Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Kwa taarifa yako Mwanahalisi ilimfuata Dr Ulimboka kule alikokuwa akitibiwa na kumuhoji kwa kina. Kwa hiyo yote waliyoyaandika yalitoka mdomoni mwa Dr na wakayathibisha kupitia rekodi za Tigo ambazo zimesababisha Wafanyakazi 30 wa Tigo kitengo cha IT kumwaga unga kwa kuvujisha habari nyeti.

Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.
 
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.
Ritz at work
 
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.
Hapa umefuka moshi wa kuni mbichi
 
Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, ameibuka toka mafichoni na kuwaambia Watanzania kwamba anayejua mpango mzima wa kumteka, kumtesa na kumpiga ni yeye pekee.

Dk. Ulimboka ambaye juzi alikuwa mafichoni, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio zima la kutekwa, matibabu yake nchini Afrika Kusini na mambo mengine yaliyojiri wakati akiwa nje.
Huku akiwa makini kuchagua maneno, Dk. Ulimboka alisema waandishi wa habari wasiihoji familia yake wala mtu mwingine yeyote, kwani ukweli wa tukio lake anaujua yeye mwenyewe.

Dk. Ulimboka ambaye tangu arejee amekuwa akiishi kwa kujificha, amewataka Watanzania kuvuta subira kwani anajipa muda wa kueleza ukweli wa tukio la kutekwa kwake.

“Najua waandishi wa habari na Watanzania wengi wanataka kujua ukweli ambao ninao mwenyewe, lakini hakuna sababu ya kuwa na haraka, wakati ukifika nitazungumza yaliyonisibu,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari uliolitikisa taifa hivi karibuni, hivi sasa anaishi kwa hofu na kujificha huku akichagua marafiki wa kukutana na kuzungumza nao. Kiongozi huyo, yuko makini pia katika kuzungumza na simu, na amekuwa akipokea zile za watu anaowajua tu.

Alipobanwa ili azungumze kwa ufupi juu ya wanaohusika na kutekwa kwake, Dk. Ulimboka alisisitiza kuwa hayuko tayari kueleza ukweli huo kwa sasa na kuongeza kuwa muda ukifika ataeleza kila kitu.

Polisi wapanga kumhoji

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova ametoa kauli inaonesha kwamba vyombo vya usalama vitamuhoji Dk. Ulimboka.

Kova ambaye alikuwa akizungumza na gazeti hili, lililotaka kujua msimamo wa vyombo vya usalama katika kulishughulikia suala la Ulimboka, hasa baada ya kurejea kutoka kwenye matibabu nchini Afrika Kusini, alisema kwamba taratibu za kipelelezi zitafuatwa.

Wakati Kova akizungumza hayo, chanzo kimoja cha habari toka kwa maofisa wa ngazi za juu wa polisi kilidokeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika uchunguzi wake atabaini kuwa kuna shahidi muhimu anahitajika, atahojiwa.

Hata hivyo Kova alisisitiza kuwa; “watu wakipeleleza hawasemi ila tambua tu kwamba taratibu za upelelezi zitafuatwa.”

Tayari taarifa na mwenendo wa tukio zima zinaonesha pasipo shaka kuwa, Jeshi la Polisi katika taratibu zake sasa linafikiria kumuita na kumuhoji Dk. Ulimboka ili liweze kuondoa maneno ya kusikia sikia.
Kuhusu kutajwa tajwa kwa mtu anayedaiwa kuwa ni ofisa wa Usalama wa Taifa wa Ikulu, Ramadhan Ingondhur kuwa alihusika na njama za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, Kova aliahidi kulizungumzia hilo siku ya Ijumaa.

Mbali na gazeti la MwanaHalisi kumtaja Ramadhan kuwa ndiye mhusika mkubwa wa kutekwa kwa Dk. Ulimboka, mwingine aliyeungana na msimamo huo ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa ambaye aliitaka Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na serikali ithibitishe hadharani juu ya mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

Dk. Slaa alisema chama chake kitaanzisha harakati za kutaka kujua ukweli wa nani anahusika kumteka Dk. Ulimboka. Mwanzoni mwa wiki, Dk. Ulimboka alirejea kwa kishindo nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, na kusema yupo tayari kuendeleza mapambano na kazi baada ya kupona kabisa. Dk. Ulimboka alikwenda Afrika Kusini Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.

Aliondoka nchini akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa kwa vile alikuwa kwenye hali mbaya kiafya, lakini alirejea akitembea kwa miguu na kuonekana mwenye afya njema.


Hiyo sentesi ya mwisho inaonyesha huko alikoenda kutibiwa kuna dawa na vifaa vya kisasa!
 
Dr. SU, vuta pumzi weka yote wazi bila chenga. Kova anatapatapa eti anataka aseme ijumaa hii. Ila kuna tetesi kuwa wanataka wamgeuzie kibao Dr. Ulimboka kwa kumsomea mashtaka. Tusubiri ila nimepata kwa mtu ninayemwamini. Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Huyu Ulimboka antafukiwa awataje haraka hao majangiri waliomteka ili awe huru, maana sasa watamwinda asipate mwanya wakuwataja. Akiwataja wao ndo watakuwa walinzi wake maaana Watanzania tutakuwa tunawajua na wakimzuru wataandamwa na watu wote! Taja haraka yaishe, waende sero tuanze biashara nyingine.
 
