Dk. Nchimbi tulia! Mwosha huoshwa

Mkuu naona umewadhamiria hasa!

Mkuu sijamdhamiria mtu, ila wao ndio wamenidhamiria maana wanadai wananijua sana kwamba ninasema uongo, sasa na mimi ninasema hivi ninawajua sana, ni waongo na wanafiki pia, na huwadaganya hata wake zao na ushaidi ninao, na wake zao ninawajua, sasa waamue kusuka au kunyoa, wako watu watatu wanafikiri kukaa nyuma ya internent na kubadili mnajina hapa frum ni ujanja sana, ninawaambia tu kuwa ninawajua sana, sasa either tukate ishus za taifa, au wakitaka mengine nipo tayari, au tushiriki hapa JF kwa kuheshimiana.
 
Eh! watu mmesha shikana pabaya nini?

Tatizo ni kwamba ninyi ni panzi na hapa mpo nyikani mkiendeleza vita yenu faida yote inamrudia MH Mwewe. Mwewe wala hatahahitaji kuflip mbawa ili awatie kinywaji kama side dish, ni kudive na kuwalamba tu.
 
wafuatao ndo wanotarajiwa kugombea mpaka sasa taendelea kuwataarifu wanapokuja new comers.
1;VAILET MZINDAKAYA
2;BENO MALISA
3;HUSEN MOHAMED
4;JERRY SLAA
5;NAPE NAWIYE
6;ZAINAB KAWAWA
7;EDWIN SANDA
8;EDWIN MTAKA
Wana JF wenzangu hao ndio wanosemwa semwa kua wanataka kumrithi Dk Nchimbi

Hao sio watu wa Nchimbi. Infact ndio wanaompa Nchimbi wakati mgumu, kwani majina ya wazazi wao na pesa za wizi pluss network ya wazazi wao vyote hivyo vinamfanya Nchimbi, kutokuwa na chaguo zaidi ya kuwaonya ndugu na jamaa zao wasiingilie uchaguzi wa UVCCM.

Mtu wa Nchimbi ni Francis Isaack Mtinga ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM Singida. Kwa sasa amepewa kazi makao makuu nafikiri Utawala, ili apate nafasi ya kujitengenezea mazingira ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu. Tatizo wajanja walishajua chaguo hilo la Nchimbi, hivyo walimfanyia kweli kwenye uchaguzi wa CCM Singida mwaka jana. Alijaribu kuomba nafasi kadha na zote walimpiga chini hii ikiwemo NEC taifa kupitia UVCCM.

Matokeo ya uchaguzi huo mwaka jana, vimemweka kwenye wakati mgumu sana Bw Nchmbi kama ilivyo kwa Bw Francis. Hivyo kumweka makao makuu huenda kukamweka karibu na watendaji wa UVCCM mikoani na hivyo kumrahisishia kazi kwenye uchaguzi.

Tatizo kubwa analopata Bw Nchimbi, ni tetesi kuwa huenda Ridhiwani Kikwete akashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi kuhakikisha swahiba wake Beno Malisa anaukwaa Uenyekiti, hili huenda likawa na baraka za JK mwenyewe na mawaziri vijana.

Kwa upande mwingine Nchimbi anaendelea kukimbia kivuli chake, kwani hana uhakika na kina Frank Uhaula wataingia kwa gia gani kwenye uchaguzi huu. Pia Nape Nnauye kama akiingia kwenye kinyanyiro, nafasi ya Bw. Mtinga itakuwaje. Lakini yote kwa yote, ngoja tuangalie haya mambo yataishia wapi.
 
kaka umetumia kauli kali kua KUNA WATU WANA PESA ZA WIZI,ungetutajia wenye pesa za wizi tuwajue kama nchimbi anapinga hao wenye pesa za wizi ni jambo jema
 
Duh,
yaani katika post yote hiyo umeona "pesa za wizi" tu! anyway, kuwapinga wezi ni jambo jema, lakini kuwa mmoja wa wapigia debe mafisadi kunaweza kuondoa dhana nzima ya dhamira yako pale unapoamua kuwapiga vita wale ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa washirika wako. Kimsingi nachotaka kusema hapa ni kwamba: Kupiga vita wezi ni jambo la maana iwapo tu wewe mwenyewe hutumiki kama kinga ya kuwakingia kifua wezi wangine. Kinyume cha hapo tunaweza kuita undumilakuwili.
 
Ubavu wa kuweka mwenyekiti mpya wa vijana ccm, Nchimbi hana huo ubavu, in fact haya makelele yake ni debe tupu, angekuwa na huo uwezo, basi angekuwa katibu wa ccm kama alivyokuwa akililia,

Mwenye ubavu wa kumuweka mtu anayemtaka hapa ni Rostam, yeye peke yake ndiye anayewadai karibu viongozi wengi hela zake alizowakopesha kwenye chaguzi mbali mbali, anayemtaka ndiye atakuwa, maana originally hata Nchimbi alipewa na yeye.

