Kama mna uhakika wamefoji vyeti basi nendeni Mahakamani...JF si mahakama. Mtikila kwa muda amekuwa anasimama Mahakamani kupinga mambo mengi tu...mengine ameshinda na mengine kushindwa. Kama mmeshindwa basi Basi tumuombe Mtikila asimamie hilo!!! kinyume chake itakuwa kuwalaumu watu pasi na Hoja nzito.
Bado zipo Online degree nyingi tu na wengi wamekuwa wanafanikiwa. Leo TZ kipo Open University sijui wao graduate wao wanafanyaje. Nakumbuka Mzee Malecela nae alipewa Dr. wa Heshima na Open University hapa DSM..(kama nimekosea naomba mniweke sawa)
You missed even the glimpse of the Train.
We are not talking about Online universities, we are talking about fake Universities.
Ziko nyingi sana hizo, na mazuzu kama Nagu Nchimbi nk wanaona ni kivuno.
Check and differenciate between the two.
PhD za heshima anaweza pewa mtu ambaye hata kusoma hajui, sifa za kupewa PhD za heshima zipo na kila chuo kinautaratibu wake.
Pia wakati inatolewa Dunia nzima huambiwa ni PhD ya heshima.
PhD yeyoteile Duniani hutolewa kwa kupiga shule isiyo pungua 3 years kama wewe ni kipanga. Wapo wazee kibao hapo Tanzania wamepiga PhD zao miaka 7 mfululizo kwa sababu pengine Presentation zao zilikuwa hazikukubaliki au ugumu wa kuweka Thesis zao katika vitendo.
Hata mimi ningependa kupata PhD.
Hiyo Masters tu inanitoa kamasi kama mtoto wa tumbiri alo lowa maji ya mvua za masika kule Morogoro. PhD Je?
PHD Fake ni dalili moja kubwa ya kukosa uaminifu katika mambo yote unayo yafanya.
Watu hawa wanao foji PhD ukiwachunguza utagunduwa kwamba hata walipokuwa mashuleni walikuwa na vyeti Feki vya Ugonjwa ili shule
iwapikie Light Diet na
kusamehewa kufanya
kazi za mikono.
MH mmoja tulikuwa naye shule kule Mazengo Dodoma, alikuwa na cheti cha daktari kwamba anaumwa Vidonda vya tumbo na Uti wa mgongo.
Sasa Kituko.
Nikiwa muajiriwa pale Dar siku moja tuligongana Joyce kwa Joyce(ana kwa ana) wote tukila Chipsi Dume zenye Pili Pili na chachandu la nguvu kwa mzee wa kuchoma mihogo pale karibu na Azania Sec School.
Jicho alilo nikata lilitosha kabisa kufunga nusu ya mdomo wangu.
Hata hivyo niliweza kumwuliza. " Vipi tatizo la tumbo liliisha?"
akanijibu yale yalikuwa mambo ya shule siku hizi kila kitu kinapita, siunajua mwenyewe dar hii na usawa ndo huu?
Nikamwuliza kazi anafanya wapi akaniambia Quality Garage kama Body Builder. Sikuwa na haja tena ya kumwuliza vipi tatizo la mgongo kwani jibu nilikuwa nalo tayari.
Ugonjwa na Vyeti vyote vilikuwa Fake
Wana JF na watanzania wote walio soma na kuelimika, jitokezeni mgombee Ubunge ifikapo 2010 ili Bunge letu tukufu liwe na Wabunge walio na elimu isiyo na maswali wala dalili za ubabaishaji.
Kusitasita kwenu ndiyo kunawafanya hawa wagonjwa hawa wenye uzoefu wa kufoji tangu secondary kutuongoza kama mikondoo mijinga wakati sisi ni watu na akili zetu.
Nchimbi subiri zamu yako ya kunawishwa.