Dhifa ya Kitaifa na Obama: Mbowe ndani ya mwaliko Ikulu

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF!

Taarifa zilizo nifikia kutoka Ikulu hivi punde zinasema, mhe Mbowe ambae ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, amepata mwaliko Ikulu na hivi sasa ana jumuika na viongozi na watu mashuhuri kupata chakula cha jioni 'dina'.

Mwaliko wa Mbowe Ikulu utaleta sura mpya hasa kwenye siasa zetu za ushindani, kwani kwa hivi sasa ushindani wa siasa umegeuka vita baina ya sisi kwa sisi, huku malengo ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi, ikiwemo kutanua zaidi demokrasi tukiyaweka kando.

Ni imani na matumaini yangu mwaliko wa Mbowe Ikulu utarejesha imani kwa baadhi ya mashabiki wa CHADEMA kwa serikali yao, ambayo imani hiyo ilianza kupotea kwa namna moja ama nyingine.

MBOWE asante kwa kuitikia mwaliko, hatimaye CHADEMA yapata mwakilishi kwenye ziara ya rais Obama.
 
Haya weka mpesa yako upate ujira wa kueneza porojo za lumumba. Slave trade still working... Tafakari, chukua hatua

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hatuna imani na CCM hata Mbowe awe analala Huko Huko IKULU maana CCM Wauwaji tu wanajulikana
 
Hatuna imani na CCM hata Mbowe awe analala Huko Huko IKULU maana CCM Wauwaji tu wanajulikana

Hizo taarifa za kuwa CCM ni wauwaji amekupa nani?

Kama hao wanaokupa taarifa wanakaa meza moja na kula na wanao watuhumu kuwa mauwaji, wewe bado unaendelea kuamini tu?
 
Ulisikia maneno ya Obama kuhusiana na demokrasi? Hapo hajaalikwa na serikali hii bali kaalikwa na US. Kwanza utasemaje dhifa ile ni yetu wakati mpaka getini wako Wamarekani?
 
Mayala pascal at work loading......................................................................................
 
ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa I am speech less!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mbowe ni noma tupu masikini slaa!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Ulisikia maneno ya Obama kuhusiana na demokrasi? Hapo hajaalikwa na serikali hii bali kaalikwa na US. Kwanza utasemaje dhifa ile ni yetu wakati mpaka getini wako Wamarekani?

Mkuu ...kunashinikizo kubwa magamba wamepewa....stay tuned!!!
 
Ulisikia maneno ya Obama kuhusiana na demokrasi? Hapo hajaalikwa na serikali hii bali kaalikwa na US. Kwanza utasemaje dhifa ile ni yetu wakati mpaka getini wako Wamarekani?

Vichaa nyie mmepewa likizo Mirembe? Dhifa aandae Kikwete mialiko atoe Obama hivi mzima wewe?????????
 
Back
Top Bottom