Nchimbi alipokuwa na ubavu, alikuwa hapigi kelele kwenye public, alikuwa akifanya chini chini, sasa kulikoni safari hii na makelele?
 
Nimesoma kwa makini maelezo yote juu ya Nchimbi na UVCCM,inawezekana kuna habari waungwana hawana,wacha nizitoe hapa muone jinsi mambo yavyokwenda.
-Kwanza orodha iliyotolewa juu ya wagombea nadhani itaongezeka,lakini tatizo kubwa la Nchimbi ni namna gani atamzuia Nape kumrithi maana alishaapa kwamba akiwa hai atahakikisha Nape hawi mwneyekiti wa UVCCM.
-Kwahiyo katika orodha hiyo yuko tayari kumbeba yeyote kwa makubaliano ya kulinda maslahi yake UVCCM kwani anauhakika Nape atamuumbua pale kwa yale alofanya.
-Nijuzi tu Francis Isack ambaye alikuwa chaguo lake no. moja katangaza kwenye kikao rasmi(baraza kuu la UVCCM) kikao cha Ffebruary Dodoma kuwa hatagombea tena,hii ikiwa ni baada ya kupewa Ukaimu Katibu Mkuu wa UVCCM(T) na baada ya kutathimini kapigwa Ujumbe wa mkutano mkuu Singida,kapigwa wekahazina CCM mkoa wa SINGIDA na kapigwa vibaya NEC,so hana chance tena.
-Nchimbi kwa sasa kawekeza kwa Beno Malisa ila kwa siri kubwa maana anajua kumuunga mkono hadharani ni kumuharibia,analijua hili na analitekeleza kwa makini sana.Mkaubaliano ni kuwa baada ya Beno kushinda katibu mkuu wake ni Francis Isack so Nchimbi atakuwa kapitisha kete zake zote,ndo mpango uliopo. N a lengo hapa ni kulinda mkataba wa kifisadi aloingia Nchimbi na Francis kwa upande mmoja na Shubash Patel kwa upande wa pili juu ya mradi wa ukarabati wa makao makuu ya Umoja wa vijana hasa kiwanja cha nyuma ya jengo kuu la makao makuu ya umoja huo.
-Lakini isitoshe kuna habari kuwa katika mpango huu Lowasa anahusika kwa asilimia mia moja.Hata habari za kutoka ndani ya kikao cha baraza kuu la Uvccm taifa cha February ulitokea mvutano mkubwa kati ya NCHIMBI washabiki wake na Nape na washabiki wake kwa upande wa pili,hoja zikiwa mbili kubwa,
1.Hoja ya namna mradi wa ukarabati wa makao makuu ulivyo na utata Nape akitaka makataba uwekwe hadharani kwa baraza kuu na ujadiliwe na habari za kutoka kambini kwake zilieleza kuwa wao wanapinga mkataba wa UVCCM kupewa 25% tu ya mapato na 75% kuchukuliwa na mwekezaji for life,wakidai kuna harufu ya rushwa tena ya 3bill. kwa Nchimbi na Francis ambazo zinaaminika kuja kutumika wakati wa uchaguzi mwezi octoba.Lowassa kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa uvccm anabaraka zote kwa mradi huo wa ki richmond.
2.Mvutano wa pili ulitokea pale kambi ya Nape ilipotaka baraza kuu litoe tamko la kukipongeza chama kwa kumanage politics wakati wa sakata la Richmond,na kupongeza uteuzi wa mizengo,ndipo nchimbi alipokuja juu na kudai hawajui yaliyotokea bungeni hivyo chini ya uenyekiti wake hawezi kukubali kutoa tamko hilo.
 
Name Emmanuel Nchimbi
Surname Nchimbi
First Names Emmanuel John
Alternate Name
Title Dr
Country of Birth Tanzania

POSITIONS

Ministry of Defence & National Services
Deputy Minister of Defence & National Service
2008
Ministry of Labour, Employment & Youth Development
Deputy Minister of Labour, Employment & Youth Development
2006-2008
Ministry of Information, Sports & Culture
Deputy Minister of Information, Sports & Culture
200-2006

Songea Mjini Constituency
MP for Songea Mjini
Date of Birth
24 Dec 1971
Political Affiliation
CCM

EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD
Mzumbe University MBA (Finance & Banking) 2001 2003 MASTERS DEGREE
CommonWealth Open University MSc. (Management) 1999 2001 MASTERS DEGREE

