Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Tafsiri ya Aya inayosema sio mitume wote Mtukufu mtume (saw) kasimuliwa habari zao ni hii:-

"Na kwa yakini tuliwatuma mitume kabla yako, wengine tumekusimulia na wengine wao hatukukusimulia----"
(40:78) Qur'an.

Tafsiri ya Aya inayosema kwamba mitume walitumwa katika kila umma ni hii hapa:-

" Na bila shaka tulimuinua mtume katika kila umma ya kwamba mwabuduni Allah na muepukeni muovu-----" (16:36) Qur'an.

Aya zingine zinazoungana na hiyo aya ni hizi hapa; 10:47, 13:7, 35:24.

Halafu nikusikie tena ukishikilia imani yako potofu kwamba waafrika na watu wengine hawakufikiwa na mitume kama kwamba sisi katika zama hizo tulikuwa kama manyani tusiostahili kupata muongozo wa Mungu ili nasi tuipate pepo pindi tulipofariki (wazee wetu wa zamani).
Hiyo aya haisemi sehemu. Ila huyu mtafsiri akajiamulia tu kusema Kila uma. Wakati hicho kitabu hakijasema hivyo
 
Mkuu kuhusu lugha..
Embu tafakali mara paapuuu umetua thailand ukataka uende kuabudu kidogo unadhani kama hujui ki thai kweli inaweza kuenda nao sawa kwenye ibada maana utakuwa huelewi chochote kinacho endele.
Allah ni muweza wa yote ndio maana akatuambia kwenye sala zote tutumie kiarabu na kwenye dua basi tumia lugha yeyote ile basi yeye atakusia.
Yaani leo hii chukua waislamu toka mataifa yoyote unayo yajua wewe na tena wawe wanajua lugha zao tu,waambie wamuabudu Mungu wao basi wote watafanya kitu kilekile na tena kwakuelewana bila tatizo lolote na dua itasomwa ya pamoja na wote wataelewa.
Hii ndio hekima ya lugha moja wakati wa kuabudu.
Ila kwenye dua wewe piga hata kisukuma.
 
Naona unaruka ruka nimekuuliza swali dogo hujibu, unatoa maelezo mbali kabisa.

Unafikiri dini inaendeshwa kwa nadharia na mawazo ya mtu binafsi siyo ? Tunataka ushahidi wa hayo unayo yasema.

Ulichotakiwa wewe ni kukoma pale pale ilipo ishia aya ila kuleta ujuaji kama huu ndiyo maana swali limekushinda. Sasa unatakiwa uwe makini, hii ni dini.

Ahsante.

Wewe, Qur'an sio kitabu cha visa na ngano za alfu lela ulela.

Qur'an inasema; افلا يتدبرون القران--- je hawaitafakari (Qur'an?? 4:82).

Wewe unataka tusome Qur'an kibubusa bila tafakuri, kila aya inahitaji tafakuri bali kila neno na herufi za Qur'an zinahitaji tafakuri, Qur'an ni muujiza.

Narudia, Wenye akili ndiyo wanaweza kujua maana za maneno ya Qur'an.
 
Kwahiyo Qur'aan inakufundisha uzue na uandike ya uongo ?

Qur'aan haitaki mtu afikiri kwa uongo kama ufanyavyo wewe bali inakutaka upite mule mule alipopita mtume na maswahaba zake.

Sasa rudi kasoma tena na ujifunze kuchukua fasili za mtume wa Allah amani ya Allah iwe juu yake. Hili swali nilijua hutaweza kulijibu, sasa dini haitaki huu ujinga.
 
Qur'an inakutaka usiwe bubusa, inakutaka unaposoma aya zake uzitafakari, mfano Allah anaposema; kuna mitume amehadithia habari zao na wapo hajahadithia habari zao maana yake tunatakiwa tutafakari kwamba ni mitume gani habari zao zimehadithiwa na hizo habari ni zipi na zina faida gani kwetu??!!, na kadhalika hao mitume ambao habari zao hajizasimuliwa walikuwa mitume gani kutoka mahali gani na kwanini habari zao hazikusimuliwa nk, -- ni maswali ya aina hiyo yanayotakiwa kufanyiwa kazi na mtu mwenye AKILI.

Angalia "commentary" kumuhusu Seydna, (Mtawa, Sage) Mchamungu Luqman yanayotolewa na Watu wenye akili ili na wewe ujifunze na uondokane na Ububusa (dogmatism).

Screenshot_20200721-175353.png
 
Duh.! Mungu wenu mbinafsi sana..Una maana vilaza hawataiona pepo.!?

