Dhifa ya Kitaifa na Obama: Mbowe ndani ya mwaliko Ikulu

ila kwa style hii ya mbowe, nadhani hana nia nzuri na babu mpora wake za watu.. kwani hawakuruhusiwa kubeba japo kwenye rambo akampelekea babu wa watu???
maskini kikongweeeeee
 
WanaJF!

Taarifa zilizo nifikia kutoka Ikulu hivi punde zinasema, mhe Mbowe ambae ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, amepata mwaliko Ikulu na hivi sasa ana jumuika na viongozi na watu mashuhuli kupata chakula cha jioni.

Mwaliko wa Mbowe Ikulu utaleta sura mpya hasa kwenye siasa zetu za ushindani, kwani kwa hivi sasa ushindani wa siasa umegeuka vita baina ya sisi kwa sisi, huku malengo ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi, ikiwemo kutanua zaidi demokrasi tukiyaweka kando.

Ni imani na matumaini yangu mwaliko wa Mbowe Ikulu utarejesha imani kwa baadhi ya mashabiki wa CHADEMA kwa serikali yao, ambayo imani hiyo ilianza kupotea kwa namna moja ama nyingine.

MBOWE asante kwa kuitikia mwaliko, hatimaye CHADEMA yapata mwakilishi kwenye ziara ya rais Obama.

Kwa udhaifu huu alioonesha Mbowe, ni wazi kwamba CHADEMA inapaswa kuchukua hatua. Lazima kitu kifanyike, endapo hakitafanyika kitu, basi tofauti ya CCM na CHADEMA haitakuwepo.
 
Mwacheni mwenyekiti wangu azoee zoee ikulu maana 2015 si mbali chadema wataingia rasmi...na nyie ccm tukiwaalika msisuse...lakini tutahakikisha ulinzi unaimarishwa ili msiingie na vibomu vyenu vya china.
 
Nimeelimishwa nikaelewa kuwa mbowe alichopata kwenye ile dhifa kitatusaidia sana kwenye kampeni zetu.
hata hivyo mbowe siyo mshamba wa ikulu yeye naye ni wa kule kule.
 
Musa alilelewa kabisa na Farao tangu katoto kachanga mpaka miaka 40, halafu akawa kinyume na Farao kwa ajili ya ukombozi wa watu wake. Msipanic, kuhudhuria kwa Mbowe kwenye vitu kama hivyo si dhambi na pia siasa si uadui. Japo ccm ya akina Mwigulu naona inakoleza Moto wa uadui. Mbowe hajahongwa na hahongeki... Lakin pia mbona Obama na Bush wamekutana hapa Tz na wote wana interest 1 japo vyama tofauti! sijasikia waMarekan wanalalamika
 
Tupe na ile ya Easter kukataa kukaa meza moja na mfalme na wafuasi wake, ilhali alijua kuwa kuna ndugu na jamaa zake wanaangamia!

Tupe na ya Easter basi ili tuweke equillibrium.

Mimi shida yangu nione namna ambavyo mnaweza ku-handle challenges, nimegundua kuwa CHADEMA ni weupe, kwa namna hii ya utetezi kwa Mbowe, hamna kitu.
 
Utetezi mwepesi kwenye hoja nzito haukubalic kabisa,Mbowe n Msaliti.
Angekuwa Zitto ungesikia afutwe chamani.
 
Last edited by a moderator:
Kwa udhaifu huu alioonesha Mbowe, ni wazi kwamba CHADEMA inapaswa kuchukua hatua. Lazima kitu kifanyike, endapo hakitafanyika kitu, basi tofauti ya CCM na CHADEMA haitakuwepo.
Kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom