Diaspora wanatamani sana kuwekeza Tanzania tatizo watanzania wengi sio waaminifu

Hyrax

JF-Expert Member
May 20, 2023
604
1,534
Leo naandika kwa masikitiko makubwa kuhusu hali ya watanzania wengi kutokuwa waaminifu kwenye mambo ya msingi hasa yanayohusu pesa, kuna taarifa nimezipokea kutoka kwa rafiki wa rafiki yangu kwamba kuna rafikiye alipata connection ya kuingia partnership ya kibiashara na mtanzania mmoja aishie nchi za ulaya(Diaspora),

Diaspora huyo alikubaliana na jamaa(mtanzania) kuwekeza kwenye biashara fulani hapa bongo Diaspora huyo atatoa fedha (mtaji) na huyu mtanzania mwenzetu huyo atakuwa anasimamia mradi wa biashara hiyo na mpaka kufika disemba 2022 diaspora huyo alitoa zaidi ya milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wa kibiashara na huyo mtanzania mwenzetu.

Yaani mpaka ninavyoandika muda huu mtanzania huyo aliyepewa kitita hicho cha pesa hapatikani kwenye simu, hapatikani popote toka mwezi wa kwanza mwaka huu wa 2023 huku juhudi za kumpata zinaelekea kugonga mwamba na kukatisha tamaa na kwa mujibu wa taarifa mpaka sasa diaspora huyo kwasasa amelazwa hopitalini huko ulaya kwa kuwa presha ipo juu na sukari ipo juu.

Mbali na stori hii kuna shuhuda za watu kadhaa huko nyuma nimewahi kuzishuhudia wakipigwa matukio na watanzania wenzao jambo ambalo ni baya sana katika maisha yaani baya sana ukishakuwa sio mwaminifu mabalaa yatakuandama tu ni suala la muda tu.

Mpaka sasa naweza kuamini kuwa watanzania wengi ni maskini, wagonjwa wa maradhi mbalimbali kwasababu ya kukosa uaminifu, hata hawa mnawaona amefanikiwa wengi ni maskini kwenye mambo mengi kwasababu ya wizi na udanganyifu, mtu ana milioni 100 benki ila furaha hana, magonjwa yanamsumbua na mabalaa kibao yanamsumbua kwenye maisha yake tatizo nini ? UAMINIFU

Mithali 13:21 (NEN): Balaa humwandama mtenda dhambi, bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.​

 
Huwezi wekeza 200m mahali ujaenda na kuona wakati unaendelea kutoa hela, kila mahali kuna matapeli, Hata Marekani.
 
Wawatumie waislam kwa uwekezaji wa mbali.

Wengi wao niwaaminifu,wamefunzwa kuheshimu vya Watu na wanaogopa albadir.
 
Hizi story za vijiweni usituletee humu. Hakuna mtu yeyotealiyetafuta milioni 200 akaipata na akaamua kuwekeza kwa kumkabidhi mtu kiholela just like tye way unavyoisimulia. Hakuna.

Acheni kukatisha tamaa vijana kwa story za kufikirika.
 
Back
Top Bottom