Institute of Development Management - Mzumbe Advanced Diploma in Administration 1994 1997 ADV DIPLOMA
Forest Hill Secondary School A-Level Education 1991 1993 HIGH SCHOOL
Sangu Secondary School Secondary Education 1989 1990 SECONDARY
Uru Seminary Secondary Education 1987 1989 SECONDARY
Oysterbay Primary School Primary Education 1980 1986 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Regional Administration and Local Governments (TAMISEMI) District Commissioner 2003- 2005
National Environment Management Council-NEMC Administration Officer 1998 2003
--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Political Committee(Bunda)
2003-2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM Chairman of Youth (UVCCM) 1998 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of National Executive Council(NEC) 1997 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Council 1997 2002
--------------------------------------------------------------------------------
SPECIAL SKILLS
Skill Name or Description Years Experience Acquired Through Skill Level
No items on list
--------
Source:http://www.afdevinfo.com/htmlreports/peo/peo_580.html

Ndugu Nchimbi alisoma degree tatu kwa wakati mmoja (simulteneously) kuanzia 2001-2003. Dedree mbili za masters na PhD. Wana JF, nadhani inabidi tuelezwe inawezekanaje hii, kama siyo uongo au kununua vyeti?
 
HAPA JF MMOJA MMOJA AJIANDAE........!(sipotoshi mada) hivikihiyo original yupo wapi?
 
Kwakweli Nchimbi amekuwa akiongoza sio vikao tu hata jumuiya yenyewe kibabe mno.Hii inathibitishwa na urefu wa vikao vya baraza hilo,kwani hua vifupi mno ka vile wanatumika kupitisha mabo yaliyokwishaamuliwa tayari.
Inaaminika hapa ndio chanzo cha mvutano kati yake na kina Frank then na sasa Nape ambao wanataka mijadala iwe hot kwenye baraza kuu maana ndipo wanapotengeneza viongozi wa CCm yao hapo.N akinachogomba pia ni elimu,wakati kina Nape wanataka wasomi,Nchimbi na watu wake wanataka vilaza kama yeye.Na kuna habari tayari ameshapanga orodha ya wa kuchaguliwa kwenye baraza kuu lijalo,naahidi nitawapa orodha tuijadili hapa,
 
Ndani ya CCM kweli kuna mambo .Nchimbi is saidi to make himself a King maker .Anautaka Urais miaka kadhaa mbele na anataka maslahi yake kulindwa .Es nakubaliana nawe juu ya hili maana Nchimbi si msemaji this time kulikoni kaanza kutoa statements na siasa za vitisho ?
 
1. Nadhani kuna haja kuwa na sheria ya kutathmini degree zote Tanzania kuangalia kama ni feki na kuchukuliwa hatua za kisheria! Uganda nao wamegundua kuwa over 30% ya wafanyakazi wa NSSF ya huko wana veti feki vya Makerere!

2. Serikali itoa tamko rasmi over hili..nafikiri haya ndo mambo JK ayaongelee na hata kama kuna jamaa zake waka degree/veti feki basi wasionewe huruma!
 
Huyu kijana Nape Nnauye anakula shule hapa India.Pamoja na kuwa anakula shahada ya kwanza lakini ukiangalia uwezo wake wa kujenga hoja ni kwamba ametofautiana sana kwa mbali na Nchimbi mwenye degree nyingi ambazo zimeonekana kununuliwa dukani zaidi kuliko kutoka darsani
 
Dk. Nchimbi tulia, mwosha huoshwa

Irene Mark

ALHAMISI ya wiki hii, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Dk. Emmanuel Nchimbi, alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa tamko zito, tamko la kuonya, la kuwachukulia hatua viongozi wa chama na serikali wanaojaribu kuingiza mikono yao katika uchaguzi wa chama hicho.

Dk. Nchimbi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alielekeza kauli yake hiyo kwa viongozi wote wa juu ndani ya CCM na serikali walio nje ya umoja huo wenye nia ya kuvuruga demokrasia wakati wa uchaguzi wa umoja huo.

Katika kile kinachoonyesha kukerwa kwa kiongozi huyo na vitendo vya wenzake, serikali na ndani ya chama, alionya kuwa atawaaibisha wote watakaotia dosari kwa namna moja ama nyingine uchaguzi huo ulioanza juzi katika ngazi ya mashina nchini kote.

Dk. Nchimbi, Mwenyekiti anayemaliza muda wake mwezi Desemba mwaka huu, alisema kwa kujiamini, namnukuu: “Tunawapa tahadhari bila kujali ni viongozi wa serikali au wa chama, waache tabia ya kuingilia uchaguzi na wasithubutu kufanya hivyo. Huu ni ushauri wa hisani, wasije wakatembea macho chini kutokana na aibu watakayoipata.”