Wanaoingia peponi ni watu wenye akili na elimu, ni wstu waliofanya mema kwa kutumia akili, lakini Allah ni mwingi wa rehema na ukarimu na huruma yawezekana hata wasiokuwa na akili akawaingiza peponi kwa huruma yake,

Yeye Allah ndiye anayejua zaidi.
 
Hahaahaaaaaa
hahaaaaaaaaaaaa
hahaaaaaaaaaaaaaaa
hahahahaaaaaaaaaaaaa
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa
teh teh teh teh teh teh teh teh
nimecheka sana hakika umejua kunifurahisha kwa huu upomoma uliouandika ni dhahiri shahiri hizo ndo akili zako complete nyie ndo wale wale wanaoziba kwa wenzao ilhari kwao kunamatundu makubwa mnooooo

Tunakazi ya kuzipeleka na akili za watu uchumi wa Kati
 
We umejuaje Sasa kama huyo mo hakuhadithiwa?? AU Allah alikuhadithia wewe au umeamua tu kusema kuwa tuliletewa

Sikia jinsi Mungu anavyomuambia Mtukufu mtume Muhammad (saw) ndani ya Qur'an kuhusu mitume wa kabla yake, Allah anasema kumuambia Mtume Muhammad (saw):

"Na kwa yakini tuliwatuma mitume kabla yako, wengine tumekusimulia na wengine wao hatukukusimulia---"

(Qur'an 40:78).

Katika hadithi moja ya mtume (saw), anasema wamepita kabla yake mitume 124,000, katika Qur'an wametajwa mitume 25 hivi, sasa jiulize, 124,000 -- 25=123,975, hao mitume 123,975 walitumwa kwa ajili ya kina nani???, au walitumwa kwa ajili ya Manyani na sokwe na nguruwe ili wamuabudu Mungu??!!, very hillarious.🤣🤣
 
Qur'an inakutaka usiwe bubusa, inakutaka unaposoma aya zake uzitafakari, mfano Allah anaposema; kuna mitume amehadithia habari zao na wapo hajahadithia habari zao maana yake tunatakiwa tutafakari kwamba ni mitume gani habari zao zimehadithiwa na hizo habari ni zipi na zina faida gani kwetu??!!, na kadhalika hao mitume ambao habari zao hajizasimuliwa walikuwa mitume gani kutoka mahali gani na kwanini habari zao hazikusimuliwa nk, -- ni maswali ya aina hiyo yanayotakiwa kufanyiwa kazi na mtu mwenye AKILI.
Nimecheka sana, ukiona mambo ambayo Allah hajayafunua kwa mtume ujue hakuna anae weza kuyaweka wazi, matumizi sahihi ya akili ni kujua ya kuwa hutakiwi kubahatisha na kufungua mlango wa uzushi.

Mathalani ili uone akili ina mipaka yake, mpaka unakufa huwezi kututhibitishia ya kuwa hao mitume ambao Allah hakuwataja walikuwepo Afrika na nchi nyingine ulizo zitaja. Bali Allah ndiye mjuzi wa ya dhahiri na yaliyo fichikana.
Angalia "commentary" kumuhusu Seydna, (Mtawa, Sage) Mchamungu Luqman yanayotolewa na Watu wenye akili ili na wewe ujifunze na uondokane na Ububusa (dogmatism).
Sasa watu wenye akili kwanza hufanya haya yafuatayo, nitakuuliza hizi habari umezipata, na na nitakwambia yale aliyo yasema mwanachuoni mbora Muhammad bin Sirin, habari hizi una zipata katika kitabu "Muqadima fi Sahih Muslim" cha Imam Muslim bin Hajaaj Allah amrahamu. Na mimi nakuuliza hivi tutajie wapokezi wa hii habari ya Mja wa Allah Luqman mwenye Hekima.

Sasa sababu wewe ni kiokote kwa ujinga wako una chukua kila kipitacho mbele yaki, halafu unajinadi kwamba unatumia AKILI.

Swali langu la msingi nataka uniambie hii "Commentary" imenukuliwa toka kwa nani na utuonyeshe usahihi wake uko wapi na kwa mujibu wa nani...?

Nikirudi natarajia nikute majibu hayo.

Ahsante sana.
 
Hahaahaaaaaa
hahaaaaaaaaaaaa
hahaaaaaaaaaaaaaaa
hahahahaaaaaaaaaaaaa
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa
teh teh teh teh teh teh teh teh
nimecheka sana hakika umejua kunifurahisha kwa huu upomoma uliouandika ni dhahiri shahiri hizo ndo akili zako complete nyie ndo wale wale wanaoziba kwa wenzao ilhari kwao kunamatundu makubwa mnooooo

Tunakazi ya kuzipeleka na akili za watu uchumi wa Kati

Hata Firauni alicheka kicheko cha aina hiyo pale Nabii Musa (as) alipomuambia kwamba yeye ni Mtume ametumwa kwake na Allah, Firauni akakebehi na kumwambia waziri wake Hammana amjengee mnara mrefu ili akamuone Mungu wa Musa.

