Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

ulizaliwa peke yako na utapokufa utakufa peke yako, usipoteze nafasi yako na muda wako kwa ajili ya kutetea watu ambao watakuja kukugeuka baadae, yu wapi Gadaf aliyeijenga libya na kuwapa kila k2 walibya? Ulimboka kaa na familia yako utulie achana na hayo mambo, Afrika hakuna shujaa.

Hakuna jambo lisilo na mwanzo Dr. Uli anaweza akatokea kuwa shujaa wa kwanza Afrika!!!
 
Namshauri huo ushahidi na maelezo yake aweke kwenye maandishi au video na asambaze sehemu mbali mbali kabla ya kwenda habari maelezo. Namna nyingine sioni mbele yake kuna nini zaidi ya kuvuruga ushahidi na ahadi kem kem za kijinga. Hata Mwakyembe alianza hivi hivi then aliishia na usemi wa "Tuwaachie vyombo vya dola"
 
Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.

Mtu mzima hatishiwi nyau ww eboooo!
Hivi hunaga cha kuandika?
 
Hapo ni mtego mkubwa sana kwa Ulimboka. Akikubali tu suluhu na TISS, amekwisha. Wanaweza kumwahidi pesa nyingi ili asitoe taarifa yeyote ya kuivua nguo serikali Lakini ajue kuwa vyombo vya dola havitakaa vitulie huku vikijua kabisa kuwa kuna mtu ana siri kubwa, na hawajui kama mtu huyo hatakuja itoa siri hiyo hadharani. Uhakika wa kuwa taarifa hiyo haitatoka ni kumwondoa. Ameokoka mara hii kwa mkono na huruma ya Mungu lakini akikubali hongo, itakapokuja nyingine, kamwe hatapona.
Hamna kitu hapo hakuna chochote cha ajabu atakacho ongea ,zaidi ya kustaajabisha taifa kwani kwa mwakyembe ilikuaje?

Aliombewa sana na wadau hasa hapa jamvini kulikuwa na thread kibao zilizo anzishwa ili kumwombea apone lakini alipopona na kurejea nchini mambo yakawa tofauti kabisa.

Kapewa kijishavu katulia tuli? Sasa na huyu nae atakuja kuongea mambo ambayo ni story za kufikirika kabisaa na kustajabisha.

Hii ndio tz ilio jaa vioja bwana.Hana ubavu wa kupanua domo lake na kumwaga mboga. Serikali inajua nini imefanya na nini itafanya juu ya Ulimboka ndio maana imetulia tuli.

Tatizo letu njaa ndio inayotumaliza na ndio huwa inatufanya tuonekane wanaharakati na wanaukombozi kumbe si lolote si chochote tukishibishwa kidogo tu hata na kiporo chari.
 
huyu ulimboka naona kalewa sifa sasa, kichwa kimemvimba!
 
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.

Hataki familia yake iulizwe cuz hawajui.........
 
"Mtu yeyote ambaye hatafanya kitu chochote, ataishi, na hatimaye atakufa, bila kufanya kitu chochote" Hata kama dr. hatasema kitu chochote, ataishi, na mwisho wake ni kifo, bila kusema kitu chochote. Bora kufia haki kuliko kuishi kwa woga.
 
huyu ulimboka naona kalewa sifa sasa, kichwa kimemvimba!

Unaona eee bora akae kimya coz hata akisema haitaongezea watanzania matonge ya ugali,labda kidogo afungue kesi mahakama ya haki za binadamu ya kimataifa,sababu huo ukweli anaotaka kuusema asilimia 99 unajulikana,sasa hiyo moja ya nini? Au ameshasahau.....anatuzingua...
 
Mkullya Damu, Kuna maana gani ulimboka Kusema anaujua ukweli halafu akashindwa kuuweka wazi? ndiyo yale yale kwamba sisi wabongo ni waongeaji sana kuliko vitendo. sasa serikali inajua wazi kabisa kwamba wengi wa watanzania ni wasahaulifu sana. nadhani ndiyo mwanzo wa huyo jamaa kusema atauweka ukweli wazi baada ya siku 40. sasa nikawa najiuliza kwanini ziwe siku 40 na sio leo ama baada ya siku mbili?!! yupo kwenye swaumu au ni kipi hasa ?. mtu mwongo utamjua tu. yaani huyu jamaa hakuna analojua, siku zote hizo 40 atakuwa anapika uongo wa kuja kutulisha.
 
