HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 2,691
- 2,303
Kazi ya mbunge siyo kutunga sheria tu pia siyo sheria zote hutokana na wabunge hasa ukizingatia wabunge wasomi ndiyo wameifikisha Tanzania hapa tulipo kwa kukosa uzalendo kwa nchi yao.
SHERIA NA VYANZO VYA SHERIA TANZANIA
MAANA YA SHERIA
Sheria ni kanuni zinazoongoza shughuli na mahusiano ya watu waishio katika jamii fulani. Sheria inaelezea haki na wajibu wa wanajamii hao, inaweka masharti juu ya mambo fulani, kuelezea makosa na adhabu iwapo makosa ama masharti yaliyotajwa na sheria yatakiukwa.
AINA ZA SHERIA
Kuna aina mbili za sheria Tanzania;-
1. Sheria za madai
2. Sheria za jinai
VYANZO VYA SHERIA TANZANIA
1. KATIBA
Katiba ni chanzo kikuu cha sheria, ni wajibu wa haki za wananchi kubainishwa katika katiba husika. Sheria zote za nchi hupata nguvu kutoka katika katiba ya nchi, hivyo basi kama kuna sheria ambayo haikubaliani na Katiba basi itakataliwa na Mahakama kuu kwani sheria zote ni lazima zifuate Katiba ya nchi.
2. SHERIA ZILIZOANDIKWA
Ni sheria ambazo zimeandikwa na kupitishwa na bunge au chombo kingine cha kutunga sheria. Sheria hizi huwa katika madaraja mawili; sheria kuu na sheria ndogo au sheria ya uwakilishi
1. SHERIA KUU
Kwa Tanzania, sheria hutungwa na bunge. Sheria ambazo hutungwa na bunge lenyewe huitwa sheria kuu; Mfano wa Sheria Kuu ni; Sheria ya Ardhi za Vijiji, 1999. Hata hivyo, bunge laweza kutunga sheria inayoruhusu chombo kingine au mtu kutunga sheria.
2. SHERIA NDOGO AU SHERIA YA UWAKILISHI
Sheria ndogo au sheria ya uwakilishi ni ile ambayo hutungwa na mtu, chombo au mamlaka yoyote ile ambayo imeruhusiwa kutunga sheria hiyo kwa mujibu wa Sheria kuu iliyopitishwa na Bunge. Mfano mmojawapo wa sheria ndogo ni ile inayotungwa na Halmashauri za Wilaya/Manispaa au Waziri.
3. SHERIA ZINAZOTOKANA NA MAAMUZI YA MAHAKAMA
Vyanzo vingine vikuu vya sheria ni maamuzi ya Mahakama ya rufaa au Mahakama kuu ambazo hufuatwa na mahakama za chini katika kuamua kesi za aina hiyo. Kwa hiyo, maamuzi yanayotolewa katika Mahakama hizi ni chanzo kingine cha sheria kwa mahakama za chini haswa katika kesi au mashauri yanayofanana. Hali kadhalika, Mahakama kuu haina budi kufuata maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kwani majaji wa mahakama hizi huitafsiri na kuzifafanua zaidi sheria.
4. SHERIA ZA KAWAIDA
Sheria ya Kawaida ni sheria ya kitamaduni ya Uingereza ambazo baadaye ziliingizwa katika mahakama. Sheria hizi zinafanana na sheria zetu za kimila kwa vile hata sheria hizi zimetokana na misingi iliyofuatwa na watu.
Asili ya sheria za kawaida katika mfumo wa kisheria wa Tanzania ni baada ya kutumiwa nchini India wakati wa utawala wa kikoloni wa mwingereza. Kwa mfano kanuni za adhabu za India, kanuni za madai za India, Sheria ya ushahidi ya India n.k. Mahakama za kikoloni za Tanganyika (kama Tanzania ilivyojulikana zama hizo) zilitumia kanuni hizi ambazo zilitungwa Uingereza katika utoaji haki kwenye mahakama zetu.
5. SHERIA ZA KIMATAIFA
Sheria za kimataifa huongoza mahusiano kati ya mataifa, zinaunda haki na majukumu ya mataifa kwa raia na inaweza pia kuunda haki za watu binafsi. Sheria za Kimataifa pia zinaweka kiada na viwango ambavyo vinatakiwa kuheshimiwa na kufuatwa na wananchi, mfano sheria ya kimataifa za mazingira, sheria za Kimataifa za bahari n.k
HATA HIVYO, kwa Tanzania sheria za kimataifa haziwezi kutumika nchini Tanzania bila utaratibu maalumu wa kuziingiza na kuzitumia ufanyike. Lazima zipitishwe na Bunge na zijumuishwe kwenye sheria za ndani ya nchi
6. SHERIA ZA MILA
Sheria za Mila zinaweza kutafsiriwa kama kanuni za kimila au jadi ambazo zinatumika, zinatambulika na kukubaliwa na jamii yoyote na kupata nguvu ya kisheria kupitia katika serikali na katiba ya nchi.
HATA HIVYO, Ili kutumiwa, ni lazima zithibitishwe na kuhalalishwa katika mahakama za kisheria pale ambapo kuna kesi zinazohitaji kutumika kwa kanuni hizo ili kuamuliwa