haya jamani.... kwa wale
waliiolewa na wanahisi wanaume zao wana nyumba ndogo, hii inawahusu,
siguarantee kuwa mmeo atamuacha huyo (kama anae) ila itasaidia kufanya
nyumba yako isitetereke.
1.dhibiti matumizi ya simu.
kiukweli mawasiliano ndio msingi imara wa mahusiano yoyote. mawasiliano
yanapokuwa lege lege hata penzi hufifia na linaweza kufa kabisa. hapa
cha kufanya ni kumdhibiti baba watoto, akishaingia nyumbani hakuna
kuchati chati tena, hakikisha hawi karibu na simu yake. sio mwanaume
mpaka mnapanda kitandani yeye anachati tu, sa tano za usiku anachati na
nani? hapo unaibiwa. akifika home ni muda wake yeye na familia tu,
kismol house kama kipo kisubiri text msg kesho.
2. dhibiti mapato na matumizi.
small house siku zote yupo kipesa zaidi, kama mmeo anamwaga madolari ya
kutosha si ajabu small house akang'ang'ania hapo mpaka azeekee kwa mmeo.
katika kudhibiti mapato yenu mnaweza mkawa mnaandaa budgets zenu
pamoja, mnapanga kiasi gani mnaiingiza kwa mwezi na vipi
mtatumia.kudhibiti mapato itasaidia kupunguza fungu analokabidhiwa bi
mdogo na si ajabu akakimbia mwenyewe baada ya kuona hakuna mavuno tena.
kama mna mapato makubwa na matumizi mengi mnaweza kuajiri financial
controller kabisa. lol.
3.verify safari zake za kikazi.
wanaume wenye vismall houses wakipata safari za kikazi unaweza kuta siku
tatu kazini siku nne kwa bi mdogo wewe nyumbani unaambiwa safari ya
siku saba kumbe mtu kasharudi amejichimbia sehemu wanakula bata. hapa
unatakiwa kukaba, hakikisha siku ya safari unamsindikiza uwanja wa ndege
au stand ya mkoa na siku ya kurudi ukampokee, hakikisha anarudi na
risiti ya hotel na tickets za bus/ndege (tena hapa tafuta na file kabisa
la kuwekea hizo receipts, mwambie umeanza utaratibu wa kutunza
kumbukumbu. lol).
4.dhibiti ratiba zake za weekend.
uwe unatoka nae weekend, mnaweza kuwa mnaenda tembelea shamba, shopping
na familia, beach, etc. jitahidi kuvurugua ratiba zake za weekend haswa
zile ambazo una mashaka nazo... nyumba ndogo akikosa muda wa kuspend na
mmeo ndio dalili nzuri la penzi lao kuchuja huku lako likishine.
5.timiza wajibu wako kama mke na ibada za pamoja.
hapa kila mtu anajua wajibu wake na anayoyafanya kudumisha furaha ya
ndoa. usihesabu mazuri unayomfanyia mwenzio. we endelea kufanya tu. pia
jiwekeni karibu na mungu kwa kusali pamoja na kufanya yale mema kwa
pamoja.
mwageni mambinu jamani hata kama ni ya kialshabab! hizi zinafaa kwa
mnaokaa nyumba moja.