Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Kwa nini Kiongozi ndani ya ccm akiondoka na kusema yake ya moyoni kila mtu ndani ya ccm ana mshambulia akiwemo mwenyekiti wenu? Mbona ni jambo la kawaida tuu mtu asiporidhika kujiengua?
Sasa mara fisadi, mara malaya sijui nini ! Mnajiaibisha
 
Sio lazima utukane ndio use umetoa hoja. Haki na sheria vina lengo LA kuleta heshima na kulinda utu wa wananchi, vipi utu Wa MTU ulikuwepo na he uliheshimiwa?

Serikali IPI sasa ya dhaifu na Escrow yake, Richmond yake, Dr ulimboka wetu, vifaa vya HIV vyetu, madawa ya kulevya yetu, wale majambazi wetu, unakumbuka msemo Wa mbayuwayu?

Unamkumbuka mtoto Wa Rais, operesheni tokomeza, operesheni nini sijui.

Tuwe wakweli, watu mmeona mpaka ghorofa inajengwa kuchungulia ikulu lakini bado tu Hanna macho na mnataka nchi ipelekwe shimoni.

Hamkuona watu wanakunywa bia bastola zikiwa mezani? Ukimgusa bega anakuuliza unanijua mimi ni nani? Sikh hizi hata humu jf hakuna kusema hunijui mimi ni nani.
Mkuu usipoteze muda na wanafiki ....tutawafunza adabu 2020 ili upinzani tujipange upya .....bora tujenge misingi mipya ya upinzani ambayo hata kama itagharimu miaka 30 ijayo kukamata dola ....lakini utakuwa mbadala wa kweli wa CCM na si photocopy na ujanja lakini akili na watu ni wale wale ....
 
Sio lazima utukane ndio use umetoa hoja. Haki na sheria vina lengo LA kuleta heshima na kulinda utu wa wananchi, vipi utu Wa MTU ulikuwepo na he uliheshimiwa?

Serikali IPI sasa ya dhaifu na Escrow yake, Richmond yake, Dr ulimboka wetu, vifaa vya HIV vyetu, madawa ya kulevya yetu, wale majambazi wetu, unakumbuka msemo Wa mbayuwayu?

Unamkumbuka mtoto Wa Rais, operesheni tokomeza, operesheni nini sijui.

Tuwe wakweli, watu mmeona mpaka ghorofa inajengwa kuchungulia ikulu lakini bado tu Hanna macho na mnataka nchi ipelekwe shimoni.

Hamkuona watu wanakunywa bia bastola zikiwa mezani? Ukimgusa bega anakuuliza unanijua mimi ni nani? Sikh hizi hata humu jf hakuna kusema hunijui mimi ni nani.
Ongea vitu vyenye ukweli .hao kina Mimi Nani kipindi hiki. ndo wamekuwa nanguvu Sana .
Mpaka wanatoa bastola hadharani nahawafanywi kitu .tena wanawatolea viongozi .
 
Nini kinaondoa uhuru wa fikra na utu wa watu! Kwa mfano unaona mateso ya Watu unasema poa kwa sababu siyo Ndugu zako; unaona Chama hiki kinatesa Chama kile unao sawa kwa kuwa wewe si Chama kile! Nini faida ya kuwa waumini wa Dini si tunaambiwa kwa nilikuwa na njaa, au kiu au kifungoni nanyi hamkuja kuniona? Je tunadhani dunia hii ndiyo maisha yanaishia hapa! Maisha ya dunia hii na vyeo vyake ni mirage na utupu Kwao walio wa haki!
 
Mbona tofauti za jk,na magufuli zipo wazi,na yeye mwenyewe magufuli amekuwa akizisema?inamaana huyu ally yeye huwa haoni,na huwa hasikii?
 
Ukiangalia mijadala ya wasomi wetu wa UDII ni tofauti kabisa na wasomi wa kule kwa Kenyatta. Wasomi wetu ni aibu tupu. Unaulizwa kingine una-prolong majibu hatumaye hata haeleweki anajibu swali gani. Poor UDSM kutoa wasomi vilaza nchi hii.
Nimekuelewa vizuri. Huyu msomi wetu ameitumia nafasi hii kama fursa, alikuwa anatuma ujumbe mahali fulani, badala ya kujibu maswali kama mtu msomi ambaye majibu yake kwa maswali yale yangeweza kuisaidia jamii yake, ambayo ni wazi kwamba iko katika mtanzuko unaotokana na kusiginwa mara nyingi kwa katiba na sheria za nchi, naye amegeuka kuwa mwanasiasa. Hovyo kabisa!
 
