Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:
Nasikia wale wa Mwanza wanatakiwa waangaliwe na Human face lakini wale wa Kimara ni Animal face
 
Taasisi inayotafsiri sheria, haki na katiba ni mahakama.

Kuandika hapa kuwa haki, sheria na katiba inavunjwa bila ya mahakama kutoa tafsiri ni haki ya fikra zako ambazo inawezekana hazina hata nguvu kisheria.
Mkuu uko sawa kabisa.Mara kadhaa mimi nimetoa changamoto humu jf tutajiwe vifungu vya katiba vilivyokiukwa au kuvunjwa katika utendaji kazi wa awamu ya tano,lakini mpaka sasa hakuna aliyejibu hata kifungu kimoja tu cha katiba.
Mkuu nilikwenda mbali zaidi kwa kuwauliza,wamewahi kumsikia Tundu Lissu (Mheshimiwa) akisema rais amevunja kifungu fulani cha katiba?Nikauliza kama hajawahi wanafikiri ni kwa nini Mh Lissu hajawahi kusema hivyo? Sikupata majibu zaidi ya kuambulia vichapo vya matusi.
 
Katika mahojiano maalum, Mtangazaji Charles Hilary wa Azam TV alianza kwa kumuuliza Dkt. Bushiru Ally kama anadhani Lazaro Nyarandu ni jasiri kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema katika siasa wakati hutoa majibu halisi, tuna orodha ndefu ya watu walioitwa majasiri. Kwa mfano Dkt. Slaa wakati akiwa Katibu Mkuu na Mgombea Urais wa Tanzania ulikuwa unamuona alivyo jasiri kwenye jukwaa, kihoja na msimamo lakini leo yuko wapi? Tuna orodha ndefu. Kuhangaika na ujasiri wa mtu mmoja mmoja ni kupoteza muda kwa sababu kuna uwezekano hata yeye baada muda akapotea katika uwanja wa siasa.

Swali kuhusu tuhuma za Nyalandu kwa serikali ya Rais Magufuli kuingilia mihimili mingine ya dola na kusema kujiondoa kwake CCM iwe ni chachu ya kuanzisha mjadala wa suala hilo.

Dkt. Bushiru alitoa jibu kwa kusema, mjadala kuhusu serikali kuingilia mihimili mingine ya dola imeanza kabla hata ya Lazaro Nyalandu hajazaliwa.

Dkt. Bushiru alisema, misuguano ya mihimili ya dola kuhusu nani anamwingilia mwenzake ipo sio Tanzania pekee bali duniani kote kwenye nchi ndogo kama Tanzania na nchi kubwa kama Marekani. Hata wakati wa tawala zilizopita nchini mjadala ulikuwepo na kwa maana hii, anachokisema Lazaro Nyalandu siyo kipya.

Dkt. Bushiru alienda mbele zaidi na kusema, mihimili ya dola ni taasisi zinazotegemeana, ingawa zinaweza zikawa na mamlaka ya kiutendaji ya ndani lakini kimfumo, hizi ni taasisi zinazohudumia taasisi kuu moja inayoitwa dola. Hakutakuwa na muafaka/makubaliamo kwa wananchi wote kwa sababu vyombo hivi pia vinaingiliana, vinategemeana, vinasaidiana na vinafanya kazi moja ya kuwahudumia wananchi.

Charles Hilary alimuuliza kuhusu madai ya Nyalandu kuhusu CCM kushindwa kuisimamia serikali.

Dkt. Bushiru alijibu na kusema, huo ni mtazamo wa Nyalandu lakini anachojua yeye CCM ndio inayounda serikali na hakuna mtu aliye na cheo cha kisiasa ambaye hajapitishwa na vikao vya CCM kwa mujibu wa katiba yao lakini kikubwa zaidi, katiba ya Tanzania inasema, hakuna mtu anayeweza kuingia kwenye siasa bila kuidhinishwa na chama cha siasa. Katiba ya Tanzania hairuhusu wagombea binafsi. Kitendo cha mbunge kuhama chama kilichomteua kuwa mbunge kinamuondolea uanachama na ubunge bila hata ya kuandika barua kwa spika wa bunge. Chama ndicho kinachotengeneza serikali kupitia uchaguzi.

VIDEO:

Hoja mojawapo ya Nyarandu ni katiba mpya, je hauoni kwa suali hilo kuto ulizwa ndio linamfanya huyo unayemuita eti msomi kueleza hayo? kwani kuondoa mchanganyiko wote huo ni wazi katiba ya Warioba ndio suluhisho kuliko huo upuuzi wa hayo maelezo yanayojikita kwenye hii katiba mbovu tuliyonayo sasa.
 
Hivi kweli katika uteuzi wa juzi wa mawaziri, kama naye angekuwa ameteuliwa kuwa waziri, tena kwenye wizara yake ya zamani ya maliasili, leo angejivua kweli ubunge na uanachama wake wa ccm kwa sababu ya ccm kupoteza dira? Au hapo ccm ingalikuwa haijapoteza dira?
 
Kwani hatujui kama wasomi awamu hii wako bize kutafuta teuzi!
 
Dr kaeleza facts mwanzo mwisho. Tatizo kuna watu wanataka awaze kama wao.
Kwa hiyo unataka sisi ndio tuwaze kama yeye, ubongo wetu hatujalia wali wewe!
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa hana maono na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
DIRA YAKE HAIENDANI NA DIRA YA CCM!
NDO MANAKE!
 
.....Hivi ni kwa nini CCM mkiambiwa mmepoteza DIRA mnakuwa wakali kama simba? The late Kolimba naye aliwahi kusema mmekosa dira dah aisee aliandamwa....
 
Taasisi inayotafsiri sheria, haki na katiba ni mahakama.

Kuandika hapa kuwa haki, sheria na katiba inavunjwa bila ya mahakama kutoa tafsiri ni haki ya fikra zako ambazo inawezekana hazina hata nguvu kisheria.
....Quite irrelevant, hivi unatarajia mahakama umuamuru rais aruhusu bunge live au kuruhusu mikutano ya kisiasa? Au unategemea Ndugai apeleke shauri mahakamani kupinga kuzuiwa bunge live?
 
Akina Bashuru Ali hawa wa sasa hivi si wale tuliowajua enzi hizo,, akina Bashiru wa leo ni wale wanaosubiri uteuzi.
Ni watu wa kujikomba kwa serikali hata kama imeenda kushoto.
Wahadhiri wengi siku hizi wamekuwa ni wasakatonge kupindukia,, usomi wao wameuweka pembeni na kugeukia maslahi binafsi.
Hofu na uwonga imewatawala.
 
udsm scholars kwa sasa wako mguu sawa kusubiri teuzi kamwe hawawezi kua critical. Mtego umewanasa. Katiba hairuhusu mgombea binafsi?
Yani alichokifanya hiyo Dr. ni kuchukua upuuzi na kuufanyia justification ya kipuuzi.
Extremely rubbish.
 
Taasisi inayotafsiri sheria, haki na katiba ni mahakama.

Kuandika hapa kuwa haki, sheria na katiba inavunjwa bila ya mahakama kutoa tafsiri ni haki ya fikra zako ambazo inawezekana hazina hata nguvu kisheria.
Mahakama ndo inapaswa kusema Mhe. Lazaro Nyalandu ni Jizi Anyway Mbona nyie mmepoka mamlaka hayo?Huko sio kuingilia mhimili wa mahakama!
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa hana maono na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?

Pamoja na ufisadi na kutapanya malia na rasilimali za nchi sasa hivi CCM imeongeza kuwa na viongozi wakatili wenye roho mbaya, hilo nadhani Nyalandu aliligusia siku chache kabla hajajiuzulu.
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho? Hajui kuwa wakati akiwa Waziri ndani ya CCM alikuwa anaambiwa hana maono na chama chake hakina dira?

Je, chama alichojiunga nacho kimepata dira baada ya CCM kukosa dira? Au dira inapatikana tu pale unapokuwa Naibu Waziri au Waziri?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
Umeuliza maswali mazuri ambayo majibu yake anayo Nyalandu mwenyewe au wanaccm, ila mwisho wa siku yamebeba hoja iliyolandana na aliyoiongea jana Rais wa nchi huko kanda ya ziwa. Anasema "....... wanaokimbilia chadema yote Majizi"?
Kwahiyo walibaki ndani ya chama sio Majizi ila wakichomoka ndio Majizi? Kwanini anaendelea kukaa kimya ilihali anawajua kuwa wapo humo humo ndani ya chama na wasichukuliwe hatua, mpaka asubiri mtu anapoondoka ndio anapataujasiri wa kumuita ni "jizi"?
 
Back
Top Bottom