Serikali hamasisha Watanzania kucheza Green Card ili tupate diaspora wengi. Ina faida za kiuchumi

Aug 4, 2011
82
80
Moja ya nchi ambayo ina wananchi wake wanaoishi ugaibuni (USA, German, Italy, France, Canada, Australia, Norway, Spain, Denmark n.k) ni Tanzania. Ukiangalia Watanzania wanaoishi nje ya nchi idadi yake tunazidiwa na Somalia.

Ukiachana na nchi kama Kenya, Misri, Sudan, South Africa na nyinginezo kwa nini Watanzania wengi hata mchezo wa bahati nasibu ya kushinda na kuhamia Marekani hawaijui kabisa, kitu ambacho wanaoomba kushinda bahati hiyo ni wachace sana.

Kwa makadirio ya haraka Watanzania wanaoomba hiyo bahatai nasibu sio zaidi ya 6000, wakati nchi jirani ya Kenya wanaoomba ni zaidi ya 800,000 hadi milioni moja. Ukiangalia Ghana na Misri wanaoomba ni zaidi ya milioni 1.5!

Watanzania wengi wakishinda na kuhamia ugaibuni wana faida kubwa kwa uchumi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na uwekezaji. Ukiangalia nchi kama Somalia, uchumi wao unajengwa na Diaspora (watu wanaoishi nje ya nchi yao especially Ulaya na Marekani).

Mkiomba wengi na ndio mnavyoshinda wengi. Nchi nyingi za Kiafrika zina mkono wake kuwawezesha wananchi wao kucheza kwa wingi Green Card na wanashinda kwa wingi. Hivyo wakiahamia Marekani wanarudisha uchumi wao makwao.

Naiomba serikali kuchangamkia fursa hii muhimu kwa kuhamasisha wananchi wake kucheza hii bahati nasibu ili wakipata nafasi na kuhamia Marekani warudishe chumi zao nyumbani kwao.

Kuna Mtanzania mmoja anayeishi Marekani na tayari ameshakuwa raia wa taifa hilo anaitwa Ernest Makulilo anafanya kazi kubwa sana kuhamashisha Watanzania wengi kuomba Green Card. Inaonesha inamuuma sana akiona nchi nyingine wanashinda wengi na Tanzania tupo tu ili mradi siku zinaenda.

Anawasisitizia sana Watanzania waombe kwa wingi ili waweze kupata nafasi ya kuishi ugaibuni. Ukiingia kwenye mitandao yake ya kijamii kama Facebook na YouTube kwa kija na IBM Scholars/Swahili utaona anavyojitahidi kuhamasisha Watanzania kucheza green card ili waweze kwenda na kuishi Marekani.

Amepost clip nyingi zenye miongozo ya jinsi ya kucheza green card na kushinda. Mwenyezi Mungu ambariki sana kwa jinsi anavyojitoa kuwaelimisha Watanzania kuwa Diapora. Watanzania tusilale jamani, tucheze kwa wingi ili wakishahamia ugaibuni waweze kurudisha uchumi nchini mwao.

Ukiangalia Mh. Rais akienda kukutana na Watanzania waishio Marekani, anakutana na Watanzania wachache sana wanaoishi huko ukilinganisha na Rais wa Kenya anapokutana na wakenya waishio Marekani.

Wakenya wengi wanaishi nje ya nchi yao hususani Marekani na Ulaya. Watanzania wakicheza green card 6000 wanaoshinda kuanzia 150-350 kwa mwaka 2023.

Naiomba serikali ilifanyie kazi hili, maana faida zake ni kubwa kuliko.
 
Mkumbuke wengi wa diaspora kulinganisha nchi na nchi kutoka bara la Africa ni WAKIMBIZI. Nchi yetu hatujapitia yale nchi nyingi zimepitia.

Somali Ethiopia Kenya Rwanda Burundi DRC Sudan(kusi na kaskazini) Uganda Nchi nyingi West Africa zilizo na migogoro baki ya Nigeria na Ghana ( hawa ni opportunists) etc.

So tusijiulize kwa nini WaTz si wengi nje ya nchi.. Huko nje sio kuzuri kiviiille. Tusisukumane.

TUMEBARIKIWA mbali na changamoto tunazopitia chini ya utawala wa sisiem..
 
Back
Top Bottom