Dkt. John Magufuli, nami namwombea radhi Mkurugenzi wa Geita - mengi mazuri ameyafanya

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,389
1,258
Mhe Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, mtoto wako kaunyea mkono "msamehe".

Mkurugenzi kafanya mengi
  • Kajenga Zahanati,
  • Kadhibiti mianya ya rushwa,
  • Kajenga shule za msingi
  • Kaongeza mapato ya halmashauri,
  • Kadhibiti nidhamu kwa watumishi wake,
  • Kadhibiti makazi holela,
  • Na mengine mengi mazuri jamani
Mkurugenzi, nawe jiombee msamaha kwa kuwa Rais wetu ni msikivu na mwenye huruma.

Mungu akuongoze vema
 
Kutumia millioni 80 kujenga bustani + na gharama za kulitunza. Bustani ambalo halina ata mabenchi ambayo watu wanaweza kaa na kufurahia mandhari. How do you justify that?

Hiyo ni sababu tosha hafai.
 
Bajeti ya kununua lile gari ilipitishwa na Bunge la Jamhuri

Utekelezaji wake uliridhiwa na Baraza la Madiwani

Kibali cha kununua kilipitishwa na ofisi ya Waziri Mkuy

Specifications na bei ilipangwa na Wakala wa Serikal wa ununuzi ( GPSA)

Fedha zikatumwa GPSA na wakanunua GPSA

Pamoja na mlolongo wote huo Jumba bovu kapewa mtu mmoja
KAMEIBUKA KA TABIA KA UANZISHWAJI WA NYUZI ZA KUWAOMBEA MSAMAHA WABADHIRIFU WA MALI ZA UMMA NA WALE WANAOTENGULIWA KWA AMA UZEMBE NA SBB NYINGINEZO. HII NI TABIA YA HOVYO KWELI KWELI.
 
Kusema kweli tumerudi nyuma miaka zaidi ya 50!

Enzi za mwalimu Nyerere pamoja na kuminywa hasa na mabeberu( enzi hizo yalikuwa mabeberu kweli) lakini kwenye miji mingi kulikuwa na maeneo maalum ya garden na zilitunzwa vizuri. Leo kimekuja kizazi cha ajabu kinachofikiri recreation ni anasa.

Mwili wa binadamu unahitaji kuburudishwa ili kupunguza msongo wa mawazo kutokana na changamoto za kimaisha. Tatizo kizazi hiki mimba zilitungwa bar kwa hiyo kuburudika ni eidha bar,guest house,ama unga na bangi.

Hakuna anayewaza kwenda garden kwenye utulivu,au hata cinema hall.
Kutumia millioni 80 kujenga bustani + na gharama za kulitunza. Bustani ambalo halina ata mabenchi ambayo watu wanaweza kaa na kufurahia mandhari. How do you justify that?

Hiyo ni sababu tosha hafai.
 
Mbunge Msukuma tu Gari lake anadaiwa na Kampuni ya Toyota milioni 20 barua kwa spika leo atakubali gari jipya la milioni 400. acheni Mkurugenzi apumzishwe mtamponza afukuzwe kabisa.

Mmeshaambiwa kuna Tume imeundwa akachunguzwe acheni lifanyike
 
Kusema kweli tumerudi nyuma miaka zaidi ya 50!

Enzi za mwalimu Nyerere pamoja na kuminywa hasa na mabeberu( enzi hizo yalikuwa mabeberu kweli) lakini kwenye miji mingi kulikuwa na maeneo maalum ya garden na zilitunzwa vizuri.Leo kimekuja kizazi cha ajabu kinachofikiri recreation ni anasa.
Mwili wa binadamu unahitaji kuburudishwa ili kupunguza msongo wa mawazo kutokana na changamoto za kimaisha.
Tatizo kizazi hiki mimba zilitungwa bar kwa hiyo kuburudika ni eidha bar,guest house,ama unga na bangi.
Hakuna anayewaza kwenda garden kwenye utulivu,au hata cinema hall.


Tatizo sio kutengeneza recreation area but spending to create one which doesn’t serve its purpose.

Hivi hiyo bustani ambayo inajengwa in front of a busy noisy road na hakuna ata mabenchi ya wananchi kukaa ndio recreation space kweli?

If not what’s the justification ya kutumia millioni 80 kuitengeneza?

Hayo ni matumizi mabaya ya hela.
 
Kutumia millioni 80 kujenga bustani + na gharama za kulitunza. Bustani ambalo halina ata mabenchi ambayo watu wanaweza kaa na kufurahia mandhari. How do you justify that?

Hiyo ni sababu tosha hafai.
Kumbuka Wasukuma hawapendi kukalia viti, Mkurugenzi kafanya vile ili Wasukumu wakienda na ngozi zao za ngombe wapate kukaa chini bila shurti.
 
Mbunge Msukuma tu Gari lake anadaiwa na Kampuni ya Toyota milioni 20 barua kwa spika leo atakubali gari jipya la milioni 400. acheni Mkurugenzi apumzishwe mtamponza afukuzwe kabisa.
mmeshaambiwa kuna Tume imeundwa akachunguzwe acheni lifanyike
Tatizo si kwamba tupo JF basi unatuchukulia powa.

Mkurugenzi wa Temeke amenunuwa gari kama hilo kwa bri hiyohiyo mara mbili katika miaka mitano hii, moja amepewa meya wa Temeke moja anatumia mkurugenzi.
 
Kafanya yote lakini ni hilo moja ni baya kuliko aliyofanya, kwa sababu hilo gari halina faida katika manispaa hiyo, ni bora angejenga hata hoteli ingeweza kuzalisha ajira na kutoa mapato, lakini hilo gari ni kuongeza matumizi kwa kuwa ghalama ya vipuri ni bei ghali ukizingatia njia za geita bado ni za vumbi.

Kwa hiyo ameongeza matumizi zaidi na hilo ni hasara.
 
Bajeti ya kununua lile gari ilipitishwa na Bunge la Jamhuri

Utekelezaji wake uliridhiwa na Baraza la Madiwani...

Hiyo inaonyesha tuna mifumo mibovu mno ya kiutawala, ama tuna katiba mbovu inayompa Rais madaraka makubwa mpaka anaweza kuyatumia vibaya, na kuamua anavyoona kwa kupuuza ngazi zote halali za kimamlaka na kimaaamizi. Ama tuna matatizo kwa vyote, mifumo ya kiutawala na madaraka makubwa kwa Rais.
 
Back
Top Bottom