Uchunguzi wa nini kuhusu nini? Dr Ulimboka ndio muhusika na ndio aliyetekwa na kufanyiwa unyama na yeye mwenyewe ndio anakuambia ukweli wa yeye kutekwa anaujua mwenyewe huo uchunguzi wa Mwanahalisi ni wakwenu nyie...Watanzania wasubiri kauli yake kama huo uchunguzi wa Mwanahalisi ungekuwa wa kweli Dr Ulimboka si angesema Mwanahalisi wameishasema ukweli kutoka na uchunguzi wao, kulikuwa na haja gani tena kusema ukweli anaujua yeye.


walichokisema mwanahalisi ni ukweli.. na ulimboka anaposema anaujua ukweli, ukweli huo unaenda mpaka alipokuwa africa ya kusini pale wapuuzi wachache walipopenyezwa wakiwa na tube iliyoonyesha ni dawa ya meno kumbe ni sumu.. japo kwa nje ilionekana ikiwa na nembo ya colgate.. walihangaika wiki mbili na hawakupata chochotena wala hawakumfikia ulimboka..hilo ni moja tu kati ya mambo manne wapuuzi na washenzi hao waliyokuwa wamepanga kuyatekeleza huko..yote yaligonga mwamba..msitumie nguvu nyingi sana kupindisha mambo
 
walichokisema mwanahalisi ni ukweli.. na ulimboka anaposema anaujua ukweli, ukweli huo unaenda mpaka alipokuwa africa ya kusini pale wapuuzi wachache walipopenyezwa wakiwa na tube iliyoonyesha ni dawa ya meno kumbe ni sumu.. japo kawa nje ilionekana ikiwa na nembo ya colgate.. walihanagaika wiki mbili na hawakupata chochotena wala hawakumfikia ulimboka..hilo ni moja tu kati ya mambo manne wapuuzi na washenzi hao waliyokuwa wamepanga kuyatekeleza huko..yote yaligonga mwamba..msitumie nguvu nyingi sana kupindisha mambo

de'levis nimekusubiri sana hapa uje utoe ufafanuzi wa nini kiliendelea,
naamini wewe ni "mwanahalisi" wa humu JF...
 
Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.

Kwani wewe ni mmoja wa watekaji wa Dr Uli? Mbona lugha na mwenendo wa ulimi vinaonesha wewe ni miongoni mwa watekaji!
 
Dr Ulimboka ataongea muda ukifika.

Ingawa hii picha ya kihindi inachelewa kuanza, lakini muda wake ukifika picha ya kihindi itaanza tusiwe na haraka.

Tuendelee kumuombea Doctor afya yake iwe nzuri, na atakapoongea aseme ukweli mtupuuuu.
Mwanahalisi nao waliujuwa ukweli 90%, ndiyo maana wakafungiwa, habari walizotoa zilikuwa na details za kutoshaaa, walifanya kazi nzuri sanaaaa, ambayo serikali haikutegemea kutoka kwa wandishi wetu wa Tanzania na pia hawakuogopa kutoa details.
Binafsi nawaamini sana Mwanahalisi kwa hili jambo la Dr Ulimboka.

Doctor Ulimboka tulizana, upone vizuri halafu utakuja siku moja kutuhabarisha, ila ni lazima uwe muangalifu sana, maana serikali this time wakikupata watakuuwa hawatafanya kosa tena kama walilolifanya, watakuchoma moto au watakupiga risasi huo ni ushauri wangu kwa Doctor Ulimboka.

Kwa bahati mbaya sana serikali za kiafrika ni za kishenziiiiiiiiiiiiii sanaaaa, siyo hapa Tanzania, ni Afrika nzima mambo na michezo ni hii hii tuuu, serikali za kiafrika hazitaki kukosolewa wala kuelekezwa.

Nawatakia siku njema

ni serikali zote duniani,sio za kiafrika tu.fanya research au muulize Julian Asange wa wikileak ataprove ukweli huu.ukionekana kukopromise national security anything can happen to you hata kama ulikua uko kwenye haki.
 
Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.

wazo la kenge kwenye kundi la mamba .
 
Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.
Aaaa! Rama! naona umeibuka mafichoni.
 
Wakati wa kupata ma movie umewadia, sisye yetu macho tu!!
 
Kitu kilichotokea Dr.Ullimboka maadui zake sasa hivi wako kwenye mazungumzo nae ndio maana analeta siasa hataki kueleza kilichomtokea usishangae asieleze kabisa au akaeleza story tofauti na ile ya mwanahalisi.Manake maadui zake wanaweza kumweleza bwana samehe yale yalikuwa ni matatizo ya kiufundi wakampa shavu akatulia zake kimya.Ndio maana ameanza kuleta porojo.
Manake hili neno:Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi... limepigwa kiufundi sio ajabu ameambiwa aliseme ili kunarrow ushaidi.......................

Umeona mbali sana kijana wangu, napenda watu kama nyinyi mnaofikiria mbali.

Nitakutafuta nikuajiri unatufaa sana kwa kazi zetu za usafety.
 
Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.

Kauli hii inaonyesha nidhamu ya woga ambayo CCM na serikali yake ndiyo imefanikiwa sana kuijenga katika nafsi za watanzania walio wengi. Heri kufa kwa kutafuta haki kuliko kufa kwa woga. Hakuna mtu atakayeishi milele. Kuacha legacy ya ujasiri katika kupigania haki ni mafanikio makubwa kuliko kuacha legacy ya woga baada ya muda wa kuishi hapa duniani. Tutakumbukwa kwa lipi? TAFAKARI!!!!!
 
Back
Top Bottom