BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Baruani Mshale ambaye ni Mkurugenzi wa Mikakati na Mafunzo kutoka TWAWEZA amesema kitendo cha Watu na hasa Vijana kutoshiriki katika masuala ya Uchaguzi kinasababisha maamuzi yanayofikia kuchaguliwa kwa Viongozi ambao hawawataki.
Amesema "Tuchukulie mfano wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pale mtaani kwenu au kijijini kwako mnatakiwa kuchagua viongozi. Kipindi cha Uchaguzi kimefika ukaona wanaogombea watafanya yaleyale tu, ukaamua usishiriki, kitakachotokea ni kwamba wale wachache watakaoshiriki watakwenda kukuchagulia wewe Kiongozi".
Akizungumza kupitia PowerBreakfast ya CloudsFM , Baruani ameongeza kuwa "Hukushiriki halafu yule atakapokuja kuwa Kiongozi ndio utaanza sasa kuona matokeo ya yule Kiongozi atakapofanya vitu ambavyo havikufurahishi wewe".
"Tuchukue miaka 10 iliyopita wakati wa mchakato wa katiba mpya Watanzania wengi sana walikuwa wakifuatilia, walikuwa wanajua kinachoendelea kuhusu mijadala ile na walikuwa wanajua kuna bunge la katiba mpya limekaa na linajadili kwa sababu ilikuwa linaoneshwa katika vyombo vya habari.
"Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 ilitamkwa wazi kwamba hata bunge live halikuwepo kwahiyo wananchi wasingeweza kuona bunge lao linajadili nini, masuala muhimu sana kwao. Pia ilitamkwa na Kiongozi aliyekuwepo kwamba uchaguzi ulikuwa umekwisha siasa ziwekwe kando tushughulike na shughuli za maendeleo"
"Watu wengi wanaogombea nafasi za uongozi wanatuaminisha kwamba wao ndio watakuwa mwarobaini wa matatizo ambayo yapo pale, wakati ushiriki thabiti wa mwananchi ni kitu muhimu sana katika hayo maendeleo.
"Bila ushiriki wa mwananchi unaweza ukafikiri wewe hivi ulivyoviweka ndio vipaumbele vya kero hasa zinazowakabili wananchi wa lile eneo lakini kumbe Wana kero zao.Ili kuleta maendeleo ya kweli ni muhimu kuchagiza ushiriki mzuri wa wananchi"
"Mfano wa uchaguzi wa serikali za mitaa pale mtaani kwenu au kijijini kwako manatakiwa kuchagua viongozi kipindi cha uchaguzi kimefika ukaona kwamba hao wanaogombea wataleta yaleyale tu, ukaamua wewe usishiriki kitakachotokea ni kwamba wale wachache watakaoshiriki watakwenda kukuchagulia wewe Kiongozi"