Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu


MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
10,607
Likes
16,264
Points
280
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
10,607 16,264 280
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:
 
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
10,607
Likes
16,264
Points
280
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
10,607 16,264 280
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa na wenye chama alichojiunga kuwa hana maono ya Uwaziri na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale yeye unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo ''dira'' ya CCM iliyokuwepo ''kipindi cha nyuma'' wakati yeye akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?

Tujikumbushe ushauri aliotoa Mbunge Joshua Nassari kwa Lazaro Nyalandu katika hii video!
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,838
Likes
21,551
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,838 21,551 280
Kuna hoja ya Nyalandu kuhusu CCM kukosa dira.

Kwanza unaposema CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?
Rubbish, huoni tofauti kati ya awamu zilizopita na hii in terms of haki, sheria, Katiba zinavyovujwa?
 
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
10,607
Likes
16,264
Points
280
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
10,607 16,264 280
Rubbish, huoni tofauti kati ya awamu zilizopita na hii in terms of haki, sheria, Katiba zinavyovujwa?
Taasisi inayotafsiri sheria, haki na katiba ni mahakama.

Kuandika hapa kuwa haki, sheria na katiba inavunjwa bila ya mahakama kutoa tafsiri ni haki ya fikra zako ambazo inawezekana hazina hata nguvu kisheria.
 
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
10,607
Likes
16,264
Points
280
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
10,607 16,264 280
Nimeshindwa kusoma Mpaka mwisho maana nimepata kichefuchefu katikati ya andiko
Hilo ni tatizo lako kwa sababu hukulazimishwa kufungua thread na kusoma.

Kumbuka huwezi kuupima ujinga wako kwa kuishi ndani ya fikra zako.

Unanikumbusha kuna mzee mmoja alikuwa anaisifia sana nyumba yake lakini siku moja akapata mwaliko kwenye ufunguzi wa nyumba ya rafiki yake, aliporudi nyumbani akamwambia mkewe alichokiona na kudai amekuwa akijidanganya kuwa nyumba yake ni nzuri kumbe kuna nyumba za rafiki zake ambazo ni nzuri zaidi yake.

Hii ni sawa na maneno ya waingereza yanayosema, ''Thinking beyond the box''.
 
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
10,607
Likes
16,264
Points
280
MsemajiUkweli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
10,607 16,264 280
udsm scholars kwa sasa wako mguu sawa kusubiri teuzi kamwe hawawezi kua critical. Mtego umewanasa. Katiba hairuhusu mgombea binafsi?
Ungeonyesha mguu wako pande kwa kuweka hapa u-critical wako kuhusu maswali ya Mtangazaji!
 
Congo

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Messages
1,384
Likes
722
Points
280
Congo

Congo

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2008
1,384 722 280
Nimeshindwa kusoma Mpaka mwisho maana nimepata kichefuchefu katikati ya andiko
Ukitaka kuwa critical soma na mawazo ya wengine. Hakuna lolote jipya alilofanya kwa kuhama na sio mtu wa kwanza. Alishanusa kuwa anaandaliwa vikao vya kumhoji kuhusu mwenendo na msomamo wake. Huko anakikwenda akifika aulize kilichomtoa zito kabwe ni nini. Kila chama kina misingi na taratibu zake. Ukiona hazikufai unaondoka kama alivyofanya.
 
Kete Ngumu

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Messages
5,066
Likes
3,855
Points
280
Age
28
Kete Ngumu

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2014
5,066 3,855 280
Huo mkaango uko wapi kwa Nyalandu? Kaikaanga Sirikali kwa kukiri kuingilia mihimili mingine na kuhalalisha ukiukwaji huo wa haki ya kikatiba kuwa upo kabla Nyalandu hajazaliwa. Acha mihemko tulieni dawa ifanye kazi.
 

Forum statistics

Threads 1,251,171
Members 481,585
Posts 29,760,816