Zanzibar 2020 Dkt. Magufuli: Nitapata tabu ya kumpata Waziri wa Ulinzi nikichaguliwa kuwa Rais

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombea urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Yuko sahihi Magufuli.Hussein Mwinyi ni kijana muaminifu na anayejiheshimu sana.Sijawahi hata siku moja kusikia tendo lake lolote ovu tofauti ni wanasiasa wengi au watoto wengine wa marais wastaafu.Kiukweli anastahili zawadi ya Urais Zanzibar.He is just too good to be true.
 
Alishinda na mpinzani wake mkuu Lowasa karudi nyumbani kama atakavyo rudi nyumbani Lissu hapo baadae.
Jiwe hajawahi kushinda uchaguzi wowote, sema 2015 alitangazwa tu na tume. Hata humo ndani ya fisiemu hawezi shinda ndiyo maana ikawekwa fomu moja kukwepa aibu. Hata angewekwa ashindane na wewe lazima ungeshinda na wao wanalijua hilo.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom