Dkt Bashiru akagua na kuridhishwa na ujenzi wa soko la kisasa Morogoro

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali Kakurwa leo Jumamosi Februari 15, 2020 ametembelea na kukagua hatua za mwisho ujenzi wa Soko kuu la kisasa katika Manispaa ya Morogoro.

Soko hilo la kisasa linatarajiwa kukamilika Machi 30, 2020 limegharimu kiasi cha *T. Shs Billioni 11,267,070,127.77 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli*

*"Niliishi Morogoro Kilosa kwa tokea 1986 hadi 1990 kisha nikafundisha Mzumbe mwaka moja, hii ndio sehemu ambayo tukitumia kupata mahitajio yetu, hali ilikuwa mbaya sana hapa hasa kipindi cha mvua, leo huwezi amini soko la kisasa la mfano nadhani hili litakuwa la kwanza nchini Hongereni sana Morogoro kwa kusimamia dhana ya maendeleo kwa wananchi kwa vitendo"* Dk Bashiru Ali Kakurwa

Dk Bashiru Alikuwa ziarani Mkoani Morogoro kuanzia Tarehe 13-15 Februari 2020.

IMG-20200216-WA0033.jpg
IMG-20200216-WA0030.jpg
IMG-20200216-WA0032.jpg
IMG-20200216-WA0029.jpg
 
Bashiru siku hizi anakagua miradi ya maendeleo kwani ndio kazi ya CCM kama chama hiyo? na waziri mwenye dhamana kazi yake itakuwa nini?

Kazi ya Bashiru ni kuisukuma serikali ifanye jambo fulani, then waziri mwenye dhamana asimamie utekelezaji wake, likikamilika Bashiru arudi kwa wananchi awaambie niliwaahidi kile tumeketeleza, endeleeni kutupa kura zenu.

Na ile ya kuwanunua wapinzani nayo ndio kazi ya Bashiru, japo nashangaa huwa hawaifanyi kwa uwazi sijui wanamuogopa nani wakati pesa za huo mchezo wanazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesema kazi ya Bashiru ni kuisukuma serikali ifanye jambo,mimi nadhani ili arudi kwa wananchi na kuwaambia kile serikali ya CCM imefanya ni lazima ajiridhishe yeye mwenyewe. Hivyo ana haki na wajibu wa kupita kote kwenye miradi iliyoahidiwa na chama chake then aende kwa wananchi akatoe maelezo kwa ufasaha.

macson
 
Alikuwa anakagua au ALIENDA kuona ujenzi wa soko la Morogoro?

Eti kukagua.

Ana fani ya UHANDISI MAJENGO?
Pia kwani hilo soko linajengwa na CCM? yani awamu hii tutaona mengi? hutofautishi Serikali na lichama.
 
Mkuu umesema kazi ya Bashiru ni kuisukuma serikali ifanye jambo,mimi nadhani ili arudi kwa wananchi na kuwaambia kile serikali ya CCM imefanya ni lazima ajiridhishe yeye mwenyewe. Hivyo ana haki na wajibu wa kupita kote kwenye miradi iliyoahidiwa na chama chake then aende kwa wananchi akatoe maelezo kwa ufasaha.

macson
Maendeleo huwa yanaonekana kwa macho, Maendeleo hayatangazwi.
 
TSHs. Billion 11,267,070,127.77

Kweli!?
Mkuu jitahidi ukalione soko lenyewe alafu ndio upate pumzi ya kubisha,lile soko ni kama limechomolewa New York limepachikwa pale morogoro.

Alafu bilioni 11 mbona ndogo sana kuna watu wana mpaka trilion kwenye akaunt zao sasa jiulize wanafanyia nini.

Magufuli sio saizi yetu ndio maana thamani ya Pesa yetu anayotuonyesha tunanaishia kutoa macho tu.

Jibu lako na kile ulichonukuu, ni Mbingu na ardhi. Kiufupi, hukuelewa ambacho Trainee alimaanisha. Ni mahesabu zaidi.

Kuna tofauti ya Tsh bilioni 11 na TSHs. Billion 11,267,070,127.77
 
Alikuwa anakagua au ALIENDA kuona ujenzi wa soko la Morogoro?

Eti kukagua.

Ana fani ya UHANDISI MAJENGO?
Hichi Kichonge siku nyuzi zote anawapigia debe wakubwa wa chechemaa. Wenzake wala yeye hata ukatibu wa kijiji hajapewa. Watu kama hawa hukaa kimya maiti za ndugu zao zikizuiliwa hospitali. Hutamsikia akitia neno watoto wa shule za msingi wakirundikwa kwenye chumba kama panya wala hutamsikia wagonjwa wakikosa kutibiwa kisa hawana hela. Yeye kusifia tu.
Kuleni hilo soko.
Nyanya moja 300
Unga 2000
Mchele 2000
Sukari 3000
Sifia na kupanda bei basi
 
Back
Top Bottom