ni takriban wiki nne sasa wanafunzi 63 wa kiislam wanaosoma shule ya secondary ya ndanda wamesimamishwa na wengine kupewa masharti magumu ili warudishwe ikiwa ni pamoja kutofanya ibada wakiwa eneo la shule, kutozungumzia jambo lolote linalohusu dini yao ilihali wenzao(wakiristo) wanafanya watakavyo ikiwa ni pamoja na kufanya mikesha ktk kanisa lililopo shuleni hapo. Rai yangu ni serikali kutoa fursa sawa ya kuabudu kwa dini zote pia kumchukulia hatua za ni dham mwalim mkuu wa ndanda secondary ambae anafanya ubaguzi na kejeli dhidi ya uislam. Boko haram Nigeria ilianza kama hivi. Tamsya(vijana wa kiislam Tanzania mashuleni na vyuoni) wametoa Tamko la mgomo na maandamano nchi nzima kulaani tukio la ndanda na kutaka wanafunzi waliosimamishwa kwa kuomba eneo la kufanyia ibada warejeshwe mara moja. Utakua mgogoro endelevu mpaka madi ya msingi yasikilizwe. Vibali vya mikusanyiko na maandamano vimeombwa nchi nzima kuanzia siku ya ijumaa iwapo madai yaliyoainishwa hayatatekelezwa mpaka siku ya alhamiisi. Waislam nchi nzima tuungane kwani Hizbullah ni lenye kushinda.