza kupanga baraza la mawaziri kwenye majukwaa ya kampeni.
 
Kuna watu ni wazito sana kuelewa mambo,

Rais alitoa kauli hiyo akilenga kuonesha ubora wa Mgombea kwa nafasi ya Urais Zanzibar , Hussein Mwinyi na sio zaidi ya hapo.
 
Hatukuchagui mzee ili usijekupata shida,, huo nao ni upendo wetu kwako mzee, hatutaki upate shida #lissu2020
 
Back
Top Bottom