Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Huyu hata ukiisikiliza miziki yake utajua uwezo wa akiri yake uko vip ...alipiga kura kwa mdee ama aliwapigia CCM leo anajiweka CDM
 
Usipanik please, kanunue bidhaa kutoka kwenye duka lenye EFD hata kama ni penseli utaona kodi unayolipa. Kajifunze aina za kodi kwanza ndio uje hapa. Mdee lazima ajifunze..kuna haki na wajibu, sie tumemchagua yeye awakikishe matatizo yetu. Wanaowakilishwa vizuri wamefanikiwa

Tunaomba utusaidie huko kuwakilisha vizuri na kuwasilisha vibaya kukoje kwani!!!.
 
Watanzania wenzangu, mbunge huwa anapeleka mahitaji yake kwa waziri husika, swala si ushawishi kwa serikali. je Mbunge anabadget ya ujenzi wa barabara?
 
Wenzake wasanii waliopata fedha wanaajiri washauri wakuwafundisha nini cha kusema kwenye public hasa kama elimu na upeo wa maarifa vimekupita pembeni. Kama hao clouds wamemtumia bila kujua kauli hii yaweza Kumponza.
 
Diamond hata hajui kama kuna serikali, elimu yake darasa la sita au form 3; Mdee achukue fedha zake na familia yake kujenga barabara??? fikiria tena
 
Kama wewe ni mbunge na katika jimbo lako kero hazitatuliwi, ujue tu hauna ushawishi.

Katika hali hiyo ya kukosa ushawishi, basi hufai kuwa mwakilishi wa wananchi husika. It's simple as that.

Halima, time to go!

Unamshawishi nani tuambie? Sisi wananchi tunajua jinsi wabunge wetu walivyoweka bidii kufuatilia mambo ya maendelea ya nchi hii ikiwa ni pamoja na barabara, huduma za maji, na huduma zingine mbalimbali za kijamii. TRA wakikusanya kodi zetu wanaipekekea serikali ya ccm. Hivi mkizila hizo pesa na kukaidi kufanya miradi ya maendekeo ikiwa ni pamoja na barabara inayoelekea nyumbani kwa msanii huyo mmataka tuwalaumu wabunge wa chadema!. Nyinyi ni walewale ambao huwa mnafanya kiburi kutosikiliza matakwa ya madaktari halafu wakigoma na wananchi wakafa hospitali mnaanza kurusha lawama kwa madaktari! Duu! kweli ccm mna mbinu chafu.
 
Huyo mzinzi anazidi kujishushia hadhi yake nafuu angekaa kimya tulimshuhudia akimwaga fedha pale Dar live kutaka sifa kama anajua umuhimu wa miundombinu fedha hizo anazomwaga hovyo hovyo si angewekeza kwenye miundombinu kuliko kutoa maoni ya kijinga kama haya pia huyu huyu ndiye anayepanda kwenye majukwaa ya CCM kutoa burudani na alituambia kuwa yeye kuingia Ikulu ni kama nyumbani si angeenda huko Ikulu akaombe wajengewe barabara.
 
Wana Ukumbi,

Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.

Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.

Akiongeza uwezo wa macho yake ya akili (mind) kuona, atakuta kuwa JK ambaye ni swahiba wake ndio tatizo!!
 
si ni billionare huyo ajenge barabara kwa kutumia pesa zake mwenyewe
 
hahaa halima anatakiwa kujenga barabara ya madale toka kwenye vyanzo gani vya mapato?? kila anapoenda nyumbani kwa mkuu wa kaya hakumbuki kumwambia madale hakuna lami anaishia kupiga picha za kupost IG tu.... huyu mwisho atamlaumu halima hata kwa ule ukuta wa nyumba yake uliodondoka......
kweli ukisikia akili za kukopa ndo hizi
 
Domo akae kimya tu,bilionea unajenga ukuta ambao ukija upepo unadondoka? Bilionea unakaa kwenye kiwanja kama kiganja ambacho hata hakijapimwa?
Hasira za nini? Nyuma na ukuta si dhani kama ni mada. Mada ya ukuta wake kuangua ilishaletwa humu watu wakaipotezea kwa kukosa mshiko. Hiyo mada peleka magazeti ya shingongo na michuzi blog
 
Halima kazi yake kelele na matusi siyo kuendeleza watu wake.
 
Wenzake wasanii waliopata fedha wanaajiri washauri wakuwafundisha nini cha kusema kwenye public hasa kama elimu na upeo wa maarifa vimekupita pembeni. Kama hao clouds wamemtumia bila kujua kauli hii yaweza Kumponza.

Kama anapendwa anapendwa tu. Ondoa uchawi wako na uganga njaa wako hapa!
 
Wana Ukumbi,

Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.

Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.

ni vizuri kuliangalia suala hili kwa kuzingatia context ya ahadi. ninaamini Halima alitoa ahadi hiyo akiwaomba wapiga kura waichague Chadema kuunda serikali.

sasa huyu dogo inabidi lawama zake azielekeze kwa serikali ya JK & CCM aliyoipigia debe wakati wa kampeni iliyomwahidi maisha bora!
 
hahaa halima anatakiwa kujenga barabara ya madale toka kwenye vyanzo gani vya mapato?? kila anapoenda nyumbani kwa mkuu wa kaya hakumbuki kumwambia madale hakuna lami anaishia kupiga picha za kupost IG tu.... huyu mwisho atamlaumu halima hata kwa ule ukuta wa nyumba yake uliodondoka......
kweli ukisikia akili za kukopa ndo hizi
Kunapesa inaitwa mfuko wa jimbo anafanyia nini au kulewa ndiyo matumizi menyewe?
 
Watu wanajua kupaisha mada kweli. Diamond hakusema kitu kama hicho jana.
wakati anahojiawa na Haris Kapinga wa Clouds Tv jana asbh Diamond aliulizwa una nini la kuiambia serikali na watawala. Akasema serikali ijitahidi kutimiza ahadi inazozitoa kwa wananchi akachomekea na hilo la barabara ya Madale akasema Halima mdee hebu fanya mambo barabara inatisha ile. Hapa alimaanisha Mdee akaisimamie serikali kuhusu ahadi ya barabara hii.
 
Back
Top Bottom