Chama Cha Mapinduzi ni genge la wezi, wala rushwa na wabadhirifu wakubwa nchi hii! Ni genge ndani msitu mnene uliojaa muumiani na monsters!!
Ndani ya genge hili hatari duniani, wanahakikisha kuna vikaragosi wao wa kutosha nje ya msitu huo wa mafedhuli! Vikaragosi hivyo vitakuwa vitapewa kwa vipipi na vibiskuti na wakati mwingine kuishia kudanganywa kwa kauli na baada ya hapo, wataingia duniani kuwatetea mafedhuli na manduli wanaoiangamiza nchi!!
Ni kweli, kwavile ni msitu mnene uliojaa majahiri wa kila aina, haishangazi wengine kujikuta wamezaliwa kwenye hilo limsitu la waovu na kujikuta wakitenda kama manduli mengine yaliyomo humo yanavyotenda!! Hata hivyo, wapo miongoni mwao ambao hatimae wanakuja kupata maono kwamba udhalimu na uovu unaofanywa na jamii yao haukubaliki, sio dunia tu bali hata akhera!
Hawa ni wale wanaoamua kuukumbia msitu huku wakirushiwa kila aina ya silaha kutoka kwa mafedhuli wao ambao hawataki kuona watu wakiungama... wanachotaka ni kuona kizazi chao cha majahiri kikiendelea kushikamana!!!