Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Nimepokea habari hizi kutoka kwa msanii wa kuitwa Nash Mc, ameandika kwenye ukurasa wake wa FaceBook, sina shaka na habari yake kama na yeye hajasikia hewani hewani.
=========
Chanzo: MKALIMANI MAARUFU WA FILAMU NCHINI 'RUFUFU' AFARIKI DUNIA. ~ g sengo
Kapteni Derick Mukandala Lufufu, Nimekuwa nikikuzingumzia mara nyingi sana kwa jinsi navyokubali umahiri wako pale unaposimulia na kutafsiri kwa Kiswahili picha za Ulaya na Marekani bila kusahau Wahindi,lakini muda si mrefu nimepokea taarifa za kifo chako na nimebaki sina la kufanya zaidi ya kusema,KAZI YAKE MOLA HAINA MAKOSA. Sina mengi ya kuongea kwani nimefanya watu waijue hata sura yako kupitia mitandao ya kijamii huo ni mchango wangu kwako.
M.A.P LUFUFU.
=========
Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkandala Rufufu aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa kutafsiri filamu za lugha mbalimbali kiingereza, kihindi, kichina, na hata wakati mwingine kifilipino yote aliyafanya kwenda katika lugha mama ya kiswahili, tutamisi zile mbwembwe, fix, uwongo uwongo wenye maana, mikogo ya sauti al-muradi kunogesha sikio la mtazamaji.
Rufufu amefariki dunia jana usiku wakati akitoka nyumbani kwake kuelekea harusini ambapo kwa mujibu wa wasimuliaji wanasema kuwa presha ilimpanda ghafla akaanguka na watu waliokuwa karibu naye walimkimbiza hospitalini na kabla hajapata matibabu akawa tayari amefariki dunia.
Dah tulifaidi sana tafsiri za filamu ulizokuwa unafanya hasa tuwapo safarini Tz ndani ndani, (wilayani, vijijini, mkoa kwa mkoa).
Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Rufufu mahala pema peponi.
Amin!
Chanzo: MKALIMANI MAARUFU WA FILAMU NCHINI 'RUFUFU' AFARIKI DUNIA. ~ g sengo