Dini zinasema nini kuhusu wanawake?

Dini zinasema nini kuhusu wanawake?

Mtoa mada kasema wanawake hawatakuwa na Chao mbinguni Kwa maana watatumika Tu,,,,hii kauli sio sahihi hata kidogo,,,,tofauti na Imani ya kikristo kwamba huko peponi watu watakuwa kama Malaika, katika Uislamu ni hivi wale waliofanya mema duniani watalipwa Kwa Yale waliyoyatenda na kuishi Raha mstarehe,huko nako ndoa zitakuwepo kama ilivyokuwepo kabla Kwa Adamu na mkewe kabla hawajafukuzwa huko Eden/ peponi. Kwahiyo watu wataishi na wake zao waliotakaswa na machafu yote.

Lakini jinsi mtoa mada alivyoeleza kana kwamba mwanamke yeye kazi yake ni kama chombo cha starehe Tu, kitu ambacho si sahihi.

"Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyo fanana; na humo watakuwa na wake walio takasika; na wao humo watadumu."
2 : 25

Na yaliyo elezwa humo ni Sawa na 4 : 57 kwahiyo haina haja ya kurudia tena

Naomba mtulie kama mnanyolewa mpaka nitakapo maliza ndio mlete maswali,,,,vinginevyo sitajibu chochote mpaka nimalize hoja zangu
 
Tuje kwenye hoja ya pili kuwa wanawake Wana thamani ndogo Sana mbele ya Allah....

Mtoa mada vile vile ameonyesha udhaifu mkubwa juu ya ufahamu wa lile aliloliongea, Aya 2:282 inazungumzia kuhusiana na kukopeshana, Allah anatoa elimu au muongozo kuwa pale watu wanapokopeshana basi waliandike Hilo deni kwani Hilo ndio Jambo Bora zaidi Kwa ushahidi,,,,na vile vile kuwepo na mashahidi wawili pale mnapoandikiashana, na ikasemwa mashahidi wawe wanaume wawili miongoni mwenu,,,,Ila kama wakikosekana wanaume wawili basi,awepo mwanaume mmoja na wanawake wawili,Kwa maana ili mwanamke mmoja akisahau basi mwanamke mwenzake amkumbushe, Mwenyezi Mungu ndio anajua hawa viumbe wake madhaifu Yao.

Hiyo maana halisi ya kuwepo wanawake wawili sehemu ya mwanaume mmoja,lkn sio kwamba wanawake hawana thamani mbele ya Allah...

"Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hilo hakika ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu"

2:282
 
"Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu."

4:34

Nimetanguliza hiyo Aya hapo juu,,,,mtoa mada amesema kuwa wanawake wakikataa kutoa penzi basi wapigeni,,,,upuuzi mkubwa alionyesha mtoa mada,,,,,Aya inazungumza Kuwa wanaume ni wasimamizi wa wanawake ndio kichwa cha familia,hivyo wanawake wasipo tii basi Kwanza waonywe,pili wahamwe katika malazi...ina maana katika Uislamu kama njia ya kumwadhibu mwanamke unaweza kumhama chumba usilale au usisex nae Kwa Mda usio zidi miezi minne,hiyo sehemu ya adhabu au ya tatu basi ni kuwapiga ili wakae katika mstari.

Naomba usiku huu niishie hapa.....mnaweza kuchangia mpaka hapa nilipo ishia,,,,panapo majaliwa insha'Allah nitaendelea kesho
 
Ukiangalia mtazamo wa watu kwenye vitu vingi umechangiwa na vitu vikubwa viwili, tamaduni na dini.

Leo nataka tutazame dini maarufu hizi mbili, Uislamu na ukristo zinazungumza nini kuhusu wanawake na mchango wao katika malezi na mtazamo wa waumini wao kwa wanawake.

Tuanze na uislamu.
1. Usilamu unasema wanawake ni viumbe ambao wako tayari kule mbinguni wakiwasubiri watu watakaoingia mbinguni. Soma Quran 2:25 na 4:57. Inasema kila atakaeingia mbinguni atapewa wanawake waliotakaswa vyema. Kwa maana kwamba wanawake hawana chao mbinguni, wao ni kutumika tu mwanzo mwisho.

2. Mwanamke ni nusu ya thamani ya mwanaume, kwa maana kwamba wanawake wawili ndio wenye thamani sawa na mwanaume mmoja. Soma sura 2:282, 14:176 na kadhalika. Hii inatoa picha kwamba wanawake wana thamani ndogo ama wao ni viumbe wa thamani ndogo mbee ya Allah.

3. Mwanamke akikataa kutoa penzi, unaruhusiwa kumpiga ama kumtandika hadi akubali. Mwanamke haruhusiwi kumkatalia mume wake anapohitaji penzi. Soma Quran 4:34.