Hili ni onyo zuri kwa wenye nia hiyo hasa linapotolewa na kiongozi wa aina ya Dk. Nchimbi ambaye baadhi ya wachambuzi wa mambo walitafsiri kuwa ni sawa na Dk. Nchimbi kujinyooshea kidole mwenyewe; wengine wanasema ni kauli ya ‘mfa maji asiyeisha kutapatapa.’

Ninakubaliana na wachambuzi hawa. Kwanza, kwa sababu sitaki kuamini kuwa Dk. Nchimbi ni mwepesi wa kusahau kiasi hicho. Historia ya kisiasa ya Dk. Nchimbi inaonyesha kuwa katika kipindi chake miaka kumi ya uongozi ndani ya umoja huo, Dk. Nchimbi amekuwa na makundi na ni muasisi wa makundi ndani ya umoja huo na katika CCM kwa ujumla.

Tafsiri ya haraka inayojitokeza kwa historia yake kisiasa na kauli yake hii ni kwamba aliokuwa akicheza nao ngoma moja sasa wamemgeuka, wamemzidi kete, wamemuacha akiwayawaya.

Tujikumbushe usemi huu: ‘Ukiua kwa upanga, utakufa kwa upanga.’ Hili linajidhihirisha kwa Nchimbi ambaye zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa siku chache kabla na baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Vijana (UVCCM), hayati Amina Chifupa, alituhumiwa kuwa chanzo cha kusambaratika kwa ndoa ya mbunge huyo kijana. Kisa siasa!

Zilikuwa tuhuma mbaya kwa Dk. Nchimbi lakini alikataa kuzijibu. Tuhuma zilionyesha kuwa aliiona dhamira ya Amina ya kuwania uongozi wa juu ndani ya UVCCM, hivyo aliamua kwa makusudi kumuundia zengwe litakalomwondoa kwenye ulingo wa siasa kijana mwenzake.

Tukiipitia historia isiyokuwa rasmi kuhusu matukio yaliyoambatana na kifo cha Amina, inaonyesha kuwa ni Dk. Nchimbi aliyeelezwa kumbeba Amina katika hatua zake za mwanzo kuingia katika siasa. Hili hajawahi kulikanusha.

Inaelezwa zaidi kwamba ni yeye Dk. Nchimbi aliyehakikisha Amina anasimikwa kuwa kamanda wa vijana kabla ya kumwingiza kwenye mchakato mgumu wa kuwania uwakilishi wa kundi hilo huku akimpigia kampeni za chini kwa chini akishirikiana na Kapteni mstaafu, John Komba.

Kwa waliowashuhudia wanasiasa hao vijana, siku za mwanzo baada ya kuapishwa Amina kuwa mbunge, walikuwa bega kwa bega katika kupiga hatua kadhaa za kisiasa.

Haikuwa siri, Dk. Nchimbi alijitolea kuwa ‘Godfather’ wa Amina huku wengi tukiamini kuwa, alifanya hivyo kwa nia njema kutokana na ukweli kwamba alikuwa kiongozi wake katika UVCCM.

Historia hiyo hiyo inaonyesha kuwa Dk. Nchimbi ni mmoja wa wanasiasa walioongoza mbinu za hila za kumwingiza Amina na kumfanya akubalike ndani ya UVCCM katika kipindi kifupi.

Katika hatua nyingine, inaonyesha kuwa kwa sababu anazozijua mwenyewe, Dk. Nchimbi aliamua kumpoteza Chifupa kutoka katika anga za siasa kwa kumtengenezea zengwe. Kweli, alifanikiwa.

Kilichomponza Amina ni nguvu alizopata katika medani za siasa, nguvu hizo zilimwogofya mwenyekiti wake, akaamua kumshughulikia. Hata hilo, mbali na kuandikwa kwa mapana na marefu, Dk. Nchimbi hakulikanusha, jambo lililothibitisha kuwa kweli alimshughulikia mwanafunzi wake huyo kisiasa.

Wakati haya yakiwa bado katika kumbukumbu za wengi, Dk. Nchimbi anaibuka akilalamika kuhusu kuwapo kwa mbinu chafu za kuwabeba wapendwa wa viongozi wa ndani na nje ya UVCCM, kwa lengo la kuwapa madaraka huku akisisitiza kuwa vijana hawapendi viongozi wa ‘kuchongwa’. Kilio cha ajabu!

Maneno mengine ya Dk. Nchimbi yanaduwaza. Kwamba upo uwezekano wa uchaguzi huo kugubikwa na vitendo vya rushwa, kupakana matope na kuingilia uchaguzi kwa masilahi binafsi. Ni maneno yanayoacha maswali mengi kuliko majibu.