Hebu soma hiyo aya na uone kama wenye elimu (akili) ni sawa na wasiokuwa na akili, (bila akili hupati elimu).

Screenshot_20200721-211806.png
 
View attachment 1513123

Kwa mantki iyo hakuna chizi wa kibaiolojia anaeweza uridhi ufalme wa allah ?
 
na nitakwambia yale aliyo yasema mwanachuoni mbora Muhammad bin Sirin, habari hizi una zipata katika kitabu "Muqadima fi Sahih Muslim" cha Imam Muslim bin Hajaaj Allah amrahamu. Na mimi nakuuliza hivi tutajie wapokezi wa hii habari ya Mja wa Allah Luqman mwenye Hekima.

Na wewe kiokote kutoka kwa huyo mwanazuoni wako, thibitisha usahihi wa hayo uliyoyaokota kutoka kwake.

Quran (Allah) anatutaka tutumie akili katika kutafakari maudhui aya zake, wewe kwa ujinga na ububusa wako unadhani akili ulizopewa ni kwa ajili ya kukariri aya za Quran na kuvukia barabara tu, akili uliyonayo ni ya "Majini-paka" na "Majini- nyoka", akili yako imelala doro.

QUR'AN inahitaji wetu wenye akili na sio Mabubusa.

Eti kwa mawazo yako ya hovyo; kipindi nyimati za mashariki ya kati wamepewa manabii kuwaongoza kumcha Allah huku Africa na sehemu zingine za dunia hakukuwa na watu waliohitaji Muongozo kutoka kwa Allah!!!??--- a shere stupid imbecility, sisi waafrika tulikuwa na laana gani kipindi hicho tukakosa neema ya manabii???, je tulikuwa kama wanyama au zama hizo huku hakukuwepo na watu ??!!.

Mjinga hawezi kujiuliza hayo maswali bali mwenye akili ya kutafakari maneno ya Allah.

Allah akuongize, akuondolee kibri cha "ujuaji" unyenyekee kwake ukilia kwa machozi huku ukiomba dua hii; "Ee mola wangu mimi sijui kitu nawe ndiye mjuzi wa kila kitu nizidishie elimu na uniruzuku ufahamu".
 
Na wewe kiokote kutoka kwa huyo mwanazuoni wako, thibitisha
Hili kwangu rahisi sana, sababu huwa nakujua ni mtu wa kukimbia maswali, wewe nithibitishie kisha nakuwekea ushahidi.
Quran (Allah) anatutaka tutumie akili katika kutafakari maudhui aya zake, wewe kwa ujinga na ububusa wako unadhani akili ulizopewa ni kwa ajili ya kukariri aya za Quran na kuvukia barabara tu, akili uliyonayo ni ya "Majini-paka" na "Majini- nyoka", akili yako imelala doro.
Safi kabisa, kweli kabisa Qur'aan inatutaka tufikiri tena sana, ila tufikiri kwa usahihi, na hakuna tafakari mbele ya nususi za kiseheria yaani Qur'aan na Hadithi, Qur'aan inapo hukumi jambo na kuliweka wazi hapo akili yako inatakiwa kufata jambo hilo na kulifanyia kazi kwani hakuna kinyume chake. Qur'aan iliposema ya kuwa kuna habari za mitume wengine mtume hajafunuliwa ujue hakuna anae zijua habari hizo ila Allah peke yake, na akili yako inatakiwa ifanye na kukiri utukufu wa Allah.
QUR'AN inahitaji wetu wenye akili na sio Mabubusa.
Qur'aan inataka wenye kutumia akili na kufanya tadaburi na haiwataki wenye akili, kwani hata wewe una akili ila bado ni zwa zwa na hufikirii kwa usahihi, hakuna aya inayosema Qur'aan inataka wenye akili, bali wenye kutumia akili na kutafakari.
Eti kwa mawazo yako ya hovyo; kipindi nyimati za mashariki ya kati wamepewa manabii kuwaongoza kumcha Allah huku Africa na sehemu zingine za dunia hakukuwa na watu waliohitaji Muongozo kutoka kwa Allah!!!??--- a shere stupid imbecility, sisi waafrika tulikuwa na laana gani kipindi hicho tukakosa neema ya manabii???, je tulikuwa kama wanyama au zama hizo huku hakukuwepo na watu ??!!.
Nacheka sana, usipate shida, weka ushahidi bwana mdogo.

