ha ha haaaa... kisa amejibu usivyotaka wewe. Sisi wanafunzi wake tunaona amejibu vizuri sana na kiuweledi. Ukisoma political science ambalo ndo somo analofundisha kuna kitu kinaitwa "checks and balances" katika serikali. ukimsoma Aristotle na Greek historians anaitwa polybius wameelezea vizuri sana suala la 'separation of power' na "checks and balances" katika serikali. chimbuko la theories zao zinatokana na huo mwingiliano kati ya vyombo vya serikali (Bunge, Mahakama na Utawala). kwahiyo ni kweli kabisa kwamba hili suala mihimili ya serikali kuingiliana lilianza kabla Nyalandu na sisi hatujazaliwa.
Tatizo ndio liko hapo. kusema kwamba tatizo limeanza kabla Bashiru na Nyalandu hawajazaliwa, ni fact, lakini siyo hoja hapa. Hoja hapa ni kwamba katika awamu zetu tano za utawala, suala la muingiliano wa mihimili limekuwa ajenda kubwa sana hivi sasa kwa sababu za msingi kabisa. kwamba tunaye rais ambaye haoni ubaya wa kuchanganya mihimili apendavyo, na anaamini kabisa kwamba hakuna mhimili wala nini. kuna mhimili mmoja tu. ufalme wake.
JPM haoni tatizo kufanya siasa chafu katika tukio la Kijeshi. Awamu zote zilizopita, kamisheni kwa wanajeshi zilitolewa Monduli na ni zoezi la wanajeshi na Amiri jeshi mkuu wao. sasa hii kashfa ya juzi, mpaka Rais anapokea wanachama wa upinzani wanaohamia CCM, katika shughuli ya kijeshi, hiyo ni kashfa kubwa haijawahi kutokea. Hapa nataka kusema kwamba Rais JPM anajiona yeye ni mfalme kabisaaaa. hana kikomo cha madaraka, hakuna checks and balances unazosema. kwake kila kitu kinawezakana tu. hakuna katiba hakuna sheria. ndio maana amediriki kupiga marufuku mikutano ya vyama vya upinzani (siyo mikutano ya vyama vya siasa - CCM ni tofauti), kwanza ya nje, na baadaye hata ya ndani, kinyume cha sheria, with impunity.
Katika awamu hii, Rais wa nchi anadiriki kusema watu fulani wasibomolewe nyumba zao kwa sababu "walinipa kura nyingi". anataka kusema nini hasa? kwamba maeneo ambayo hawakumpa kura wataisoma namba? na kweli, angalia maeneo ambayo kitakwimu hawakumpa kura nyingi, wanaisoma namba. Bukoba, maeneo ya Dar ambapo Bomoa Bomoa ya kufa mtu inaendelea. Anabomoa hata nyumba ambazo Mahakama imezuia zisibomolewe. Hiyo hatujawahi kuiona katika taifa letu. Serikali ina-ignore mahakama wazi wazi namna hii, tena kwa matukio ambayo yanawaumiza raia wake yenyewe? Hapo kuna mihimili?
Rais ambaye anadiriki kuiambia mahakama kwamba kama kesi zikihukumiwa haraka na serikali ikapata fedha, basi robo ya mapato yatapelekwa kwa mahakama. Rushwa ya wazi. lugha kama hizo zina utata mkubwa sana.
Bunge ambalo Naibu Spika siyo mbunge wa kuchaguliwa, ni wa kuteuliwa na Rais. na Rais anaagiza Spika afanye hiki na kile, moja kwa moja. Anaagiza hata wajumbe wa kamati za Bunge. hayo yote ni mapya ya utawala huu. na inafikia hatua anaagiza spika awashughulikie wapinzani. hapo tuna haki ya kujiuliza hata hiyo concept ya separation of powers siyo tu kwamba ina matatizo, bali haipo kabisa as far as awamu hii is concerned
Kwa hiyo uchambuzi wa Dr. Bashiru umejikita katika ukada wake wa CCM, na kuogopa kuuchambua utawala. anatumia theory za Political Science kama nyenzo za ku-advance sentiments zake kwa utawala. sasa huo siyo uchambuzi wa kitaaluma. huo ni utetezi tu, tena usio na hoja za kisomi