Kimsingi, Dk. Nchimbi ameanza kushughulikiwa na wanamtandao wenzake wanaoendekeza siasa za makundi na kuua demokrasia ya kweli ndani ya CCM na taifa zima.

Kwa wafuatiliaji wa siasa za hapa nyumbani, watakubaliana na mimi kuwa CCM ni kinara wa propaganda, kashfa, siasa za mizengwe na kupakana matope, hasa katika vipindi vya chaguzi mbalimbali.

Dk. Nchimbi ni mmoja wa wanamtandao, kundi linaloaminika kuwa kinara wa siasa za kuchafuana na kupakana matope, hivyo si rahisi kuamini kwamba hivi sasa anachukizwa na siasa hizo. Kinachoingia akilini ni kwamba amezidiwa nguvu na kundi jingine la wanasiasa linalompinga ndani ya chama chake.

Na kama anavyowalalamikia sasa wanasiasa na viongozi wenzake wanaotaka kuharibu uchaguzi wa UVCCM, ni hivyo hivyo alivyolalamikiwa yeye na wanachama wenzake ndani ya UVCCM hadi ikamlazimu Mwenyekiti wa zamani wa CCM, Benjamin Mkapa, kumtenganisha na wana UVCCM kwa kumpa wadhifa wa mkuu wa wilaya.

Aidha, dhambi anayoikemea sasa Dk. Nchimbi aliwahi kuhusishwa nayo wakati akitetea nafasi ya uenyekiti kwa awamu ya pili, baada ya kutuhumiwa mambo mazito hadharani na aliyekuwa mgombea mwenzake, Jane Mihanji.

Kwa kauli hii ya Dk. Nchimbi, mwanasiasa asiyependa kuzungumza na vyombo vya habari, ni wazi kwamba sasa anaelekea ukingoni, siku zake katika jukwaa la siasa zinahesabika baada ya kujijengea maadui wengi ndani na nje ya chama chake.

Dhambi aliyoshiriki kuifanya kwa muda mrefu sasa imemgeukia yeye, ameamua kukimbilia katika vyombo vya habari, ambako nafasi ya ukombozi ni finyu zaidi, kwa sababu iwapo mabingwa wenzake wa siasa za kupakana matope na kuchafuana wataamua kumshambulia kupitia vyombo vya habari, basi siku za uhai ndani ya siasa za kibabe na kuchafuana sitazidi kupungua.

Source: Tanzania Daima

Maswali ya kizushi: Hivi Mh. Nchimbi siku hizi yuko kundi gani? Maana Mtandao ndiyo huo umeishayoyoma, na kinachoandaliwa ndani ya UVCCM kwenye huu uchaguzi wa mwaka huu ni "Focus 2010" au "Focus 2015"! Kuna mtu yeyote ambaye ameishaonyesha nia ya kutaka kumrithi Nchimbi? Kuna kipindi ilisemekana kwamba alikuwa na mtu wake, ni yupi huyo aliyeandaliwa kumrithi?

Irene ana chuki zake mwenyewe kwa Nchimbi

Na Zephaniaanjela

Nimeisoma kwa makini makala ya Mwandishi Irene Mark ya kumtaka Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Dk. Emmanuel Nchimbi atulie kwa vile mwosha hatimaye naye huoshwa.

Katika makala hiyo iliyoanza kuchapishwa kwanza katika gazeti la Tanzania Daima Toleo la Jumapili Machi 9, 2008, Irene amejitahidi kwa kadri awezavyo "kumshambulia" Dk. Nchimbi kama mtu binafsi zaidi tofauti na chanzo kilichopelekea achukue hatua hiyo ambayo hakika inasikitisha!

Tatizo nililoliona katika makala yake hiyo ni kuingiza ushabiki na chuki binafsi, itikadi za kisiasa huku lengo lake hasa likiwa ni kutaka kumdhalilisha kwa maslahi anayoyajua mwenyewe.

Waliokuwepo katika mkutano wa Dk. Nchimbi na waandishi wa habari, Machi 5, 2008, wanajua kile alichozungumza na kujibu vizuri maswali yote aliyoulizwa na watu kama Muhibu Saidi wa gazeti la Mwananchi, hivyo kuja na madai nje ya kile alichosema katika kikao hicho ni sawa na kufanya ukuwadi wa kisiasa kwa niaba ya Chadema, na pia inawezekana amefanya hivyo kwa nia ya kutaka kumfurahisha mwajiri wake wa kweli, Freeman Mbowe.

Dk. Nchimbi anayehusishwa na historia ya kuunda na kusimamia makundi katika Umoja wa Vijana na CCM kama taasisi za kisiasa hata siku moja hajawahi kuhusika na hilo, badala yake waandishi wa habari wasiojua siasa kama Irene ndio wamekuwa wakihadithiwa uongo na wapinzani wa CCM na kuubeba kama ulivyo bila ya kutafiti.

