Nakupenda hadi naumwa! Ila sio kwa kukuoa maana kwa utashi tulionao kila mmoja wetu atataka afuate upande wake kwa kuona ndio yuko sahihi zaidi, balaa litaanzia pale tutakapopata watoto, kila mmoja atapenda watoto wafuate upande wake, hii haiwi?! dhahiri bali kwa siri. Balaa zaidi ni pale tutakapoachana kila mmoja atang'ang'ania watoto ni wake na kutaka wafate upande wake kwa kuona ndio yuko sahihi, bado kwenye maswala ya mirathi na mambo mengine. Kwanini tu nisimpende mtu wa upande wangu, kiasi kwamba hata kama tukiachana watoto bado wako upande wetu, mirathi pia itafanyika kwa mujibu wa upande wetu pamoja na mambo mengine yote yatafanywa kwa mujibu wa imani yetu??