5. Usijaribu kutaka kumtendea wema mwanamke, ni jambo gumu na lisilowezekana. Quran 4:129, Quran 23:6 inasema kua na huruma ama kua mwema kwa mke wako.

6. Mwanao wa kiume akiachana na mke wake unaruhusiwa kumuoa mtalaka wa mtoto wako. Kwa maana kwamba baba na mtoto mnaruhusiwa kucheza uwanja mmoja. Quran 33:37.

7. Allah alimpa Mtume Mohamed ruhusa ya kuoa wanawake wengi atakavyo. Quran 53: 50-51.

8. Mbinguni kuna mabikra wa kutosha wakiwasubiri watakaoingia mbinguni. Quran 38:52.

9. Unaweza kumpa mkeo talaka hata kama hajabalehe. Quran 65:4.
Tuishie hapo kwa uchache

B. Twende kwenye ukristo.
Wanawake hawana chao mbinguni mbona ni uwongo wakati peponi kila mtu atapewa mpaka ataridhika na starehe za kila aina ambazo jicho hakijawahi kuona ,sikio hakijawahi kusikia wala mtu kudhania Ktk fikra zake
483-quran-english-tawbah-9-72(1).png

IMG_1278.jpg
 
mtoa mada uisoma Qurani tukufu kama vile unasoma kitabu cha sadiki na chitemo ..mkuu ertu bey ameshamaliza kila kitu maswali yako yote amekujibu
 
Mtoa mada amesema katika 4:129 kuwa usijaribu kumtendea mwanamke wema kwasababu ni Jambo lisilo wezekana....

Kama kawaida mtoa mada kaingia chaka tena,,,,,Aya imezungumzia mambo ya mitala hapo au uke wenza,kwamba Kwa maumbile ya mwanadamu mwanaume mwenye wake wawili hawezi kuwapenda wote kisawasawa hata kama akijitahhidi,Hilo swala ni gumu Ila wameaswa waume hapa kwamba basi ndio wasije kujisahau kumpenda mke mmoja zaidi mpaka mwengine kujiona sasa kama ametengwa au ametundikwa sehemu.

Na inasemwa kuwa Kwa Yule mwanaume ambaye atafanya upendeleo WA wazi Kwa mke moja zidi ya mwingine basi siku ya kiama atafufuliwa bega moja limeinama Kwa upendeleo alioufanya hapo awali.

Kikubwa mwanaume jitahidi kufanya uadilifu kadri utakavyo jaaliwa,sio huku anakula nyama kila siku halafu mwengine matembele kila siku hapo unafeli.
 
Mtoa mada Yani nimekupenda bure Kwa uzushi wako,,,,,33:37 inazungumzia kuhusu mtoto wa kupanga,je mtoto wa kupanga ni yupi? Ni mtoto ambaye huna nasabu naye kabisa ya kindugu au Kwa maana nyingine ni mtoto wa hiari ambaye umeamua Tu kumuita mwanao.

Sasa huko nyuma enzi za ujinga watoto wa kupanga walikuwa wanapewa haki zote na kuhesabika kama watoto halali wa mtu Fulani,,,ndio Mwenyezi Mungu akaja kuliweka Hilo Jambo Sawa,kwamba sio sahihi mtoto wa kupanga akahesabika kama mtoto wa damu.

Sasa unajua siku zote ili Jambo lieleweke vizur katika jamii basi halina budi kutolewa mfano,na Mwenyezi Mungu alitaka mfano huo utolewe na Mtume mwenyewe (rehma na Amani ziwe juu yake).

Na utaona katika Aya hapo Chini kuwa Mtume mwenyewe alitaka asilifanye hili Jambo Kwa kuhofia watu watamuonaje kwakuwa huyo Zaid alijulikana kama mwanae,,,,lakini Mwenyezi Mungu alimsema Kwa kumwambia unaacha'' kufanya Jambo Kwa sababu ya kuogopa watu badala ya kumuogopa Mwenyezi?

Kwahiyo baada ya Zaid kumwacha mkewe basi Mtume aliamrishwa amuoe ili avunje Ile desturi ilivyokuwepo awali na watu kubadilika na kuona tofauti ya mtoto wa nasabu ya damu na mtoto wa kupanga.

"Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliye mneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea. Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa."

33:37
 
Umetoa hoja kuwa mbinguni kuna mabikra WA kutosha wanasubir watu watakao ingia peponi,,,,Aya hiyo 38:52 haijazungumzia swala Hilo Bali imezungumzia kuwa watakuwa na wake zao ,yaani pamoja na starehe nyengine na mambo mazuri watakayopata basi watakuwa pamoja na wake zao.

"Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao."
38:52

Nitakuja kumalizia hoja kama mbili zilizo Baki insha'Allah
 
Ukiangalia mtazamo wa watu kwenye vitu vingi umechangiwa na vitu vikubwa viwili, tamaduni na dini.

Leo nataka tutazame dini maarufu hizi mbili, Uislamu na ukristo zinazungumza nini kuhusu wanawake na mchango wao katika malezi na mtazamo wa waumini wao kwa wanawake.

Tuanze na uislamu.
1. Usilamu unasema wanawake ni viumbe ambao wako tayari kule mbinguni wakiwasubiri watu watakaoingia mbinguni. Soma Quran 2:25 na 4:57. Inasema kila atakaeingia mbinguni atapewa wanawake waliotakaswa vyema. Kwa maana kwamba wanawake hawana chao mbinguni, wao ni kutumika tu mwanzo mwisho.

2. Mwanamke ni nusu ya thamani ya mwanaume, kwa maana kwamba wanawake wawili ndio wenye thamani sawa na mwanaume mmoja. Soma sura 2:282, 14:176 na kadhalika. Hii inatoa picha kwamba wanawake wana thamani ndogo ama wao ni viumbe wa thamani ndogo mbee ya Allah.

3. Mwanamke akikataa kutoa penzi, unaruhusiwa kumpiga ama kumtandika hadi akubali. Mwanamke haruhusiwi kumkatalia mume wake anapohitaji penzi. Soma Quran 4:34.

5. Usijaribu kutaka kumtendea wema mwanamke, ni jambo gumu na lisilowezekana. Quran 4:129, Quran 23:6 inasema kua na huruma ama kua mwema kwa mke wako.

6. Mwanao wa kiume akiachana na mke wake unaruhusiwa kumuoa mtalaka wa mtoto wako. Kwa maana kwamba baba na mtoto mnaruhusiwa kucheza uwanja mmoja. Quran 33:37.

7. Allah alimpa Mtume Mohamed ruhusa ya kuoa wanawake wengi atakavyo. Quran 53: 50-51.

8. Mbinguni kuna mabikra wa kutosha wakiwasubiri watakaoingia mbinguni. Quran 38:52.

9. Unaweza kumpa mkeo talaka hata kama hajabalehe. Quran 65:4.
Tuishie hapo kwa uchache

B. Twende kwenye ukristo.
We kma mkristo nakuomba uachane na mambo ya uislam ujui kitu!!

Na kma muilsam unaitaji kusaidiwa kabsa uniongea vitu sivyo kabsaaa
 
Ukristo+ushoga ndo maana mapadri hawaowi
 
Mtoa mada amesema katika 4:129 kuwa usijaribu kumtendea mwanamke wema kwasababu ni Jambo lisilo wezekana....

Kama kawaida mtoa mada kaingia chaka tena,,,,,Aya imezungumzia mambo ya mitala hapo au uke wenza,kwamba Kwa maumbile ya mwanadamu mwanaume mwenye wake wawili hawezi kuwapenda wote kisawasawa hata kama akijitahhidi,Hilo swala ni gumu Ila wameaswa waume hapa kwamba basi ndio wasije kujisahau kumpenda mke mmoja zaidi mpaka mwengine kujiona sasa kama amtengwa au ametundikwa sehemu.

Na inasemwa kuwa Kwa Yule mwanaume ambaye atafanya upendeleo WA wazi Kwa mke moja zidi ya mwingine basi siku ya kiama atafufuliwa bega moja limeinama Kwa upendeleo alioufanya hapo awali.

Kikubwa mwanaume jitahidi kufanya uadilifu kadri utakavyo jaaliwa,sio huku anakula nyama kila siku halafu mwengine matembele kila siku hapo unafeli.
Legasi za bega moja kuninama dah...
 
Tuje kwenye hoja ya pili kuwa wanawake Wana thamani ndogo Sana mbele ya Allah....

Mtoa mada vile vile ameonyesha udhaifu mkubwa juu ya ufahamu wa lile aliloliongea, Aya 2:282 inazungumzia kuhusiana na kukopeshana, Allah anatoa elimu au muongozo kuwa pale watu wanapokopeshana basi waliandike Hilo deni kwani Hilo ndio Jambo Bora zaidi Kwa ushahidi,,,,na vile vile kuwepo na mashahidi wawili pale mnapoandikiashana, na ikasemwa mashahidi wawe wanaume wawili miongoni mwenu,,,,Ila kama wakikosekana wanaume wawili basi,awepo mwanaume mmoja na wanawake wawili,Kwa maana ili mwanamke mmoja akisahau basi mwanamke mwenzake amkumbushe, Mwenyezi Mungu ndio anajua hawa viumbe wake madhaifu Yao.