Kwa mfano, ni ujinga mtupu kumhusisha Dk. Nchimbi kwa namna yoyote ile na suala la mgogoro na hatimaye kusambaratika kwa ndoa ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia UVCCM, hayati Amina Chifupa, mwaka jana.

Nimejaribu kuisoma makala yake hiyo kuanzia gazetini hadi katika mtandao, lakini sikuona popote alipothibitisha kwa namna moja ama nyingine kuhusu jambo hilo iwe kwa kuonyesha ushahidi wowote usio na mashaka, badala yake ametumia uvumi wa mitaani unaoweza kuzungumzwa na mtu yeyote wakiwemo makuwadi wa fitina kwa watu.

Uandishi wa kusukumwa na utashi wa kisiasa na kujifanya mpiganaji wa mstari wa mbele kuliko hata Mbowe, Dk. Slaa na viongozi wengine wa Chadema ni kushusha hadhi ya taaluma, hivyo Irene kama anataka kuingia katika siasa ni vuzuri akatangaza hadharani ili wanasiasa pia anaowatungia uzushi kama Dk. Nchimbi nao waweze kumjibu kwa haki majukwaani ama vinginevyo kuliko kubishana kwa njia anazotaka wafanye akidhani ni watoto kama yeye.

Ni makosa makubwa kushabikia kile anachoita "kumbukumbu" ama rekodi huku akijua kwa uhakika kabisa kuwa hazipo na kumhusisha mtu na jambo kubwa kama kusambaratisha ndoa ya mume na mke, tena kwa sababu za kisiasa, suala ambalo haliingia kichwani ila labda kwa mtu asiyekuwa na akili timamu!

Kwa mfano, hivi Irene akiulizwa kuwa ndoa ya Amina Chifupa na Mohammed Mpakanjia ilikuwa na uhusiano gani na ubunge, Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM ama Unaibu Waziri wa Dk. Nchimbi atatoa ushahidi gani?

Atajitetea kwamba watu walikuwa wakizungumza na yeye akasikia ama atatoa ushahidi wa maandishi alioupata kutoka kwa Mpakanjia?

Au, kama ni kweli kuwa Dk. Nchimbi alifanya hila kuisambaratisha ndoa ya Amina ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa, Irene anataka watu waamini kuwa Mpakanjia ana akili finyu kiasi cha kufikia hatua ya kumtaliki mkewe aliyezaa naye mtoto kwa kuamini uvumi wa barabarani?

Ni ujinga mwingine mkubwa kutaka kumlazimisha Dk. Nchimbi awe anajibu kila upumbavu na tuhuma za utumbo zinazotolewa na wapinzani wake kisiasa na kuacha shughuli zake za kuitumikia nchi yake kutokana na madaraka makubwa matatu ya kisiasa aliyonayo akiwa Mbunge wa Songea Mjini, Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Wakati Irene akisema mwishoni mwa makala yake kuwa Dk. Nchimbi ni mwanasiasa asiyependa kuzungumza na vyombo vya habari, mimi nasema kiongozi huyo hapendi kuzungumzia "umbea" na majungu, na pia hapendi kuongea na waandishi wa habari wanaoandika maoni yao zaidi katika habari zao badala ya kutoa taarifa sahihi walizoziona, kusikia au kuhadithiwa kwa kuambatana na ushahidi na vielelezo vya dhati pale inapobidi kufanya hivyo.

Mwandishi wa habari anayekusanya "umbea" na kudai ni kumbukumbu zilizosemwa zamani huku mtuhumiwa akiwa kimya na bila popote pale alipojaribu angalau kumtafuta iwe kwa simu ama ofisini kwake bila mafanikio

Waandishi waliosheheni "umbea" kama Irene ndio wanaweza kuja na uvumi kutoka uchochoroni kwamba Dk. Nchimbi alimpoteza Amina kutoka kwenye anga za siasa kwa kumtengenezea zengwe kutokana na sababu anazozijua mwenyewe.

Kila ninapotaka kumshangaa mtoto huyo wa kike anayekuzwa na kulelewa Bilcanas Club ninashindwa.

Hivi Amina alikuwa na kitu gani kinachoweza kusababisha Dk. Nchimbi apoteze ubunge wake, apoteze Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM au Unaibu Waziri alionao kama siyo uongo na upeo mfupi wa kuchambua mambo?

Iko wapi nguvu anayodaiwa kuwa nayo Amina katika ulingo wa kisiasa iwe katika UVCCM, CCM na kadhalika? Angewezaje kuwa na nguvu na kufikia hadi kumtisha Dk. Nchimbi wakati alikuwa chini kabisa katika matawi akiendesha kampeni za kusaka ukamanda wa Vijana ili angalau apate jukwaa la kusemea?

