KAMARA KUSUPA NA FALSAFA YA DINI Kuna maneno ukiyasoma sharti uingie hofu. Dini za Kigeni. Dini za Asili. Kutoka kwa Mchungaji. Uh

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
KAMARA KUSUPA NA DINI ZA KIGENI NA DINI ZA ASILI

Kuna maneno ukiyasoma sharti uingie hofu.

Dini za Kigeni.
Dini za Asili.

Kutoka kwa Mchungaji.
Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa chini ya msaada mkubwa wa Waislam.

Kitabu changu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (1998)...

Hapa piga mstari maneno haya: "Muslim Struggle Against British Colonialism."

Waafrika wa Tanganyika walikuwa hawana jumuiya yao kama Wazungu, Waasia na Waarabu.

Waafrika waliwakilishwa na Father Gibbons kutoka Misheni ya Pugu.

Kleist Sykes, Mzee bin, Ali Said Mpima kwa kuwataja wachache wakaunda African Association.

Kisha wazalendo hawa hawa waliounda African Association wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kuitia nguvu African Association.

Aliniuliza msomaji wa kitabu changu kuwa alisubiri aniulize kama kweli kulikuwa na "Muslim Struggle."

Jibu akalipata ndani ya kitabu kuwa hakika ni "Muslim Struggle."

Kiongozi wa harakati za kupigania uhuru Mwalimu Nyerere alikuwa Mkatoliki akiungwa mkono na kundi kubwa sana la Waislam.

Ushahidi upo mkubwa tu.
Leo Nyerere Day iwe ya Dini za Asili.

Wako wapi hao wefuasi wa Dini za Asili?

Hawakuwapo wakati wa kuunda African Association 1929 wala kuunda TANU 1954 watazuka leo 2023.

Serikali ipo na Kanisa lina nguvu kubwa katika mihimili yote ya dola.

Waislam wapo lakini hawana sauti kubwa ndani ya serikali kwa kushika madaraka na mengineyo lakini sijapata kusikia kuwa hawafurahishwi na Nyerere Day.

Zaidi utasikia wakisema Nyerere asienziwe peke yake kwani hakuwa peke yake alikuwa na wenzake wengi katika kupigania uhuru wa Tanganyika na wengi wao walikuwa Waislam.

Leo anatoka mtu anatamani ati ipachikwe Dini Asilia katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwa kufanya hivyo kutamuenzi vizuri Baba wa Taifa.

Nyerere alikuwa Mkristo Mkatoliki na kautumikia Ukristo kwa mapenzi makubwa.

Nyerere anasubiri kupewa utakatifu.
Ajabu hii leo historia hii ya uhuru inatakiwa ati inasibishwe na Dini ya Asilia.

Uislam na Ukristo unaonekana haustahili kwa kuwa ni Dini za Kigeni.
Maneno haya hayawezi hata siku kutoka katika kinywa cha Muislam.

Ukisikia pametajwa Upagani jua kwanza huo Upagani unaletwa kupambanishwa na Uislam.

Mtu huyu anaesema haya hataki kabisa kusikia kuwa ndani ya TANU kulikuwa na masheikh waliombeba Nyerere mgongoni na mabegani kwa mapenzi makubwa na wakiuza kadi za TANU ndani ya misikiti.

Kamara Kusupa anaona historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere inastahili kunasibishwa na kujumuishwa na historia ya waumini wa Dini Asilia.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere ina uhusiano wowote na wafuasi wa Dini Asilia?

Ukiwaleta hawa wafuasi wa Dini Asilia wasiokuwapo Waislam waliokuwapo unawaweka wapi?

Picha ya Kwanza: Kushoto nyuma wa kwanza ni Father Gibbons kutoka Pugu Mission aliyekuwa Mwakikishi wa Waafrika wa Tanganyika.

Sijaona picha ya Father Gibbons na Waafrika aliokuwa anawawakilisha katika serikali ya kikoloni.

1697395595412.jpeg

1697395642862.jpeg

1697395671073.jpeg

1697395697369.jpeg

1697395722089.jpeg
 
Waislam mlishiriki kupigania uhuru kwasababu Mkoloni alikuwa Kafiri ingelikuwa kinyume chake msingelishiriki hata kidogo badala yake mngelisimama nyuma Mkoloni.

Dpw imethibitisha ilo.
History inawahukumu.

Wakati wa Ottoman empire inajipanua Afrika na mtu mweusi kuupoke uislam kwa kasi akaitoa Ardhi yake kama Sadaka kwa Mwarabu na pindi dhuluma,ubaguzi etc toka kwa Mwarabu kulipomzidia ilimbidi aachie maeneo yake bila hiana na kukimbilia upande wa Kusini.

Waislam weusi hawakutaka kupigania Ardhi yao badala yake wakaitoa sadaka kwa Mwarabu.leo Misri,Moroco, Tunisi hakuna Mweusi wakati kulikuwa na full black people.
 
Upo sahihi kabisa walikuwa wanaongozwa na chuki kwakuwa muingereza alikuwa mkristo laiti angekuwa mwarabu wasingeyafanya hayo
 
Waislam mlishiriki kupigania uhuru kwasababu Mkoloni alikuwa Kafiri ingelikuwa kinyume chake msingelishiriki hata kidogo badala yake mngelisimama nyuma Mkoloni.

Dpw imethibitisha ilo.
History inawahukumu.

Wakati wa Ottoman empire inajipanua Afrika na mtu mweusi kuupoke uislam kwa kasi akaitoa Ardhi yake kama Sadaka kwa Mwarabu na pindi dhuluma,ubaguzi etc toka kwa Mwarabu kulipomzidia ilimbidi aachie maeneo yake bila hiana na kukimbilia upande wa Kusini.

Waislam weusi hawakutaka kupigania Ardhi yao badala yake wakaitoa sadaka kwa Mwarabu.leo Misri,Moroco, Tunisi hakuna Mweusi wakati kulikuwa na full black people.
I seee!;)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom