Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Huu ni msiba wa kujitakia na sidhani kama ni rahisi kumrudisha mtu mwenye addiction ya madawa refer Chid Benz,Pauline Zongo nk naona jamaa kaamua kujimaliza mwenyewe, Walaumiwe management/familia yake kwa kutomsaidia mwanzoni tu alipoanza, kama ni kweli basi tushampoteza Guavo low budget,Ni suala la mda tu tutaanza kuambiwa pray for Guavo
 
Huu n mwaka wa sita km c wakumi mnaimbaga wimbo huo huo mara anatumiaa madawa mara n freemason ,mara anawala wenzie jicho ,

Ss ww dai afanye yt ww unapata tabu gan mkuu hapo ulipo ,,

Acha kupangiaa mwenye Hela zake starehee yakufanyaa..
Kijana hata Kipindi zilipo anza tetesi Chid benz ana bwia unga hakuna aliyekubali na watu walisema sana na ilikuwa vigimu kukubali lakini baada ya miaka mingi ya sasa kila kitu kilikuwa hadharani….
Kuna kitu hakiko sawa kwa Diamond kwa sasa hata ukimuangalia unajua kuna shida fulani….
Kama kweli hatumii basi Diamond kuna shida ya kiafya anayo lazima tukubali amepungua sana kila kukicha…..
Watu wakisema jambo lazima kuna viashiria vimeanza kuonekana…..
Muda ni mwalimu mzuri sana sana…….
Diamond ana muda wa kubadilika kama ni kweli au kushughulikia kila kinachoonekana kwa watu…
Maana hapa sote tunakubaliana kuwa Diamond ame loose weight …na inaonekana wazi shida ni nini?

Hawa watu wote wanaosema hawawezi kuwa vichaa au haters…..
Nafikiri hizi taarifa zinapaswa kufanyiwa kazi vizuri na watu wa karibu na Diamond….!
 
Huu ni msiba wa kujitakia na sidhani kama ni rahisi kumrudisha mtu mwenye addiction ya madawa refer Chid Benz,Pauline Zongo nk naona jamaa kaamua kujimaliza mwenyewe, Walaumiwe management/familia yake kwa kutomsaidia mwanzoni tu alipoanza, kama ni kweli basi tushampoteza Guavo low budget,Ni suala la mda tu tutaanza kuambiwa pray for Guavo
Kwanini asilaumiwe mwenyewe? Kama ni kweli anatumia.
 
Ni ujinga mtu kufuatilia jambo ambalo halitamnufaisha kwa namna yoyote ile.

Sikusema kama ni ushaur mbaya ila kinachonishangaza mim mtu anatoa wapi mda wa kufuatilia mambo ya watu?

Mda ni mali unapoona mtu asubuh asubuh badala kufanya mambo yake ya maana ila yeye anaamka nakuanza kufuatilia mambo yatu ujue kuna tatizo mahal.

Me sio mgeni apa jukwaani nipo kitambo sana na hii sio ID ya kwanza kutumia mara nyingi hupenda kusoma tu labda mara moja moja weekend nikiwa home siendi kazin ndo kama ivi napananikisha watu apa jukwaani
Sasa huu muda wa kuandika haya wewe una utoa wapi? Kwa taarifa tuu hii si mara ya kwanza hili jambo kuja hapa…! Wanasema jambo likisemwa sana linapaswa kuangaliwa kwa jina la pili zaidi hakuna ubaya kwenye hili….! Mtoa mada kaandika jambo zuri sana na nina hakika watu wa karibu na Diamond lazima walifanyie kazi!
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Hivi unaamini kabisa kama ni kweli anatumia madawa ataacha sababu umeandika thread humu ndani?
 
Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Umeandika insha ndefu, lakini hujajua kuwa that nigga's soul belongs to the devil, he sacrificed his soul to the devil

Anza kwa kumuombea kwa Mungu amuondoe huko kwanza, maana kwa sasa nafsi yake ni mateka...
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha ya
Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Wewe ni mpumbavu na isitoshe wewe ni teja mtumiaji.

Wewe unafikiri kwa nini serikali inapambana kudhibiti madawa ya kulevya kwa watu?

Kama mtu kutumia madawa ya kulevya ni "Maisha ya mtu" kwa nini serikali iingilie kati kupambana na wauzaji madawa ya kulevya?

Kwa nini isi ingilie walevi wanywa pombe?
 
Hilo mimi nilipoanza kulisikia nikaanza kumtazama sana kwenye youtube, kuna ukweli kwenye hilo, Diamond hata kuongea kwake kumebadilika, anaongea kama teja kabisa.

Chanzo kikuu kinachowasibu hawa vijana ni kutaka kuonesha udume kwa njia yoyote ile kwenye ufuska.

Tumuombee abadilike, hakuna ataeweza kumbadili isipokuwa yeye mwenyewe. Lakini hali ni mbaya kweli, mpaka kubadilika namna ya kuongea, ni pakubwa si padogo.

Inatisha.
Kwanini bibi usiendee kuongea na kikongwe mwenzio Mama Dangote mkamshauri kijana?
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?

Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Sijawahi kuona Elijah mpumbavu kama wewe. Badili jina ujiite Faiza.
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Kuna ulevi ukitumia kujitoa ni ngumu sanaa..
Nacho jua mtu yoyote anae tumia kilevi chochote for recreational purpose na Kwa kiasi (kipimo itamchukua muda sanaaa kuweza kuharibikiwa)

Hii haina ubishi uki istimulate akili Kwa Madawa uwezo wa kufikili ,akili,maarifa na upeo Huwa mkubwa na waajabu shida utaanza kuongeza mdogo mdogo mpaka unaaribikiwa Hawa watu nyuma ya pazia na mioyon mwao wamebeba vitu vingi sanaa....

Nina story ya brother angu mmoja yeye aliondoka home miaka 32 iliyo pita akawa maarufu sana na currently ana miaka 50 na ushee NDIO amekuja juzi kupatikana jamaa ni sharobaro balaa ni kama Kina Jay Z, P.diddy na Birdman
Madawa ya kulevya ni hatare sana
 
Back
Top Bottom