Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,322
- 219,638
Wazungu wasingeweza kuleta Chakula Tanzania ikiwa nchi hii inajitosheleza kwa Chakula , wanayo macho na wanaona hali halisi ya Wananchi
Viongozi acheni uongo wa kijinga , okoeni maisha ya wananchi wenu ambao ni wazi mnajua wana dhiki utadhani nchi iko vitani , mnataka kuficha kitu gani na ni kwa manufaa ya nani ?
Kwa mfano , Wilayani Temeke familia nyingi zinaishi kwa mlo mmoja tu tena wa ugali mkavu , Keko , Tandika , yombo , Buza , Mbagala na maeneo kibao dhiki imetamalaki , ni lini serikali ya Tanzania ilipeleka msaada wa msosi maeneo haya ? mnadhani vijana wanaosoma wana hali gani ?
Eti ushoga ! ni nani aliwaambia ushoga unaletwa na chakula ? kwa taarifa yenu chanzo kikuu cha ushoga , mimba za utotoni , maambukizi ya Ukimwi huletwa na dhiki duni ya kujikimu ikiwemo dhiki ya msosi , Tafiti kibao zimefanyika , kwanini mnaficha ? hebu kueni na huruma pokeeni chakula ili kuokoa raia wenu ambao wengi wamezeeka kutokana na dhiki .
Tunafahamu kwamba nyie mnashiba na Mara zote aliyeshiba hamjui mwenye njaa .
MUNGU WABARIKI WAZUNGU