Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 16, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, ameibuka toka mafichoni na kuwaambia Watanzania kwamba anayejua mpango mzima wa kumteka, kumtesa na kumpiga ni yeye pekee.

  Dk. Ulimboka ambaye juzi alikuwa mafichoni, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio zima la kutekwa, matibabu yake nchini Afrika Kusini na mambo mengine yaliyojiri wakati akiwa nje.

  Huku akiwa makini kuchagua maneno, Dk. Ulimboka alisema waandishi wa habari wasiihoji familia yake wala mtu mwingine yeyote, kwani ukweli wa tukio lake anaujua yeye mwenyewe.

  Dk. Ulimboka ambaye tangu arejee amekuwa akiishi kwa kujificha, amewataka Watanzania kuvuta subira kwani anajipa muda wa kueleza ukweli wa tukio la kutekwa kwake.

  "Najua waandishi wa habari na Watanzania wengi wanataka kujua ukweli ambao ninao mwenyewe, lakini hakuna sababu ya kuwa na haraka, wakati ukifika nitazungumza yaliyonisibu," alisema.

  Hata hivyo, Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari uliolitikisa taifa hivi karibuni, hivi sasa anaishi kwa hofu na kujificha huku akichagua marafiki wa kukutana na kuzungumza nao. Kiongozi huyo, yuko makini pia katika kuzungumza na simu, na amekuwa akipokea zile za watu anaowajua tu.

  Alipobanwa ili azungumze kwa ufupi juu ya wanaohusika na kutekwa kwake, Dk. Ulimboka alisisitiza kuwa hayuko tayari kueleza ukweli huo kwa sasa na kuongeza kuwa muda ukifika ataeleza kila kitu.

  Polisi wapanga kumhoji

  Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova ametoa kauli inaonesha kwamba vyombo vya usalama vitamuhoji Dk. Ulimboka.

  Kova ambaye alikuwa akizungumza na gazeti hili, lililotaka kujua msimamo wa vyombo vya usalama katika kulishughulikia suala la Ulimboka, hasa baada ya kurejea kutoka kwenye matibabu nchini Afrika Kusini, alisema kwamba taratibu za kipelelezi zitafuatwa.

  Wakati Kova akizungumza hayo, chanzo kimoja cha habari toka kwa maofisa wa ngazi za juu wa polisi kilidokeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika uchunguzi wake atabaini kuwa kuna shahidi muhimu anahitajika, atahojiwa.

  Hata hivyo Kova alisisitiza kuwa; "watu wakipeleleza hawasemi ila tambua tu kwamba taratibu za upelelezi zitafuatwa."

  Tayari taarifa na mwenendo wa tukio zima zinaonesha pasipo shaka kuwa, Jeshi la Polisi katika taratibu zake sasa linafikiria kumuita na kumuhoji Dk. Ulimboka ili liweze kuondoa maneno ya kusikia sikia.

  Kuhusu kutajwa tajwa kwa mtu anayedaiwa kuwa ni ofisa wa Usalama wa Taifa wa Ikulu, Ramadhan Ingondhur kuwa alihusika na njama za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, Kova aliahidi kulizungumzia hilo siku ya Ijumaa.

  Mbali na gazeti la MwanaHalisi kumtaja Ramadhan kuwa ndiye mhusika mkubwa wa kutekwa kwa Dk. Ulimboka, mwingine aliyeungana na msimamo huo ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa ambaye aliitaka Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na serikali ithibitishe hadharani juu ya mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

  Dk. Slaa alisema chama chake kitaanzisha harakati za kutaka kujua ukweli wa nani anahusika kumteka Dk. Ulimboka. Mwanzoni mwa wiki, Dk. Ulimboka alirejea kwa kishindo nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, na kusema yupo tayari kuendeleza mapambano na kazi baada ya kupona kabisa. Dk. Ulimboka alikwenda Afrika Kusini Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.

  Aliondoka nchini akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa kwa vile alikuwa kwenye hali mbaya kiafya, lakini alirejea akitembea kwa miguu na kuonekana mwenye afya njema.

   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hii picha mbona inachelewa kuanza mwishoni tutasinzia
   
 3. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

  Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

  Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Kova anatapatapa, mara aseme habari za Ulimboka ziko mahakamani tusizizungumzie, mara aseme ye mwenyewe atazizungumzia ljumaa. Huyu jamaa hana weledi
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

  R.I.P MWANAHALISI.
   
 6. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  unamtisha nani sasa?
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  This yet another fieces
   
 8. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii kweli picha ya kihindi..! Huko mafichoni ni wapi ambako mwandishi amefika.?
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mbona hizi ni kama vile pumba tupu?
   
 10. u

  ureni JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kitu kilichotokea Dr.Ullimboka maadui zake sasa hivi wako kwenye mazungumzo nae ndio maana analeta siasa hataki kueleza kilichomtokea usishangae asieleze kabisa au akaeleza story tofauti na ile ya mwanahalisi.Manake maadui zake wanaweza kumweleza bwana samehe yale yalikuwa ni matatizo ya kiufundi wakampa shavu akatulia zake kimya.Ndio maana ameanza kuleta porojo.
  Manake hili neno:Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi... limepigwa kiufundi sio ajabu ameambiwa aliseme ili kunarrow ushaidi.
   
 11. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  jk alisema serikali haihusiki wakati naye haujui ukweli, maana anayeujua ni ulimboka peke yake, thubutu basi kumwambia rip!
   
 12. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  vuta subira mkuu tuone atafunguka lini na atafungukaje?
   
 13. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Dr Ulimboka kwa sasa apumzike baada ya matibabu, hakuna udharura katika kuongea kilichompata muda ukifika atasema. Tunaendelea kukuombea ili hatimaye uemdelee majukumu yako.
   
 14. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nnachoamini kwa jinsi alivyoponea tundu la sindano,na hali ya vyombo vyetu vya usalama ilivyo anahitaji mda wa kujipanga,ila kama anamawazo tofauti na nnampa pole.
   
 15. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  ni kule ambako wewe hujafika, mbona jibu lake rahisi tu.
   
 16. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu chupi zimelegea safari hii. Ndio maana nilisema kama kova Amefunga Ramadhan basi funga yake ni sifuri kwa Mwenyezi Mungu.
   
 17. u

  ureni JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Utasubiri mpaka yesu ashuke lakini hiyo ndio fact itakua ni porojo tu maadui zake wanakaa nae mezani wanayamaliza kiutu uzima.
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wewe, ni lazima aseme ukweli ili isije ikatokea tukasikia tena kirahisirahisi kwamba Radhia Sweety ameuawa msitu wa pande na watu wa Ikulu, kwasababu tu huwa anachangia kwenye mijadala ya JF against Serikali
   
 19. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaweza kuwa kweli mkuu.
   
 20. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hakuna wa kuogopwa zaidi ya Mungu,nidhamu ya uoga na kumsujudia mwanadamu mwenzako ni mbaya na dhambi mbele ya Mungu,walishashindwa kumuangamiza mara ya kwanza sasa ni zamu yao kupata pigo takatifu ambalo familia zao hawataka kuja kusahau
   
Loading...