Nani asiyejua kuwa Amina alikuwa akifanya hadi utapeli kwa kuahidi kutoa misaada ya kifedha kwa UVCCM kama alivyofanya katika mkoa wa Dar es Salaam, lakini "akaingia mitini" na kuwaacha solemba chipukizi aliodai kuwa angewapeleka mkutanoni Dodoma?

Kama Irene haamini haya aende kwa Katibu wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sixtus Mapunda katika jengo ilipo Studio ya Redio Uhuru, jirani na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM akaambiwe ukweli huo, tena kwa kuonyeshwa kumbukumbu za maandishi na siyo kwa hadithi za kuchonga kama anazokuja nazo yeye.

Akitoka huko aende pia awaulize Makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni ili katika sehemu hizo zote nako apewe uthibitisho na kisha atoe hukumu mwenyewe.

Katika hali hiyo hata bila kuzungumzia matatizo mengine makubwa aliyokuwa nayo Amina, hivi mwanasiasa kama huyo angewezaje kumtisha Dk. Nchimbi na katika jambo lipi?

Tukiachana na Amina, Irene pia anaonyesha kuwa ni mbumbumbu mkubwa kabisa wa masuala ya kisiasa anapokuja na mfano mwingine dhidi ya Dk. Nchimbi kuhusu kile anachodai ni mgogoro uliokaribia kuzuka kati yake na aliyekuwa mpinzani wake katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM, Jane Claude Mihanji.

Pamoja na kuishia kusema tu kuwa Dk. Nchimbi alihusishwa hadharani na mambo mazito kwamba alijaribu kumfanyia Mihanji, hilo nalo haliwezi kukubalika hata kidogo na ndiyo maana hata Jeshi la Polisi liliona kuwa ni uongo uliotungwa kwa malengo "machafu".

Jane alidai aliitwa nyumbani kwa Dk. Nchimbi huko Tabata jijini Dar es Salaam, na kwamba wakati wakiwa pamoja sebuleni wakizungumza na kujadiliana mambo kadhaa ya kisiasa, ghafla alikuja mtu dirishani na kupuliziwa sumu asiyoyajua, tuhuma ambazo hata mjinga kabisa hawezi kuzikubali.

Namshauri Irene aulize watu wanaojua undani na ukweli kuhusu uongo huo ili wamwambie kwa ushahidi namna Jane alivyokuwa ameahidiwa ubunge wa kuteuliwa na hatimaye Unaibu Waziri wa Habari na mmoja kati ya "vigogo" waliokuwa na nia ya kugombea urais mwaka 2005 ili amtumie kukidhi matakwa yake ya kisiasa.

"Kigogo" huyo wa CCM hakutaka Dk. Nchimbi agombee Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM kwa sababu alijua kuwa angeibuka mshindi, hivyo ili kuzuia jambo hilo akapanga kumwibulia kashfa na kumtafuta Jane ambaye bila hiyana akaingizwa "mkenge" na kujifanya kapuliziwa madawa yenye sumu sebuleni ili apofuke macho au afe kabisa.

Hata madaktari kama Maua Abeid Daftari walihoji kwenye kikao cha Kamati Kuu na "kigogo" aliyekuwa akimtumia binti huyo akashindwa kutetea uongo wake ni namna gani sumu hiyo ipulizwe sebuleni walipokuwa wawili, lakini imfuate Jane peke yake na kumuacha Dk. Nchimbi utadhani ina akili na macho.

Mkakati huo ulikuwa ni jaribio la pili la kutaka kumwengua Dk. Nchimbi baada ya awali kuletwa hoja ya umri kuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM aliyevuka miaka 30 hata kama hajafikisha 35 asigombee Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM, lakini likagonga mwamba na kusambaratishwa.

Kilichoulizwa na watu wenye busara katika Kamati Kuu ya CCM ni jinsi gani sharti hilo liwepo katika ngazi ya taifa peke yake huku kwenye matawi, kata hadi wilayani wanachama wa Umoja wa Vijana wenye umri wa zaidi hadi miaka 34 wakiwa wamegombea uenyekiti na nafasi nyingine za kuchaguliwa katika ngazi hizo na kushinda.

Wakashindwa kujibu swali la kama uchaguzi huo katika ngazi hizo zote nchini kote ufutwe na kuanza upya au kama sharti hilo la dharura lilikuwa ni maalum kwa ajili ya mtu mmoja, hivyo ikaamuliwa kuwa kanuni hiyo ya uchaguzi ianzie uchaguzi mkuu wa UVCCM unaofanyika mwaka huu kwa sababu ilichelewa kuletwa.

