Derick Gaspar Mkandala Lufufu afariki dunia

Derick Gaspar Mkandala Lufufu afariki dunia

Jipe moyo mkuu utampata tu,the hard way is the only way
 
Wabongo tuache wivu dj afro mkali
Unaangalia movie kupoteza stress,movie iliyo tafsiliwa na dj Afro hata kama mbaya utaipenda tu,sio Wabongo mtafsiri anakaa kimya zaidi ya dakika 5,
Najiuliza c bora ningenunua original nijitafsrie mwenyewe
 
Mtu anaanzaje kizusha kifo cha mwenzake ambaye sio mwanasiasa na wala sio ccm?
Wako gado hawa majamaa...
upload_2017-5-30_16-20-6.jpeg
 
Lufufu kafariki nafikiri ni mwaka jana ila huu uzi ni wa mwaka juzi
 
Sancho huyo nadhani atakuwa ndo yule shombeshombe alikuwaga hadi pale VINGUNGUTI MTAKUJA CCM KWA PELAPELA kuanzia saa 1 mpk saa 5 usiku anatafsli picha za kihindi live hadi kuna mastaa kawapachika majina
kuna
TENGATENGA
MTAMBO WA KUREKEBISHA
MZEE WA NGUMI JIWE dah kitambo sana

halafu LUFUFU alikuwa anaishi VINGNGUTI TRAMPO kwa muda mrefu sana
Ndo huyohuyo shombeshombe
 
Tanzania kila sekta ina mtu wake aliyeitaendea haki, kwenye siasa tuna Mwalimu Nyerere, Mpira tuna Runyamila, Kwenye Movie tuna kanumba, Kwenye Jamii forums tuna Pascal Mayalla Kwenye Mziki tuna Professor Jay,

Kwa wale watu wa zamani kidogo mtakuwa mnamjua fika mtu mwenye kipaji cha kutafsiri filamu, huyu aliiweza sekta hii
Derick Gaspar Mukandara, ni mzaliwa wa bukoba, Tarafa kiziba, kata Lukurungo mtaa wa kyaya, alizaliwa mwaka 1955 na kuaga dunia mwaka 2015,
Kazi yake kabla ya kuanza kujihusisha na kutafsiri movie ilikuwa ni askari Jeshi ambaye aliamua kuachana nayo na kuanza rasmi shughuli za kutafta movie mbali mbali,
Alianza na studio yake iitwayo chui video Libra ipatikanayo bukoba mjini mtaa wa migeyo, na baadae kuhamia jijini dar es salaam mbagala kuu,

Lufufu wakati anaanza kazi za kutafsir nakumbuka mbagala kwa Mangaya jumbani kwa Limonga Justin wa Limonga (R.I.P), huyu Limonga ndiye aliyemu hosti enzi hizo nikiwa darasa la 5 sikumbuki vizuri. Asiee kila kazi ina hatua zake alianza kututafsria ukumbukini hadi pale Limonga alipoona dili akawampa chumba ambacho alifanya studio. Bahati nzuri Lufufu alikuwa mtu wa watu akipita mtaani enzi zile na kofia yake ya Cowboy tulimpamba kwa nyimbo..Lufufu Lufufu Lufufu...nina mengi sana acha niishie hapa kwanza


Sauti yake ya pekee iliyosikika kutoka vibanda umiza vya kuchek filamu ilivuta hisia za watu na kutaman kulipia wakaangalie,

Pamoja na kutafsiri aliongeza mbwembwe na vionjo kadhaa hata maneno ya kuchekesha ambayo mengi yalikuwa ya kihaya na mengine ya mtaani,

Maneno maarufu
1. Kanyampasiila, akimaanisha kwenye kona
2. Kukotora akimaanisha kukimbia au kutoka mbio,
3. Byataba akimaanisha sehem za siri za mwanamke
4. Kijiji akimaanisha sehem za siri za mwanaume
5. Kyembadoka, kushangaa
6.Mwani akimaanisha risasi
7.njugu pia risasi,
8. Viazi akimaanisha mabomu
9. Katebatebe kusimamia mguu mmoja

Yapo mengi sana ambayo yalivutia sana,

Kipaji chake kimeweza kuonesha njia kwa vijana wengi na kuichukulia kazi ya kutafsiri movie kama sehem ya kujipatia kipato,

Anastahili heshima alale maala pema peponi

FB_IMG_1535193176089.jpg
FB_IMG_1535193173667.jpg


Kipande cha filamu Chenye sauti yake

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom