Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Mijadala kama hii ni vizuri kualika watu wenye misimamo tofauti tukasikia wakilumbana.Bashiru ni kada wa CCM.Angealikwa pia mtu anayemuunga mkono Nyalandu ili kuupa mjadala uwiano mzuri kama wanavyofanyaga CNN
 
Ngosha inabidi aongeze mafuta ya taa kwenye kichuguu...inaonekana bado kuna nyoka wengi...na kila anayetokeza analamba rungu la kichwa....Hapa kazi tuu

hakuna namna hala lazima kujipa faraja

Toka yuko CCM tulisema nanyi mlisema..
Au huo ukibaraka uliisha lini? Alivyohamia CDM??
hapa ndo tunaona unafiki wa watanzania ilikuwaje aendelee kuiwakisha serikali ktk nyazifa mbalimbali na huko ccm alikuwa na vyeo vyote vikubwa ndani ya chama akaachwa ikiwa na kibaraka?
 
Mtu kajiuzulu ubunge ataogogopa vp kupotea kwenye siasa hizi za bongo
Tz hamna siasa
 
Nyalandu alikuwa hana jinsi zaidi ya kuondoka CCM hasa baada ya baraza la Mawaziri kutangazwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupewa Kingwangalla.
Mnaosuggest kilichomtoa nyalandu ni uwaziri nawashangaaa sana mjue tofauti ya scale ya waziri na mbunge is not more than 500k tshs.[emoji13] [emoji13] plus status na vingora tuu how come MTU aweze Ku surrender mamilioni kadhaa kwa ajili ya kukosa vijihela vya juu?? Kuweni logical wandugu halafu huko alikoenda ndio atapata HUO uwaziri?? Kuna sababu nje ya hizo zilizomo kwenye fikra zenu na zilizotoka kwenye kinywa chake mi mstari Wa kudadisi nauchora kuanzia alipoenda kumuona Lissu Nairobi na kuitwa kujieleza alionekana ni Bonge LA msaliti
 
Baada ya mahojiano hayo nini kikafuata??
Charles Hilary akamtukana mgeni wake alimwambia "weee fala nini?ina maana yote anayosema nyalandu huyaoni kuwa yamezidi mara kumi kuliko awamu zilizopita?ebu potea hapa!"
hicho ndicho kilichotokea baada ya mahojiano
 
Hawa kina Dr Bashiru kuwahoji maswali kama haya kwa wakati huu ni kuwaonea tu. Anajua fika kitakachompata endapo atasema maneno yanayomuuzi mfalme! Kama wastaafu wanaweza kuambiwa "wanawashwa", vipi hawa waajiriwa wa vyuo vikuu vya serikali? Hajipendi?
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa hana maono na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
Kwani kusema Chama chako kumekosa dira in dhambi? Unaweza kusema ukiwa ndani au nje ya Chama. Tatizo Chama kimejenga utamaduni wa wanachama wake kutosema ukweli wakiwa ndani ya Chama, sasa mnataka wakiwa nje waache kusema pia??
 
Mwacheni Nyalandu apumue. Sasa yuko huru na anaweza kusema tena yaliyomo moyoni mwake. Wengi wenu mko utumwani, lakini hamjielewi tu.
 
Mihimili kuingiliwa swala hili halijaanza leo, unyanyasaji wa vyama vya upinzani haujaanza leo, hata hao wanaosema eti ni bora awamu zilizopita basi labda kama wamekuja Tanzania hivi karibuni, awamu zilizopita zilikuwa vinara wa uvunjifu wa amani nchini, hata tunaowasifia ndo walishiriki kikamilifu kumuibia ushindi Maalim seif wakajaza polisi na wanajeshi kila mahali, operesheni tokomeza watu walipigwa na kunyang'anywa mifugo yao, sheria za uchochezi hayo makina cyber crime wao ndo waanzilishi, ukija katika swala la ukandamizaji wa sheria tukiacha mambo ya itikadi Tanzania tumeaumia kwa muda mrefu katika awamu zote ambazo mimi nimezishuhudia nikiwa na akili zangu, yaani awamu ya mkapa , kikwete na hii ya sasa.

Nyalandu kwenda upinzani sio vibaya ,ana haki hiyo na lazima tuheshimu maamuzi yake, rai yangu ni kwa vyama vya upinzani kuwa makini na kila mtu anaekimbilia huko, tunaweza tukafurahi kuwa tunaongeza nguvu kumbe tukawa tunajimaliza maana wengine wanakimbia baada ya kuanza kushikwa katika maslahi yao.
 
Ukosekanaji katika baraza la mawaziri hakujamuacha salama Nyalandu atupishe na sizitaki mbichi hizi.
Zama zake zimekwisha alivyoibia Taifa vinamtosha😎😎
 
Mtoa mada, Mbona hajamkaanga Nyarandu, Bali ameikaanga CCM!!

Sio kosa lako ni shida ya Kopi and Paste bila kujua habari inahusu nini.
 
CCM ilimjenga Nyalandu mpaka hapo alipofikia,kudai eti CCM imepoteza dira na mwelekeo sio kweli.Aliepoteza dira na mwelekeo ni Nyalandu mwenyewe.aende tu akaungane na ndg yake Lowassa kwenye CHADEMA ya Lowassa ili iwafie mkononi
 
Huyu si yule wa ppltical science pale UDSM? Kama ni yeye ukimkuta pale nkurumah huwa anakisoa saaana. Hasa mada za zanzibar. Yaani hpo angeulizwa kuhusu znz angefungua mhadhaa kbsaa lakini sujui nini kimempata amebadilika kdgo ktk hayo majadiliano
Labda luninga siyo sehemu zake za kusemea
 
Mimi siku zote nilidhani anaitwa Bashiru Ally kumbe ni Bushiru Ally?
 
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Sasa hapa kamkaanga au katoa maoni yake?
 
Anaitwa Dr. Bashiru Ally. MsemajiUkweli amepofushwa na haraka za kuleta mada yake hapa ili malipo yaandaliwe. Ha ha ha ha ha ha ha

Nashukuru kwa kunielewa na kuungana nami katika ' Kushangaa ' juu ya hilo jina jipya la huyo Daktari wa Falsafa la Bushiru Ally badala ya Bashiru Ally.
 
Back
Top Bottom