Mimi nipo hapa nasubiri huo ushahidi.
Mjinga hawezi kujiuliza hayo maswali bali mwenye akili ya kutafakari maneno ya Allah.
Wenzako Mayahudi walipotea kwa sababu ya kuuliza uliza maswali, siyo tu maswali bali walikuwa wana uliza maswali ya kijinga kama haya uliyo uliza wewe na yanao nyesha huujui Uislamu, kwahiyo hatuangalii kuuliza maswali bali tunaangalia unauliza nini na je umepatia kuuliza hayo maswali, kwa ujinga wako wewe unaweza kuuliza "Je yule mbwa wa vijana wa Pangoni, alikuwa jike au dume au alikuwa ana rangi gani ?" kisha ujione kwamba una akili, aisee Qur'aan haitutaki tuhoji ujinga bali tuhoji vya maana.
Allah akuongize, akuondolee kibri cha "ujuaji" unyenyekee kwake ukilia kwa machozi huku ukiomba dua hii; "Ee mola wangu mimi sijui kitu nawe ndiye mjuzi wa kila kitu nizidishie elimu na uniruzuku ufahamu".
Safi.

Sasa tuletee ushahidi wa ile "Commentary" uliyo tuwekea, kijana huwa una tabia ya kutia huruma sana baada ya kuona mambo yamekuwa magumu kwako na kuanza kunitupia lawama za "Ooh najiona mjuaji mara Ooh nina kibri".

Sasa Itifaki lazima izingatiwe, hii dini imekamilika na hatutaki vya kuzua.
 
Kwa mantki iyo hakuna chizi wa kibaiolojia anaeweza uridhi ufalme wa allah ?

Hapa hatuongelei juu ya Wagonjwa ambao hao wana udhuru (an excuse).

Tunaongelea juu ya watu wasiotumia akili zao vyema, hao ndio wasiokuwa na akili, hatuzungumzii wehu (wagonjwa wa akili). Mtu mwenye akili ni yule anayetumia uwezo wa ubongo wake ipasavyo kutafakari mambo yaliyolazimishwa kufanyiwa tafakur, mfano Allah ametuasa katika sehemu mbalimbali ndani ya Quran tuzitafakari aya za Qur'an, na hayo ndiyo matumizi bora ya ubongo aliotujalia Allah mwenyewe.

Kuhusu huyo mginjwa wa akili Nimekuambia, Allah ni mrehemevu, msahemevu na mpole na pia ni mbora wa kuhesabu, basi ni yeye atajua amfanye nini huyo kiumbe wake, na bila shaka atamsamehe madhambi yake kwani mtu huyo anao udhuru.

الله يعلم
 
Safi kabisa, kweli kabisa Qur'aan inatutaka tufikiri tena sana, ila tufikiri kwa usahihi, na hakuna tafakari mbele ya nususi za kiseheria yaani Qur'aan na Hadithi, Qur'aan inapo hukumi jambo na kuliweka wazi hapo akili yako inatakiwa kufata jambo hilo na kulifanyia kazi kwani hakuna kinyume chake. Qur'aan iliposema ya kuwa kuna habari za mitume wengine mtume hajafunuliwa ujue hakuna anae zijua habari hizo ila Allah peke yake, na akili yako inatakiwa ifanye na kukiri utukufu wa Allah.

Matumizi ya akili ni kutaka kujua je hao mitume ambao mtume hakuambiwa habari zao ni mitume gani??, na walikuja wapi?? Kwa kazi gani??, usipojiuliza maswali hayo na mengine kama hayo wewe ni mfu wa akili, huna tofauti na punda abebaye vitabu asijue ndanimo kuna nini.
 
Naona unarudia utoto na ujinga ule ule.

Nasubiri shahidi na majibu ya maswali yangu.

Ahsante.
 
Qur'aan inataka wenye kutumia akili na kufanya tadaburi na haiwataki wenye akili, kwani hata wewe una akili ila bado ni zwa zwa na hufikirii kwa usahihi, hakuna aya inayosema Qur'aan inataka wenye akili, bali wenye kutumia akili na kutafakari.

Mjinga wewe, maneno: Afalaa taa'kiluun???, nini maana yake??
Qur'aan inataka wenye kutumia akili na kufanya tadaburi na haiwataki wenye akili, kwani hata wewe una akili ila bado ni zwa zwa na hufikirii kwa usahihi, hakuna aya inayosema Qur'aan inataka wenye akili, bali wenye kutumia akili na kutafakari.

Sasa asiyekuwa na akili anaweza kutumia akili???--- wewe kweli sio mjinga tu bali ni zezeta pia.
 
Back
Top Bottom