Uchaguzi 2020 GEITA: Dkt. Magufuli awataka wasichague Viongozi wa majaribio

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Leo Jumatano, Dkt. John Magufuli yupo mkoani Geita baada ya jana kutoka jijini Mwanza kuendelea na kampeni ya Urais kuomba ridhaa ya kusalia madarakani kwa muhula wa pili. Tuwe sote kujuzana yatakayojiri.

F8A0A4F1-1EAA-486D-9FFB-4A195C4A94AC.jpeg

=======

10:15 Asubuhi: Dkt. Magufuli awasili uwanjani

10:18 Asubuhi: Dua na Sala kutoka kwa viongozi wa dini

10:27 Asubuhi: Nyimbo za Asili kutoka kwa msanii Eliza

10:33 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita amemkaribisha Dkt. Magufuli aweze kuhutubia wananchi waliofika

MAGUFULI: Suala la utalii, Mkoa wa Geita umebarikiwa na fursa nyingi za utalii japokuwa kwa miaka mingi kulikuwa na hifadhi moja tu ya Rubondo
hivyo katika miaka 5 iliyopita tumeanzisha hifadhi nyingine mpya ya Burigi, Chato ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.

Katika nchi hii tumepanga kila zone ya Tanzania iwe na utalii, tulizoea utalii uko Arusha, Kaskazini. Tunataka maeneo haya ya kanda ya ziwa utalii ufanane kama ulivyo wa Kaskazini.

Tunataka maendeo ya kusini, Mbeya, Iringa napo utalii ufanane hivyo hivyo na ndio maana tumeanzisha hizi kanda na ndio maana tunaujenga uwanja mkubwa sana pale Mwanza, watalii wawe wanatoka Ulaya wanateremka Mwanza.

Tulipokuwa tukipewa madaraka, nchi yetu ilikuwa inahesabika nchi maskini duniani. Leo tuko kwenye uchumi wa kati, kweli mtu umemtoa kutoka mahali ameenda mahali penye maendeleo mazuri, mtunyime kura kweli ndugu zangu wa Geita.

Kama nchi tumeikuta masikini, leo imeingia uchumi wa kati, huu ndi wakati wa kutupa kura nyingi ili tuingie kwenye uchumi ulio mkubwa zaidi, mbinu za kufika huko tunazijua, mbinu za kutafuta fedha tunazo, mbinu za kubana mafisadi tunazo.

Msichague watu wa majaribio katika uongozi, uongozi sio wa kujaribu. Madhara yake ni makubwa ndugu zangu wa Geita, ndugu zangu watanzania msijaribu kwenye uongozi, unaweza ukajaribu gongo.

Mnipe kura za kutosha mbunge Kanyasu, nataka niwaeleze watu wa Geita, tulikuwa na michakato yetu ya CCM, hiyo ni yetu wanaccm, wapo walioongoza, tulifanya uchambuzi tukamuona ndugu Kanyasu anatosha na Kanyasu katika kipindi chake cha miaka mitano nilimteua kuwa naibu waziri wa maliasili na utalii.

Anafanya kazi vizuri lakini nimeambiwa walioshindwa kwenye kura za maoni za CCM yuko mmoja amenuna na hata kwenye mkutano huu alikuwa anapita anawaambia watu wamzomee Kanyasu, nimekusikia.

Watu wa Geita kama mnataka maendeleo ya kweli nileteeni Kanyasu, msinichanganyie. Kazi zangu zinakuwa rahisi ninapokuwa na mbunge wa CCM.
 
Leo Jumatano, Dkt. John Magufuli yupo mkoani Geita baada ya jana kutoka jijini Mwanza kuendelea na kampeni ya Urais kuomba ridhaa ya kusalia madarakani kwa muhula wa pili. Tuwe sote kujuzana yatakayojiri.
=======

10:15 Asubuhi: Dkt. Magufuli awasili uwanjani

10:18 Asubuhi: Dua na Sala kutoka kwa viongozi wa dini

10:27 Asubuhi: Nyimbo za Asili kutoka kwa msanii Eliza

10:33 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita amemkaribisha Dkt. Magufuli aweze kuhutubia wananchi waliofika
 
Na huko wanafunzi wameahirishiwa masomo? Mwanza kulikuwa na mafuriko ya wanafunzi uwanja wa Furahisha. Wahudhuriaji wa mkutano, zaidi ya 60% walikuwa watoto (wanafunzi).

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwashee hapa ni full watu wazima watoto wako darasani muda huu.

Tucheki kupitia TBC, ITV, Channel ten, Star tv, Azam nk....nk!
 
Wasanii kama wote Wa Bongo fleva achana na wa kisukumua hadi Fid Q wamempandisha jukwaani
 
Back
Top Bottom