Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada ya muda tunaweza tusifahamu aliko.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Kimsingi ninachokiona hapo ni kwamba Dr. anazungumzia upatikanaji wa katiba mpya ili kuondoa mawaa na misigano huku akiwapa changamoto wanasiasa kuwa na misimamo thabiti ambayo haitawapoteza katika medani ya siasa.
Upande wa pili Dr. anajaribu kukilinda kibarua chake kwani msimamo wake wa awali katika mijadala unajulikana
 
Hawa wasomi wetu jaman.baadhi yao wamesoma lkn hawajaelimika.Huyu ni Dkt.lkn hamna kitu pale au anajitoa akili makusudi kwa maslai yake binafsi.
 
Huwezi kuelewa ''amekaangwa'' kama uelewa wako wa kupambanua masuala ni mdogo!

Kwa hiyo ulichokiandika siwezi kushangaa!
Mbona nikama ss ccm kuanzia mwenyekiti wetu mpaka wanachama wakawaida tumechanganyikiwa na kuhama kwa nyalandu vip nn shida kwa huyu fisadi
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa hana maono na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
Ilikua na dira wakati akiua wanyama na kuuza vitalu!
 
Nyalandu kaghafilika!!

kawa mtoto ghafla, ndo mlitaka mumpe nchi?

nitakubaliana nae tu siku akisema lini tuhuma alizosema hazijawahi kuwepo ccm?

uko nako watamtenga
 
Hatumshangai huu ni mtizamo wa kisiasa (amboa ndio taaluma yake nafikiri) na sio USAHIHI.
 
Ndio mkuu sasa hapa watu hawataki kujua kama dr ni mtaalamu na aliyakiwa kujibu kitaalamu,

Kibaya zaidi naziona kashfa za Nyalandu zikiishia mtandaoni tu
Ulitegemea akazitoe mahakani au wapi Mkuu!?
 
Dr.banna amepambana weeeee mwishowe ameona hapati cheo sasa hivi yupo kimya anapambana na hali yake
 
Rubbish, huoni tofauti kati ya awamu zilizopita na hii in terms of haki, sheria, Katiba zinavyovujwa?

Sio lazima utukane ndio use umetoa hoja. Haki na sheria vina lengo LA kuleta heshima na kulinda utu wa wananchi, vipi utu Wa MTU ulikuwepo na he uliheshimiwa?

Serikali IPI sasa ya dhaifu na Escrow yake, Richmond yake, Dr ulimboka wetu, vifaa vya HIV vyetu, madawa ya kulevya yetu, wale majambazi wetu, unakumbuka msemo Wa mbayuwayu?

Unamkumbuka mtoto Wa Rais, operesheni tokomeza, operesheni nini sijui.

Tuwe wakweli, watu mmeona mpaka ghorofa inajengwa kuchungulia ikulu lakini bado tu Hanna macho na mnataka nchi ipelekwe shimoni.

Hamkuona watu wanakunywa bia bastola zikiwa mezani? Ukimgusa bega anakuuliza unanijua mimi ni nani? Sikh hizi hata humu jf hakuna kusema hunijui mimi ni nani.
 
Sijaelewa hoja yako please! nieleeshe
 
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Amkaanga . kamkaangaje sasa .
 
Taasisi inayotafsiri sheria, haki na katiba ni mahakama.

Kuandika hapa kuwa haki, sheria na katiba inavunjwa bila ya mahakama kutoa tafsiri ni haki ya fikra zako ambazo inawezekana hazina hata nguvu kisheria.

Hadi Mahakama ikivunjwa utasubiri hadi irudi ikutafsirie kuwa haki na katiba ilivunjwa siyo.............
 
Huwezi kuelewa ''amekaangwa'' kama uelewa wako wa kupambanua masuala ni mdogo!

Kwa hiyo ulichokiandika siwezi kushangaa!
Jibu kamgaangaje ??acha kujifanya unauelewa mkubwa wakati huna kitu kichwani .Fafanua alivomkaanga kama huwezi kufafanua hoja kama hizi mwadisie mkeo chumbani.
 
Rubbish, huoni tofauti kati ya awamu zilizopita na hii in terms of haki, sheria, Katiba zinavyovujwa?
Unawaza kwa kutumia ubongo au nini?..Kwahiyo awamu zilizopita zilikua sawa kwenye kila kitu!?..you have just Retired, enjoy yah pension!!
 
Back
Top Bottom