Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

I think this story is not clear!

1.Alitaka gonga polisi wakakwepa
2.Akashuka na kisu akajeruhi watatu
3.Akataka kunyang'anya bunduki Kwa askari
4.Akapigwa risasi
5.Akafa
Mmmmmh
1.Akateswa
2.Akafa
3.Akashuka kuzimu
4.Siku ya Tatu akafufuka
5Akapaa Mbinguni
6.Ameketi mkono wa kuume wa Mungu baba kutoka huko atakuja hukumu walio hai na wafu.
Jeshi la polisi nchini linatakiwa kufumuliwa loooote!!! Na kama Samia haamini siku yatakapomkuta yeye mwenyewe binafsi asitulilie. Polisi wetu hawafai aisse. Kuqnzia sheria, muundo na baadhi ya maafisa hasa wa vyeo vya juu hawafai kabisa kuonekana katika sura ya jeshi la polisi makini
 
Kwasasa serikali haiamini kwamba siron na jeshi lake ni Vimeo Ila siku wakizingua kwenu (gvt) msiombe tuwasaidie kulia.
 
Nawajua polisiccm unadhani kwanini HAMZA Watanzania wengi walimuona ni shujaa? Unadhani kwanini polisiccm wanachukiwa sana na Watanzania wengi?
Usilete uchama hap... mbon hawaandamani kupinga tozo na bei za korosho hafifu?
 
Jeshi la polisi nchini linatakiwa kufumuliwa loooote!!! Na kama Samia haamini siku yatakapomkuta yeye mwenyewe binafsi asitulilie. Polisi wetu hawafai aisse. Kuqnzia sheria, muundo na baadhi ya maafisa hasa wa vyeo vya juu hawafai kabisa kuonekana katika sura ya jeshi la polisi makini
naunga mkono hoja mkuu Tena inahitajika reformation ya kufa mtu Hawa wanatia kinyaa aisee daaa!
 
Uchunguzi utafanyika na yatajulikana. Lakini kama kweli alitaka kuchukua silaha kwa nguvu kwa polisi anastahili alichopata.

Kama alisimamishwa akakaidi anastahili pia.

Tanzania tunakua na tabia ya ajabu ya kuona sisi tuna haki kuliko wengine. Polisi wangegongwa wafe mngeshabikia. Lakini hamtaki kuona kwamba raia pia wana makosa.

Sikatai kuwa polisi wanazingua lakini ni ukweli kwamba na sisi raia tuna makubwa ya ajabu tunayowafanyia.

Hamza alichukua silaha kwa nguvu kwa polisi yakatokea yaliyotokea.

RIP DAVOOO. ILA KAMA ULIZINGUA JUA UMEACHA MAJONZI KWA WANAO
Usijifanye unawajua watanzania wakati hata mikoa mitano ya Tanzania hujafikisha...

Hyo habari nimeiona ITV ,Ni Kama ina ukakasi flani Mara waseme Ni jambazi Mara Ni dereva..
Na mpk dereva anashuka kwenye Gari alikuwa tayari ameacha njia imeenda kusimamia porini

Hatuwezi jua Ni kwa namna gani wale Askari waliisimamisha Gari mpk lipotee njia...

Majeruhi wenyewe hawajahojiwa na mwandishi Wala kuoneshwa sura km tunavyoona kwenye matukio mengine.

Tazama marudio ya taarifa halafu uje hapa useme police wanaonewa au la
 
Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinki anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
Askari watatu mnamshindwa kumdhibiti mtu mmoja asiye na bunduki tena dereva na si jambazi mnaua
 
Acha kuishi na umbea kichwani mwako ndugu, leta vielelezo hapa vya kuporwa Mali za hamza.

Umesikia tu umbea pahali huna hata muda wa kutafakari na kujiuliza unabeba kama ulivyo, hii tabia ukiiendekeza itakuja kukupa matatizo ndugu
Kwahiyo mkuu wewe unaamin taarifa za Polisccm?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hata kamanda wa polisi kakangamia sana....roho ilikubali ila mwili ulikataa kabisa kutamka kilichotokea. Polisi hawaaminiki aisee. Kuna motive gani dereva afanye unyang'anyi wa silaha?
Imagine dereva atoke na kisu kwenda kuwanyanganya Police silaha tena za moto
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nawajua polisiccm unadhani kwanini HAMZA Watanzania wengi walimuona ni shujaa? Unadhani kwanini polisiccm wanachukiwa sana na Watanzania wengi?
Ww mbwiga unakera sana kila kitu unaongea mafi mafi yako u ccm na chandema we bwege.
Hilo tukio linahusiana nini na vyama?
 
Inafikirisha kwakweli,ukiangalia taarifa hata daktari aliyepokea majeruhi na mfu anaongea kwa wasiwasi maana anajua anaongopa.
Kamanda ndo kabisaa unaona tu huyu mwongo huyu.
 
ALONE YO CANT FIGHT WIUH WORLD...
haiingii akilini kuanzia mwanzo wa tukio mpaka mwisho kama wewe una utimamu wa 100% basi utajua hapa hakuna ukweli wowote ni muvi imetengenezwa ili raia aonekane mwenye makosa heti jamaa paap ametaka kuwagonga akawakosa... mara paap akatoka na kitu.. kama kisu.... mara paap akataka kumunyang'anya afwande silaha hahaha wajomba sio kila anaesoma hayo maandishi ni TAHIRA kama walioamini huu ujinga anyway pongezi sana kwenu, (IN MRISHO MPOTO VOICE) LILIKUWA LIKIPAMBANA POLISI TUKARISHINDA
 
Back
Top Bottom