Hiyo maana halisi ya kuwepo wanawake wawili sehemu ya mwanaume mmoja,lkn sio kwamba wanawake hawana thamani mbele ya Allah...

"Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hilo hakika ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu"

2:282
Nakunukuu "awepo mwanaume mmoja na wanawake wawili,endapo mmoja akisahau mwenzake amkumbushe"
Huyu mwanaume mmoja akisahau inakuwaje Sasa?
 
Imesemwa hoja kuwa mwanamke aweza pewa talaka ambaye haja baleghe 65:4,,,,, kiuhalisia Aya hii inazungumzia juu ya kipindi gani a wakati gani mwanamke anapaswa kukaa eda!

Kwanza eda ni nini? Ni wakati ambao mwanamke anakaa Bila kuolewa mara baada ya kuachwa na mumewe,na makusudio makubwa ni kujua je mwanamke aliyeachwa ana mimba au laa? Hii yote ni hekima kumuepusha mume mpya kuoa mwanamke ambaye ana mimba tayar ya mumewe wa awali .

Aya inafafanua kuwa mwanamke ambaye hedhi yake imekoma basi eda yake atakaa miezi mitatu (3),,,,na mwanamke ambaye hapati hedhi muda wake pia ni miezi mitatu,,,na mwanamke ambaye ameachwa akiwa na mimba basi eda yake ni mpaka pale atapojifungua.

Hayo ndio mafunzo ya hiyo Aya na si vinginevyo:

"Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi."

65:4

Tuje kwenye hoja kwamba Mtume ameruhusiwa kuoa wake wengi kadri apendavyo,,,,,,Kwanza sio kweli na pia Aya uliyotaja sio sahihi vile vile nimeona uvivu hata kuandika kwasababu inazungumzia watu WA thamudi na ukaidi wao mbele ya Mwenyezi Mungu.

Sasa tuje kwenye hoja sasa,,,,Kwanza ieleweke wazi Mtume hakuoa ovyo ovyo Kwa tamaa ya kimwili, Bali alioa wake wengi kutokana na sababu maalumu au mazingira maalumu katika kufanikisha kazi yake ya Utume!

Hakuoa Kwa tamaa Kwasababu ndoa yake ya Kwanza alidumu nayo Kwa miaka 23 mpaka pale mkewe alipopatwa na umauti,,,,na alimuoa bi khadija ambaye tayar alikuwa ameshawahi olewa mara mbili na mwanamke huyo vile vile alikuwa mkubwa kiumri Kwa Mtume Kwa miaka 15,je kama Mtume anapenda dogo dogo bilashaka asingekubali kumuoa mwanamke kama huyu,,,,na hata baada ya mke huyo kufariki,Mtume alikaa Bila kuoa tena Kwa Mda wa miaka minne au mitano,Kwa maana wakati mkewe anafariki yeye alikuwa na Miaka 48 na akaja kuoa akiwa na Miaka 53 au 55.

Wanawake wengi alio waoa ilikuwa ni katika kuunganisha koo mbali mbali ili imuwezeshe kutangaza Dini ya Mwenyezi Mungu na kuondoa uhasama,kama unavyojua ukishaoa basi koo hii na hii zinaungana na kuwa kitu kimoja,,,,lakini vile vile alioa ili kuzidisha mahusiano mazuri na mawaziri wake,mfano alipo muoa Aisha bint Abubakar, na Hafsa bint Umar.

Alioa vile vile wajane ambao walifiwa na waume zao na hivyo kuwastiri na kusaidia kulea watoto wao na kuwapa huduma Bora,,,,alioa vile vile katika kubadilisha desturi ambayo ilikuwepo awali ya kuwa mtoto wa kupanga ni kama mtoto wako wa kumzaa mwenyewe,na hapa alimuoa Zaiynab bint jarsh baada ya kutalikiwa na Zaiyd bin Haritha,,,, kifupi ni kwamba alioa wake wengi Kwa sababu na mazingira maalumu.

Alioa wanawake Tisa (9) na wakati huo Sheria ya kuoa wake wa nne ilikuwa bado haijaletwa na baada ya kuletwa hata yeye hakutakiwa kuongeza wake wengine baada ya wale ambao alishakuwa nao tayar. Na Kikubwa zaidi Mtume aliwapatia wake zake hao makazi,chakula na mavazi Kwa uadilifu mkubwa Sana.

Kwa uwezo wa Allah,,,,nimejibu hoja zote zilizo letwa mezani na mtoa mada,pamoja na kwamba lengo lake lilikuwa ni kupotosha ukweli,,,lkn siku zote penye Ukweli basi Uongo hujitenga.

Namkaribisha siku nyingine tena na nipo palee kumsikiliza na kujibu hoja zake!

Ni hayo Tu!
 
Back
Top Bottom