Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinki anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
HUO NI UONGO MKUBWA KABISA. NCHI HII HAINA CHOMBO ZAIDI YA POLISI KWA UPELELEZI TUNAKOSEA SANA TUNAPOLIAMINI JESHI L polisi kutoa taarifa..HATUNA LA KUSEMA MUNGU ATAHUKUMU HAKI KESHO . TZ IMETAMALAKI DHULUMA TU

KWA NINI NASEMA NI UONGO KWA DEREVA WA MALOLI KAMA MIMI NI IMPOSSSIBLE KILICHOELEZWA

UKWELI UNAWEZA KUWA HIVI

" KWENYE KIZUIZI ITAKUWA ALIRUHUSIWA KUTOKEA MBALI APITE, GHAFLA POLISI AKALAZIMISHA KUSIMAMA NA KUAMUA KUMKWEPA NA KUINGIZA LORI POLINI. BAADA YA HAPO AKAPATA HASIRA KWENDA KUPAMBANA NA POLISI UENDA HICHO KISU AMEBAMBIKIWA NDIPO POLISI WAKAAMUA KUFANYA MAUAJI"

MIMI NAWAJUA SANA HAWA WAKIWA KWENYE KIZUIO NI HOVYO...KABISA.
SITORUHUSU MWANANGU AFANYE KAZI YA UPOLISI
 
Ila Dah... mafunzo na mazoezi yanaitajika zaidi...

Mtu mwenye kisu na kuja kujeruhi askari watatu na pia katika askari hao ana silahaa.
Na mbali zaidi wanatumia nguvu kubwa kuchapa raia risasi lihali raia ana kisu tu..!

Kweli bado kuna changa moto katika kukabiliana na Magaidi hasa katika kitengo cha police

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Kisu nacho ni silaha. Kwa wenzetu wakikuambia weka chini ukagoma ni risasi zinakuhusu. Kwanza si moja. Kwa nn ukaidi agizo?
 
Kama kweli alitaka kuwagonga. Basi risasi ilikuwa halali yake bila hata kutoa kisu. Sema watu wa haki za binadamu watasema askari wangemshika tu..Ila am sure mtu akitaka kukugonga ukamshoot Mungu anakuelewa kabisa
 
Ila Dah... mafunzo na mazoezi yanaitajika zaidi...

Mtu mwenye kisu na kuja kujeruhi askari watatu na pia katika askari hao ana silahaa.
Na mbali zaidi wanatumia nguvu kubwa kuchapa raia risasi lihali raia ana kisu tu..!

Kweli bado kuna changa moto katika kukabiliana na Magaidi hasa katika kitengo cha police

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

usikazi fuvu.kuanzia leo jua hivi.

ni wakati gani utachapwa risasi.

ukiwa na silaha nyingine ta moto na una kila dalili ya kudhuru watu au kujidhuru.

ukiwa na silaha nyingine ambayo inaweza kudhuru kama panga upinde na unadalili zote za kudhuru au kujidhuru.

ukiwa umeyaweka hatarini maisha ya mtu mwingine either umemkaba au umemkalia na anaelekea kufa.

ukiwa umeshika kilipuzi na una kila dalili ya kukiweka kwenye sehemu kama mafuta au gas.

NOTE:hakikisha katika harakati zako za kila siku huwapi sababu polisi ya kukupiga risai,hawata kupunguza kasi kwa kurengachini ya goti ila watakuua kabisa ukapumzike.
 
Hii story imeletwa kwa ufupi sana humu, ila ukweli ni kuna askari watatu wamejeruhiwa mmoja kavunja bega, inaonesha kulikuwa na mapambano alafu pia dereva mwenyewe wa ili gari ndo akieendesha kwa muda huo kwaiyo inaonesha hata uyo dereva labda alitekwa au vipi, na kiukweli kabisa walio karibu na eneo la tukio walisikio mirindimo ya risasi kwa mda fulani, Mimi nipo Lindi hapa musilaumu sana hao Police bila kujua magumu wanayopitia, kumbukeni huku ndo njia ya kwenda Msumbiji, alafu uko Msumbiji kumechafuka sio kitoto, tuwaheshimu tu makamanda tusipende kulaumu kila ktu
 
Hii story imeletwa kwa ufupi sana humu, ila ukweli ni kuna askari watatu wamejeruhiwa mmoja kavunja bega, inaonesha kulikuwa na mapambano alafu pia dereva mwenyewe wa ili gari sio akieendesha kwa muda huo kwaiyo inaonesha hata uyo dereva labda alitekwa au vipi, na kiukweli kabisa walio karibu na eneo la tukio walisikio mirindimo ya risasi kwa mda fulani, Mimi nipo Lindi hapa musilaumu sana hao Police bila kujua magumu wanayopitia, kumbukeni huku ndo njia ya kwenda Msumbiji, alafu uko Msumbiji kumechafuka sio kitoto, tuwaheshimu tu makamanda tusipende kulaumu kila ktu
 
Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinki anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
Huyo akuwa dereva ila ni alshababu take from my source
 
Ila Dah... mafunzo na mazoezi yanaitajika zaidi...

Mtu mwenye kisu na kuja kujeruhi askari watatu na pia katika askari hao ana silahaa.
Na mbali zaidi wanatumia nguvu kubwa kuchapa raia risasi lihali raia ana kisu tu..!

Kweli bado kuna changa moto katika kukabiliana na Magaidi hasa katika kitengo cha police

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Police wetu Wana utu sana, na ukiona hivyo walimvumilia hadi mwisho
 
Jina lake sasa na ugaidi havipishani
Kama hukijuwi kizuwizi cha lindi basi ongea kwakuwa huwo mdomo ni mali yako ila kiufupi huyo dereva atakuwa ni giadi na itakuja thibitishwa baadae... Kizuwizi cha Lindi nimoja ya vizuwizi madereva na maharamia wanakichukia sana.
 
Ni ngumu sana kuwaamini hawa akina Kingai. Taarifa yoyote inayotolewa na Jeshi la Polisi la Tanzania, kuweza kuaminika, labda awepo mtu mwingine huru aliyeshuhudia.

Kwa hisia zangu, hii habari kwa 80% itakuwa ya uwongo, imetengenezwa na Polisi. Kama alikuwa na fedha, itakuwa ndiyo sababu ya kifo chake.

Ukiwa na hela, ujitahidi polisi wasijue.
 
Back
Top Bottom