Last edited by a moderator:
Dr. Ulimboko kuficha ukweli ni dhuluma kwa wananchi tuliokuchangia matibabu yako. Wengi tunahisi serikali ilikufanyia ujasusi, hivyo tunataka kuwajua hao majasusi.

Dr. Ulimboko kama umetishwa au umehaidiwa cheo na serikali, kumbuka ni serikali hiyo hiyo iliokutesa na inaogopa nguvu ya umma. Dr.Ulimboko! kama Mh Mwakyembe angeweka ukweli hadharani, yasingekutokea yaliyokupata maana serikali ni DHAIFU. UDHAIFU wa serikali, uliwatumia watu wake ambao walishindwa kutekeleza kazi 100% kwako na Mwakyembe.

Dr. Ulimboko kuficha maradhi, ni kueneza maradhi maana we don't know who is going to be a next victim? Dr. Ulimboko sasa wakati umefika kusema ukweli, kwani ni haki yetu kuujua. Dr. Ulimboko remember " GOD do not like ugly" ulipona kwa dua zetu na utaangamia kwa dua zetu
 
Kasema ukweli anaujuwa yeye mwenyewe na yuko eda ya siku 40 kabla hajasema lolote kuhusu kichapo alichochezea.

Ni matumaini yangu kuwa hatarudia. Hata hizo fedha alizozifata leaders usiku hana hamu nazo. Angoje chenji ya mchango wa matibabu, hiyo ni halali yake, tena msimzike mnaozishikilia, msione karudi mkasema ndio basi kisha pona mumtie ndani chenji yake. Inabidi baada ya muda aende tena akaone na madaktari wake waliomtibu waone maendeleo yake na.
 
Ha ha ha ha ha ha...halafu Mwakyembe hajakoma.
 
Dr ulimboka yuko smart kuliko mwakyembe.Ulimboka ni 'war strategist' tusubiri tuone.
 
Kasema ukweli anaujuwa yeye mwenyewe na yuko eda ya siku 40 kabla hajasema lolote kuhusu kichapo alichochezea.

Ni matumaini yangu kuwa hatarudia. Hata hizo fedha alizozifata leaders usiku hana hamu nazo. Angoje chenji ya mchango wa matibabu, hiyo ni halali yake, tena msimzike mnaozishikilia, msione karudi mkasema ndio basi kisha pona mumtie ndani chenji yake. Inabidi baada ya muda aende tena akaone na madaktari wake waliomtibu waone maendeleo yake na.
Acha utani, hapa si mahala pake, we are serious about the TRUTH and we can handle it. Hakuna eda ya 40 days. Hatukupewa 40 days kukuchangia kwenda kutibiwa, nor we are not going to wait that long.
 
Mimi nilishasema kwenye thread moja kuwa dr uli lazma awekwe mfukoni wa sirikali vinginevyo atalazwa mahala pema na nilitoa ushauri dr uli akamwulze mwakyembe ampe ushaul kabla ya kufungua kinya na ndicho kilichotokea.Hii ndo bongo bhana
 
Kasema ukweli anaujuwa yeye mwenyewe na yuko eda ya siku 40 kabla hajasema lolote kuhusu kichapo alichochezea.

Ni matumaini yangu kuwa hatarudia. Hata hizo fedha alizozifata leaders usiku hana hamu nazo. Angoje chenji ya mchango wa matibabu, hiyo ni halali yake, tena msimzike mnaozishikilia, msione karudi mkasema ndio basi kisha pona mumtie ndani chenji yake. Inabidi baada ya muda aende tena akaone na madaktari wake waliomtibu waone maendeleo yake na.
How could you be so insensitive to a plight of a fellow human being? What makes you think that you are safe? Particularly when the "jungles rule returns?
 
Dr ulimboka yuko smart kuliko mwakyembe.Ulimboka ni 'war strategist' tusubiri tuone.

Baada ya siku arobaini? Anakusanya ushahidi nini? Au kwa sasa hawezi kunena bado afya haijatengemaa? Watu tuna mambo na vijambo kwelikweli ngoja baada ya siku arobaini aje amtambe Mlundi kuwa ndiye aliyemteka sijui tutasemaje?
 
Back
Top Bottom