Tatizo wengi hawafahamu historia, wamekuta tu shule zipo na majengo yapo. Shule hii naifahamu ipo ndani ya eneo la Abatia ya Wamisionari Wabenediktini Ndanda (OSB - Order of St. Benedict). Shule hiyo ilijengwa na Watawa Wakatoliki Wabenedictini Kutoka Ujerumani na Uswis na kuendeshwa nao, na kanisa linalozungumziwa lipo ndani ya eneo la shule lilijenga sanjari na majengo ya shule. Ingawa shule hiyo ilitaifishwa na kuendeshwa na serikali, lakini bado ina mapokeo ya waazishaji.
Ni kitu cha kawaida shule kama hizi kukuza na kuenzi waanzilishi na moto ya shule iliyokuwa nayo tangu awali. Si jambo la kuanza kulalamikiwa na waislamu kwamba nao wajengewe msikiti katika eneo la shule vinginevyo shule zote Tanzania zitahitaji kujengewa misikiti na makanisa mashuleni. Kinachoangaliwa kuyaenzi yaliyoanzisho ambayo yanatunza historia ya shule, vinginevyo ni uelewa finyu wa baadhi yetu kufikiria kama walivyozoea kusema kudhulumiwa.
Mbunge Januari Makamba alipokuwa Marekani amesoma shule kama hizo za Wamisionari Watawa (wamonaki) Wabenediktini, napengine alishirika hata baadhi ya vipindi vya dini na wala hakuathirika na leo anaendelea na dini yake bila shida na anashukuru ilmu aliyopata huko na amewahi kueleza kwenye jukwa lake la face book kuhusu dhana hiyo, na kwamba mabarother waliomlea walimsaidia mengi sana wakati wa mwanzoni akiwa na dhiki ya kukamilisha usajiri na karo. Hali kadhalika viongozi wengi tu wamesoma shule za dini tofauti katika ujana wao na leo wengine ni wakulu wa nchi hii, wangefikiria kama wanadhulumiwa leo hii wasingekuwa kama walivyo, ila walijua kilichowapeleka pale ni ilmu si udini. Walimu wao pia walijitahidi kuwamegea ujuzi bila kinga ya dini ila tu jinsi kila mmoja alivyokuwa na ushindani wa kuipata aliifaidi na ndicho tunachotaka.