Dkt Ananilea Nkya: Nafasi za ubunge wa Viti Maalum zifutwe kwa sababu zimeanza kutumika isivyostahili. Zilianzishwa ziwe za Mpito sio za kudumu

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
365
563
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Dk Ananilea Nkya amesema nafasi za ubunge wa Viti Maalum zilianzishwa kwa kipindi cha mpito kutokana na uwakilishi mdogo wa wanawake.

Dkt Nkya amesema hali imebadilika tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 (miaka 42), wanawake wametumia nafasi hiyo ipasavyo huku lengo la kuanzishwa kwake kwa muda likikiukwa badala yake nafasi hizo zimeanza kutumika isivyostahili.

1716653771064.png
“Hivyo viti wanawake tulivipigania kweli kweli lakini viliwekwa kwa transition (kwa muda) kwa sababu wakati ule miaka ya 1970 hadi 1980 utafiti uliyoonyesha wanawake walikuwa wanaogopa kwa sababu mfumo ulikuwa unawanyima wanawake kufanya kazi nje ya nyumbani” amesema Dkt Nkya.

Dkt Nkya ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto amesema uzoefu unaonyesha kuna udhalilishaji kwa wanawake wanaogombea nafasi za viti maalum ndani ya vyama vya siasa huku baadhi ya viongozi katika vyama hivyo wakivitumia kwa maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 25, 2024, wakati wa mdahalo wa wazi wenye lengo la kujadili mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania ulioitishwa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

“Katika kuvipata inakuwa kwa mbinde wanavipata kwa njia ya unyanyasaji, ni wachache wanavipata kwa njia ya uhalali. Pia hawana fursa sawa na wabunge wa kuchaguliwa majimboni mfano nafasi ya Waziri Mkuu hawezi kuingia mbunge wa viti maalum,” amesema Nkya. Idadi ya wabunge wa viti maalum bungeni inafika 113 wanaoigharimu Serikali zaidi ya Sh200 bilioni kila miaka mitano ya uchaguzi, Dk Nkya amesema wabunge hao pamoja na kutowajibika kwa wananchi, pia wanaiingiza Serikali katika matumizi yasiyohitajika.

Pia amesema endapo wilaya zitageuzwa kuwa majimbo idadi ya wabunge itapungua kutoka wabunge 393 hadi angalau wabunge 276 huku ukiokoa gharama kwa Serikali ya hadi Sh200 bilioni zinazotumika kulipa wabunge wa viti maalum, fedha inayoweza kugharamia Bima ya Afya kwa watoto chini ya miaka mitano.

1716653857958.png
Naye Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa, Deus Kibamba, mwarobaini wa changamoto ya viti maalum bungeni itaondolewa kwa kuanzishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, mchakato alioutaja kwamba utaondoa mambo yaliyopitwa na muda.

Ili kufikia suala hilo, Kibamba amesema Katiba itakayoanzishwa inatakiwa kuja na mapendekezo ya kufumua na kupunguza mamlaka ya Rais ikiwemo ya kiuteuzi na kuyarejesha kwa wananchi huku akidokeza kwamba ili suala hilo lifanikiwe halihitaji utashi wa kisiasa bali kijamii.
1716653835974.png
Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Ziwa, Steven Kitale ameshauri kuanzishwa Katiba ambayo inashughulikia mapungufu ya kisheria yaliyopo katika taasisi za nchini likiwemo Bunge.

“Mapendekezo haya yatasaidia kujenga msingi imara ya Katiba inayozingatia matakwa ya wananchi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Ni rai yetu kwa Serikali na viongozi wetu kuyazingatia ili kuwapunguzia wananchi mzigo na kurejesha uwajibikaji katika kodi inayotolewa na wananchi,” amesema Kitale.

1716653875283.png

Mbona inajulikana kwamba viti maalum ni mzigo tu. Wametia pamba tu masikioni wanabebana kwenye ulaji.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Dk Ananilea Nkya amesema nafasi za ubunge wa Viti Maalum zilianzishwa kwa kipindi cha mpito kutokana na uwakilishi mdogo wa wanawake.

Dkt Nkya amesema hali imebadilika tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 (miaka 42), wanawake wametumia nafasi hiyo ipasavyo huku lengo la kuanzishwa kwake kwa muda likikiukwa badala yake nafasi hizo zimeanza kutumika isivyostahili.

“Hivyo viti wanawake tulivipigania kweli kweli lakini viliwekwa kwa transition (kwa muda) kwa sababu wakati ule miaka ya 1970 hadi 1980 utafiti uliyoonyesha wanawake walikuwa wanaogopa kwa sababu mfumo ulikuwa unawanyima wanawake kufanya kazi nje ya nyumbani” amesema Dk Nkya.

Dk Nkya ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto amesema uzoefu unaonyesha kuna udhalilishaji kwa wanawake wanaogombea nafasi za viti maalum ndani ya vyama vya siasa huku baadhi ya viongozi katika vyama hivyo wakivitumia kwa maslahi yao binafsi.

Bao moja ubungr miaka 5, cc mbowe ila hakupata basi hasiraaa covid19
 
amekuja kugundua kuwa wameongeza mlango wa machawa wengi kwelikweli wa ccm. si huyuhuyu mama kipindi kile cha GENDER alipambana sana wabunge wateuliwe huyu?
 
Ameongea ukweli mtupu viti maalum hazina maana.
 
..Tume ya Warioba ilipendekeza bunge la muungano liwe na wabunge 150.

..Na walipendekeza liwe na wabunge wanawake 75 na wanaume 75.
 
Tunafunga mkono na miguu, viti maalumu viondolewe
 
Back
Top Bottom