Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,531
65,298
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.

Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.

Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!

Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida. Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano. Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya...
Vigumu Kuacha Madawa Bila kwend Rehab
 
Uzi wako umenipa mixed feelings
Nimecheka hapo ulipoandika chanzo chako kikikuambia kesho unafariki unaanza kutubu

Nimeshuka para hapo ulipoanza kwa kumtaja kwa jina lake Naseeb kisha ujumbe wake nimejikuta napatwa na goosebumps...nimesikia uchungu

Hope ujumbe utamfikia,kama ni kweli aamue kuacha
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki kila kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
hata afya yake imekongoroka, uwezo wa kutunga umeporomoka ana flow nyimbo za matusi tu.. he is loosing mentally and physically kila siku.. in 10 years anaweza kuwa vibaya maana balaa la madawa ni kwamba the more you take the more u need it.
wanaomzunguka waache uchawa na upambe wameambie ukweli, family na ma manager wamsaidie..
vita za madawa huwez ishinda mwenyewe , amuulize Lord Eyez katokaje huko.
 
Naseeb Abdul Juma Issack, professionally known as Diamond Platnumz, is a Tanzanian bongo flava recording artist, dancer, philanthropist and businessman. He is the founder and CEO of WCB Wasafi Record Label, Wasafi Bet and Wasafi Media. Diamond has gained a massive following in East and Central Africa.He became the first Africa-based artist to reach 1 Billion views on YouTube.
 
Akivuka umri alioushindwa ivan atakua na bahati sana. Chai jaba ua jeusi lilimchanganya sana hakutegemea kutoswa ndo maana hadi wa leo anamkana yule mtoto aliyesababisha valentine yake iwe ovyo.

Ustaa una gharama kubwa sana,wanaofaidi matunda yake ni watu wa pembeni ,yeye kutwa stress tupu kubuni mbinu za kubaki juu na kuongelewa daily
 
Screenshot_20231028-113108.png
 
Back
Top Bottom