Huwezi kuelewa ''amekaangwa'' kama uelewa wako wa kupambanua masuala ni mdogo!

Kwa hiyo ulichokiandika siwezi kushangaa!
Tatizo lako ni lipi? kila mtu anaeonekana kua kinyume na maneno ya huyo Dk. bashiru weww ni kupinga na kutetea umetumwa na nani haswa? au hio ndo kazi yako inayokuweka mjini?
 
Huo mkaango uko wapi kwa Nyalandu? Kaikaanga Sirikali kwa kukiri kuingilia mihimili mingine na kuhalalisha ukiukwaji huo wa haki ya kikatiba kuwa upo kabla Nyalandu hajazaliwa. Acha mihemko tulieni dawa ifanye kazi.

hata mie sijaona mkaango.lakini kuwepo kwa mwingiliano wa mihili hata kama ulikuwepo pengine umebadilika zaidi sasa.bado nyalandu anaweza kuwa sawa kwa mawazo yake.
 
Huyu Dr naye anatia huruma. Anabembelezea nafasi za uteuzi! Madokta na maprofesa wengi wa bongo wametia DOA sana hadhi ya wanataaluma kwa ajili ya kuganga njaa! Leo hii hawaheshimiki kabisa! Kuanzia profesa mzee wa kutengua barua ya kujiuzulu hadi profesa "mkweli" aliyetetea escrow hadharani kuwa si pesa za umma! wote ni majanga! hata aliyefumba macho ili ambebe kwa mbeleko profesa "mkweli" yamemshinda! Jamaa habebeki hata kwa mbeleko ya chuma lazima itoboke na amwagike tu!
 
Kuna wa wakati mahakama nayo hushindwa kutoa tafsiri hapa tukumbushane iliposhindwa kutoa tafsri
 
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Tatizo kubwa pengine kulikoni yote ya huyu dakitari ni upeo wake ni finyu.

Vyama vya siasa havina demokrasia ndani yao na hivyo hoja yake wabaki ndani ya vyama kuwahudumia wananchi haliwezekani.

Kuhama vyama siyo jibu bali ni kuonyesha ukubwa wa tatizo.

Jibu ni katiba inapaswa ipunguze minyororo ya vyama vya siasa kupitia uanachama kama rungu la kuwalazimisha wawakilishi kutetea masilahi ya viongozi badala ya wananchi

Wawakilishi wakihama au kufukuzwa chama wasipoteze sifa ya uwakilishi wao. Hapo umangi meza wa vyama vya siasa VYOTE utakuwa mwendazake
 
Rubbish, huoni tofauti kati ya awamu zilizopita na hii in terms of haki, sheria, Katiba zinavyovujwa?
Kipi cha ajabu ktk utawala huu?awamu zilizopita tulishuhudia 2001 watu Zanzibar wakigeuka wakimbizi,tulishuhudia mauaji Arusha,tumeshuhudia mauaji ya mwangosi,tulishuhudia utesaji wa kibamba,ulimboka. Tulishuhudia mauaji morogoro,tumeshuhudia mikutano ya chadema ikipgwa mabomu Arusha,tulishuhudia viongoz wa CUF wakipigwa huko temeke,mabomu kila semester huko vyuo vikuu,kufungiwa kwa magazeti,kutupwa mbali kwa maoni ya wananchi,kuanzishwa kwa cyber crime act. Hata maneno MAAGIZO KUTOKA JUU yameanza kutumika awamu zilizopita kuonesha mambo ya mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine. Cha ajabu sana ni kipi?Huyo anayesema CCM imepoteza mwelekeo kipindi hicho ndo alikua busy kula Bata na warembo mamtoni.

WANASIASA WANACHEZA NA AKILI ZETU na ticket kubwa WANAYOTUMIA ni UJINGA NA UMASKINI WETU. Hakuna mwanasiasa wa kuacha madaraka yake yote kisa eti aje akupiganie ww.
 
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Kuna uteuzi uliobakia? Watu wanajitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom