Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah

"machungu sana"

Diamond is doing very well, he is way better financial, humzidi hata ukijumlisha ukoo wako wote na ukoo kwa mkweo humzidi.

Kama hiyo ndo akili ya drugs, acha avute, maana yako timamu haijakufikisha popote zaidi ya kukusaidia kupata uchungu

Diamond was asked once kama anatumia madawa, alikataa, akasema hatumii, in that case nachagua kuamini maneno yake kwamba hatumii.
 
Acheni ulozi, madawa hata trump anatumia. Kuna madawa classic hayana madhara sio hayo wanaotumia watoto wenu huko kinondoni
Screenshot_20231028-115345.png
 
Tatizo unaongea theory. Watu wapo wanaishi kwa madawa kwa zaidi ya 30years ww unakuja kunipa jibu la chatgpt? Unacomment kuhusu kitu usichokijua ndo maana umeenda chatGPT
Unadhani waliokaa chini wakatengeneza algorithms za chatgpt unaweza ukawa nao sawa kiakili kama unawaza madawa ya kulevya yapo ambayo ni "classic" yasiyo na madhara.
Hiyo ni program imekupa jibu jepesi ambalo akili yako imeshindwa kutafakari.
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Wanasrma huwapa nguvu kwenye kazi zao yaani hawachoki.

Lakini hudhohofisha mwili zaidi pale yanapo mzidi.

Na asilimia kubwa ya wasanii hutumia hayo mambo.
 
Kwani akifanya vizuri sisi huwa inatuhusu nini? It is not about that “Kufuatilia maisha yake” tunatoa maoni yetu kwa jinsi tunavyoona inafaa na si lazima ayafanyie kazi. Halafu hajashauriwa kitu kibaya brother, tatizo ninini?

Sisi wengine ni mashabiki zake humu, unless wewe ni mgeni JF, Nifah ni mtani wa Jadi wa timu yetu, maoni yake ya leo ni constructive sioni ubaya.
Ni ujinga mtu kufuatilia jambo ambalo halitamnufaisha kwa namna yoyote ile.

Sikusema kama ni ushaur mbaya ila kinachonishangaza mim mtu anatoa wapi mda wa kufuatilia mambo ya watu?

Mda ni mali unapoona mtu asubuh asubuh badala kufanya mambo yake ya maana ila yeye anaamka nakuanza kufuatilia mambo yatu ujue kuna tatizo mahal.

Me sio mgeni apa jukwaani nipo kitambo sana na hii sio ID ya kwanza kutumia mara nyingi hupenda kusoma tu labda mara moja moja weekend nikiwa home siendi kazin ndo kama ivi napananikisha watu apa jukwaani
 
Mama yake anachojali ni kijana wake awe single ili awe na uhakika wa kuzitumbua mali za mwanae. Akioa au kuwa kwenye mahusiano hatakua na nguvu kwenye mali za mwanae. Hivyo nguvu nyingi anawekeza kuvunja mahusiano yoyote serious ya jaba
Tukubaliane kuwa yule mama yake naye ni tatizo kubwa, hivi halioni hilo kwa mwanae? Ameweza kucontrol mangapi ya Diamond hilo limshinde? Diamond ana access na wataalamu wa kila aina angetaka wamsaidie kuishinda addiction asingeshindwa.

Diamond wa kipindi cha wema alikuwa amekonda bado kapauka pauka kiasi, Diamond wa kipindi cha Zari alikuwa ana ka mwili, anavaa smart anapendeza, akivaa suti inakaa, huyu Diamondi wa Tanasha na wa Zuchu aisee pamoja na hela zote hatazamiki, kakondeana, ngozi imevutika, ana mirasta yaani haeleweki.

Anyways: It is never too late, kama ni addict kweli bado ana nafasi ya kupona, watu wake hawawezi kumwambia ukweli yamkini wanafaidia na yeye kuwa alivyo. Na pakisambaratika kila mtu atabeba mbao zake atasambaa!

Binafsi ntasikitika sana tukimpoteza huyu kijana wa Tandale aliyefanikiwa kufika mahali ambapo wasanii wetu hawakuweza kufika, “Super star”.
 
Unadhani waliokaa chini wakatengeneza algorithms za chatgpt unaweza ukawa nao sawa kiakili kama unawaza madawa ya kulevya yapo ambayo ni "classic" yasiyo na madhara.
Hiyo ni program imekupa jibu jepesi ambalo akili yako imeshindwa kutafakari.
ChatGpt 3.5 haina Nguvu sana ki algorism kama chatGPT4 ...
Na Bard ni bora zaidi ki Algorism kuliko ChatGpt kwa sababu ya RNN
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?

Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Pathetic thinking
 
Back
Top Bottom