Dini ni Utamaduni wa watu fulani



Kwani huo utajiri wa waarabu si umekuja hii miaka ya 70s tu, baada ya kupanda bei ya mafuta ??

mbona uislamu upo miaka mingi kabla na hali zao zilikuwa ni za kimasikini ??

Na huko ulaya na Marekani utajiri umekuja karibuni tu, hapo kabla na wao walikuwa ni masikini ??
 
W Wayahudi hawajawahi kuwa wakristo bora ukristo ungeuita Roman culture,wayahudi wana wana dini yao ya Yuda yaan Judaism na siyo wakristo.
 
Narudia tena
Kama Adam,Eve, Ibrahim na Musa hawakuwa na dini yoyote basi hakuna dini iliyoshushwa na Mungu.
Na hata hizi zilizopo hakuna iliyo Bora au juu ya zile zilizokwepo kabla hazijaja hizi.
 
Waafrika wengi vichwa vyetu nikama ubao kila mwenye chaki anakuja na kuandika cha kwake na tunakipokea tunaona ni bora kuliko chetu
 
We ndo umeharibu kabisa sasa[emoji3][emoji3][emoji3]

Utamaduni sio sehemu ya dini, bali dini ndo sehem ya utamaduni. Rudi shule ukasome elements of culture mkuu[emoji3]
Thanks kwa kumjibu vizuri kabisa, dini ni sehemu ya utamaduni wa jamii husika na tafsiri ya culture ni total way of living of a given society (Walter Rodney) kama yalivyofafanuliwa vizuri kabisa na mleta mada. Yanajumuisha dini/Ibada, kula, kuvaa, kumkaribisha mtoto anayezaliwa, kumuaga anayekwenda kuanza maisha ya ndoa, kumuaga/kumpumzisha aliyefariki nk nk nk nk.
 

Nimenakili baadhi ya maneno yako hapo juu, ili kujenga hoja.
Wewe wasema HAYO YOTE SI MAAGIZO YA MUNGU.
Laini ulinimaliza Nguvu pale uliposema kuwa ''Tujadili kwa hoja. Huu ni mtazamo wangu tu, unaweza kuwaza tofauti''.
nikapwaya.
hata hivyo , ujuwe kuwa mawazo kila mtu anayo na ndio ubinadamu.
sasa nikuulize swali
Wewe unaamini uwepo wa Mungu MMOJA Muumba?

Je wewe Umeshawahi quisoma na kuifahamu Qur-an?
Je wewe umesha wahi kuisoma na kuifahamu Bibilia?
Umefahamu Azimio zima la Dini katika vitabu hivyo?
Tunajuwa wazi kuwa tamaduni za watu ziko tofauti ,Lakini Dini pia Inautamaduniwake Makhsusi, Je uliwahi kulijua hilo?
 
W
Wayahudi hawajawahi kuwa wakristo bora ukristo ungeuita Roman culture,wayahudi wana wana dini yao ya Yuda yaan Judaism na siyo wakristo.
Kuna wayahudi wakristo Israel, ingawa ni wachache.
Pia Judaism imejikita kwenye vitabu vitano vya Musa tunaita 'Pentateuch' au Hebrew Bible, au Torah au five books of Mosses.
~Genesis,
~Exodus,
~Numbers,
~Leviticus na
~Deuteronomy.
Hivyo vyote vipo kwenye Biblia wanayoitumia Wakristo kwenye Agano la kale.
 
Maswali ni mengi sijui nianze lipi, ila kiufupi bandiko langu linaashiria kabisa kuwa Nina imani ya uwepo wa Mungu Mmoja. Kama umesoma vizuri.

Pia suala la kuisoma Biblia na Qur'an, vyote nimevisoma ABC's zake nazijua ndizo zilizonifanya niweze kuandika Uzi huu. Yawezekana wewe umesoma zaidi Ilimu hiyo Kama profession yako, tuendelee na mjadala. Tupo hapa kujifunza.
 
Shs 500/=, yaani Jero??!!, halafu unatamba humu ndani ya ukumbi wa Jf kwamba eti nawe huwa unatoa pesa!!!??, kweli wewe ni Tajiri kichwa sio Tajiri pesa.

Kumbe umeelewa eeh ..kunywa maji mengi upunguze jaziba
 
Kumbe umeelewa eeh ..kunywa maji mengi upunguze jaziba



Umesema ukitoa mwisho ni mia 5, kwani hiyo ni shs ngapi?, sio shs 500/=, yaani Jero??!!.--- kama ni sawa basi wewe ndiye uliyelewa konyagi na kama sio sawa basi mimi ndiye niliyelewa. 🤓
 
Na umasikini hawauendekezi, Binadamu wa leo mfia dini akiona unamiliki vitu vya thaman kama magari wanaanza kuingiza kifo kwamba fanya ibada ayo magari tutayaacha,

ni Mungu yupi anapenda wanadamu wake waishi kwa dhiki. uku mtaani kwetu ukiwa tajiri basi wew sio mwamini mungu. tunakufa masikin kwa kukosa akili
 
Mfia dini , mbna unapenda mabishano yasiyo na hoja ndani yake ? Mtoa mada ameeleza kinaga ubaga kuwa sisi tumeiga / tohoa tamaduni za watu ambazo zimeenda sambamba na Dini zao .
Mkuu samahani sana kama nimekukwaza .

Binafsi hujanikwaza.

Ila nimeuliza bila matusi wala kejeli ila nimeweka alaza za kuuliza ambazo zinaashiria kuwa nauliza.

Sijajua kitu gani nimekosea,ila niseme tena samahani sana kama nimekukera mkuu naomba niendelee na mtoa mada..
 
Nimekusoma mkuu.

Ila naomba nijue kwa uwazi kuhusu swala langu..

Tumekubaliana kwamba Mungu anajidhihirisha kwetu kupitia dini mbali mbali kama ambavyo umetoa dini kadhaa.

Ila ninachouliza mimi ni kuwa..
wewe unatumia mizani ama kipimo gani kujua kuwa haya kweli yanatoka kwa Mungu na haya yanatoka kwa watu tu ?
 
Huo utamaduni ambao unadhani ni wetu mkuu ni ule wa miaka gani ?
 
Kabisa mkuu. Yani tumekubali kutenganishwa kwa mambo ya kijinga sana. Imagine mwafrika mwenzenu mnaishi nae mnasaidiana kwenye shida na raha ni mwenzenu pengine alikuwa na msaada mkubwa kwenu jamii yake anaoishi nao lakini eti anakufa mnamzika kama mbuzi au mbwa kisa hakuwa dini yenu. Au mnakataa kumzika. Utu uko wapi? Tumeletewa ubaguzi baina yetu. Inauma sana
 
tunakipokea tunaona ni bora kuliko chetu


Chenu kilichobora ni kipi wewe muafrika??-- hiyo simu au laptop unayoitumia kuandika malalamiko yako hapa ni muafrika gani katengeneza???, Uchawi na kulogana na kuuana ndicho pekee mnachojua na maneno tu.
 
Chenu kilichobora ni kipi wewe muafrika??-- hiyo simu au laptop unayoitumia kuandika malalamiko yako hapa ni muafrika gani katengeneza???, Uchawi na kulogana na kuuana ndicho pekee mnachojua na maneno tu.
Hatuja zungumzia technology tumezungumzia dini na tamaduni.
 
Mfano kabla ya ujio wa wageni tulikua tuna abudu nini hasa babu zetu na kufa kwao je watachakuliwaje? maana hakukua na ukristo Wala uislamu na pia kwanini dini hizi mbili zilichelewa kufika Afrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…