Viti Maalum wanamaliza hela za wananchi bila sababu

Selemani Sele

Senior Member
Feb 25, 2023
157
421
Kwa msaada wa wiki pedia

Viti maalum vya wanawake ni nafasi bungeni zinazotolewa kwa utaratibu unaopatikana katika nchi mbalimbali na unaolenga kuongeza idadi ya wanawake na athira yao katika bunge na mabaraza na kwa njia hiyo katika siasa ya nchi hizo kwa jumla.

Kuna nchi nyingi za dunia zilizochukua hatua za kuongeza nafasi za wanawake serikalini kulingana na mkataba kuhusu ufutaji wa ubaguzi wote wa wanawake (Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women) uliosainiwa na mataifa 189 tangu kuanzishwa mwaka 1981 na kuimarishwa na azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2011.

Ambapo kwa Tanzania imeidhinishwa kwenye kanuni 66 1 (b) ya katiba ya Tanzania inaidhinisha wanawake kupewa nafasi ya viti maalum kama ifuatavyo;

"Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais,watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;

Tukirudi kwenye heading hapo juu mimi kama Mtanzania mwenye damu ya kuipenda nchi yangu nikafanya uchunguzi na kudadavua kazi za viti maalum kwa kina, kwa mtazamo wangu naona inamalizia serikali hela ambayo ingeendeleza kwenye miradi ya taifa kwa ajili ya maendeleo kama kilimo na elimu badala ya kuhangaikia headless posts ambayo hatujui kazi zake ni zipi haswa.

Kwa maana viti maalum wapo 113 ambapo 94 wapo CCM na wengine wapo 19 wapo vyama vya upinzani ambapo kwa utafiti niliofanya naona ni upotevu wa rasilimali na kodi za wananchi.

Sababu za kukataa viti maalum wengi
A. Nini kazi ya viti maalum wakati mbunge yupo anaiwakilisha jimbo lake kwa nn kila mkoa kusiwe na viti maalum mmoja badala ya kuwa kila jimbo maana kati kutatua kero mbunge atakuwa kashazitatua viti maalum atamalizia shida ndogo ndogo hivyo ni hasara.

B. Mishahara mikubwa ambayo inaweza geuzwa hela ya miradi ya visima na madarasa,mshahara wa mbunge ni mil 12 zidisha 113 mara miaka mitano inakuja Bilioni 81.3 ya mishahara na kitega uchumi bàada ya ubunge cha Billion 22.6 na viposho posho vya  Billion 5 jumla ambayo itakuwa Billion 109 ambayo inaweza jenga madarasa zaidi ya 1000 na furniture ambazo zitasaidia watoto wasome kwa amani na kwa raha

Nini kifanyike ili kuleta usawa
A. Mishahara ipunguzwe
Viti maalum walipwe mshara tofauti na wabunge kwakuwa kazi wanazoonesha zinafanywa na wabunge wa majimbo yao hii itafanya serikali isave hela kwa matumizi mengine.

B. Idadi ya viti maalum.

Kupunguza idadi ya viti maalum kuja kuwa 35 hii kwa maana uwakilishi kwa mkoa kwa kila viti maalum ambapo itasave hela asilimia 50 ambayo.itajenga visima,madarasa, zahanati na mahitaji muhimu megine kuliko kuwekeza kwenye watumishi kikatiba kiroho ni upepo.

Roast me as you can but i have spilled the truth.
 
Back
Top Bottom