...Lawama zinakwenda pande mbili, kwa serikali kufumbia macho raia wakiendelea kujenga karibia na kambi za jeshi, na Raia wenyewe.
Haya madhara hayataishia kwa waliojenga karibu na maghala haya ya silaha, ....hata waliojenga bonde la Jangwani, ipo siku 'El Nino' au 'tsunami' litawachukua waliokuwamo na wasiokuwamo. Tuangalie mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoathiri dunia, hususan yaliyotokea Australia.
Ujenzi karibia na kambi ya jeshi Lugalo, kambi ya jeshi Monduli, na hata ujenzi wa maghorofa marefu karibia kabisa na Makao makuu ya jeshi Upanga ni hatari kwa raia na jeshi pia.