Hata hivyo, wale waliokuja nayo mwaka 2003 wakiwa na umri wa miaka 26 hivi leo wanasaga meno kwa vile tayari wana umri wa miaka 31, ule ambao kama walivyotaka iwe mwaka huo hivi sasa hawana sifa ya kuwania uongozi wowote katika UVCCM.

Hata madai kuwa Dk. Nchimbi ni mmoja katika kile kinachoitwa ni kundi la wanamtandao linaloaminika kuwa kinara wa siasa za kuchafuana na kupakana matope nao pia ni uongo mwingine.

Wanasiasa dhaifu ndani na nje ya CCM ndio wanaeneza uvumi huo, lakini hawataki kabisa kuzungumzia ukweli kuwa kinachowakera wengi akiwemo Irene na wale wanaomtuma kuonyesha ujinga wake ni ubora wa mikakati ya wana CCM waliokuwa wakimuunga mkono aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete katika harakati zake za kuwania uteuzi wa kugombea urais mwaka 2005.

Katika mbio hizo, jumla ya wana CCM 11 walichukua fomu za kuwania nafasi hiyo. Mbali na Kikwete, wengine waliojaribu bahati zao ni Mzee John Malecela, Frederick Sumaye, Salim Ahmed Salim, William Shija, Idd Simba, John Shibuda, Ali Abeid Karume, Abdallah Kigoda, Mark Mwandosya na Patrick Chokala.

Hivyo, idadi hiyo ilisababisha kuwe mitandao 11 ya kusaka wadhifa huo, lakini unaong'ang'aniwa na waandishi wenye chuki zao wenyewe ni mtandao wa Kikwete utadhani Mwandosya, Malecela, Sumaye, Kigoda au Salim Ahmed Salim hawakuwa na ya kwao.

Inaeleweka kuwa Mei 3, 2005, mitandao yote hiyo iliishia hapo baada ya Kikwete kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini wajinga wa kufikiri na wale wenye chuki zao bado wanaeneza majungu dhidi ya viongozi kama Dk. Nchimbi waliokuwa katika kundi hilo lililoshinda kwa ubora wa mikakati.

Kina Irene hawasemi hata kidogo kama Mbowe naye alikuwa na mtandao wake alipokuwa akichuana na kina Anna Maulida Komu, Hebron Mwakagenda na wengineo katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kutoka Chadema.

Hawasemi kabisa kuwa mitandao yote ya harakati hizo huishia pale mshindi anapopatikana na kubakia mmoja tu unaowaunganisha wanachama katika ujumla wao, hivyo wanachofanya wale wanaong'anga'ania kuwepo "mtandao" wa Kikwete hadi leo katika CCM na kuwahusisha wanasiasa mahiri kama Dk. Emmanuel Nchimbi wana chuki zao wenyewe!
 
Heshima Mbele,
Wakti mwingine huwa najiuliza UVCCM imejaa watu wa ovyo sana.ukianzia wakina benno Malisa na hata Jerrry,sio watu amkini.Jerry alikuala sana pesa ya DARUSO wakti akiwa Waziri wa mambo ya Michezo na Burudani.kuan haja ya kuchukua watu makini katika cham,ila kwa tabia hii ya CCM maslahi tutegemee hawa majamaa kurudi tena.

Mie kuna wakti nilisikia kada mmoja wa CCM ambaye alishwahi kuchukua fomu ya kugomebea u-spika mwaka 2005,kama sikosei anaitwa mnyeti naye laikuwa anjipanga kugombea nafasi itakayoachwa na nchimbi.

1;VAILET MZINDAKAYA--simafahamu vyema huyu binti ila anaonekana anakubalika.
2;BENO MALISA---huyu ni mfano wa mtu aina ya lowassa,hana historuia na chama ila anataka kmtumia Riz ili aaminike.hii ni mbaya sana!!
3;HUSEN MOHAMED---simfahamu
4;JERRY SLAA----hafai..abaki kwanza katika udiwani na atatue matatzio ya watu wa ukonga huko..
5;NAPE MNauye-- arite candidate
6;ZAINAB KAWAWA---mambo ya kurecicle hatutaki,,

kuna jambo ambalo nimegudua watoto wengiu wa wakubwa kukata ishu kwao ni tatizo kubwa ndio maana wanaimbilia short cut ..siasa,waje katika masiha ya proffessionalism kama wataweza.

mtu kama beno kasoma Sheria,ila sidhani kaam aanaweza kupractise Law.ni sawasawa na mtu aliyesomea Uchumi ila anashindwa kujua kwanini watu wake ni masikini.

naona watu wamenunuliwa hapa,
karibu zephania..ila vita ni kubwa..Nchimbi asafishiki
 
Back
Top Bottom