Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania;
Dini ya Uislam iliwezaje kuenea kwa wingi "Sub Saharan Africa" ilhali waarabu hawakuwa na makoloni huku? Ni kupitia biashara pekee ama kuna njia nyingine za ziada zilitumika?
Orodha ifuatayo ni baadhi tu ya nchi zilizopo katika eneo hilo la "Sub-Saharan Africa";
Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Central African Republic, Chad, Congo, Cote d'Ivoire, Eritrea, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Somalia, South Africa pamoja na Tanzania.
Ninaomba kuanza kwa kusema kwamba, kwa msio nifahamu mimi Infantry Soldier ni mkristo mkatoliki ila ninafahamu fika ya kuwa dini ya uislamu ni dini safi sana tena ya watu waungwana kweli inayohubiri amani na upendo kama ilivyo dini ya kikristo. I love and respect all my muslim brothers and sisters out there.
KWA UFUPI KUHUSU UKOLONI NA KUENEA KWA UKRISTO BARANI AFRIKA
=====
Ushahidi wa kihistoria unaonyesha ya kuwa Waafrika walikuwa na mila nyingi za kitamaduni na kidini ambazo zilichangia pakubwa katika kuenea kwa haraka kwa dini ya Ukristo katika bara letu.
Wamishionari wa Magharibi waliamua kukataa au kuweka pembeni mila hizi, ambazo ilikuwa msingi wa imani zetu tangu zamani. Mifumo hii ya msingi ya mila na tamaduni ya Waafrika ilitoa msingi thabiti ambao Ukristo ulifikishwa (kwa kiingereza changu kibovu ninaweza kusema upon which Christianity was conceived), kueleweka na kupokelewa.
Hata hivyo, wamishionari wengine walijaribu kuaminisha watu kwamba hakuna mila na wala tamaduni za urithi kama huo wa kidini uliokuwepo kabla ya kuwasili kwao katika bara la Afrika miaka hiiiyoooo ya zamani.
Ukristo na ukoloni mara nyingi huhusishwa kwa karibu kwa sababu Uprotestanti (wasabato, anglikana, Lutheran) na Ukatoliki walishiriki kama dini za serikali/kidola za mamlaka ya kikoloni ya Ulaya na kwa njia nyingi zilitumika kama "matawi ya udini" ya tawala hizo za kikoloni.
Wakati Wazungu walipokuja kuitawala Afrika, hawakufanya hivyo tu kwa nguvu waliyoitumia dhidi ya Waafrika. Hapana. Ukoloni ulifanywa vema pia kwa matumizi ya dini, na haswa Ukristo na ndio maana mpaka sasa, Waafrika wengi hujitambulisha kama Wakristo.
Inaonekana dini imetumika zaidi kuathiri utambulisho wa mtu mweusi barani Afrika. Dini za jadi za Kiafrika zimetupiliwa mbali na zinaonekana kama za kipagani na za kishamba kwa asili.
Wakati kila mtu anastahili kuwa imani katika dini yake, ni dini hiyo hiyo ambayo imetumika kuvuruga historia ya Afrika haswa na ujio wa ubeberu na ukoloni ambao umejengwa juu yake.
Dini zilifanikisha jambo moja kubwa sana barani Afrika: kuwafundisha Waafrika weusi kuachana na mila zao zote na kuwezesha kuenea kwa tawala za kikoloni.
SWALI KUU: Dini ya Uislam iliwezaje kuenea kwa wingi "Sub Saharan Africa" ilhali waarabu hawakuwa na makoloni huko? Ni kupitia biashara pekee ama kuna njia nyingine ya ziada ilitumika?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.