Demokrasia ni hitaji la Wanasiasa tu. Wananchi Hitaji lao kubwa ni Maendeleo

Wanasiasa wa upinzani wasitutanie. Sisi hatuhitaji katiba. Lakini na wanasiasa wa chama tawala wasitutanie. Sisi tunadai umeme na maji, pamoja na kupungua kwa bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kula na yale ya kuendeshea mitambo. Sasa katika hao wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala, anayejua anadaiwa hivyo vitu ajiandae kuwajibishwa

Sasa unapinga nini? Huko kudai umeme, na maji ndio de,okrasia yenyewe. Yaani demokrasia inakupa nafasi ya kudai haki yako au hitaji lako toka kwa serikali au kiongozi. Bila demokrasia hiyo nafasi ya kudai huna! Kwani nyie wenzetu akili za kufikiri mmeweka kwenye chumba gani cha giza pale Lumumba?
 
Itamsaidia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu, Hospitali, Miundo Mbinu, Umeme na Maji?

Yaani kuwa mwanasiasa wa Chama cha Upinzani atakuwa huru kufanya na kusema atakayo then mwananchi anakosa huduma muhimu ndo iwe issue ya kitaifa?

Ni Bora sana kwa Nchi kama Tanzania apatikane Rais Dikteta mwenye maono ya Kimaendeleo nchi iende mchaka mchaka kuliko kuwa na Rais mwanademokrasia na kuruhusu uhuni ufanyike.

Libya walitaka Demokrasia. Leo wanasemaje? Mimi nadhani nchi zetu za kiafrika hazihitaji Demokrasia. Zinahitaji maendeleo ya nguvu na nguvu ya maendeleo kwa pamoja.

Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.

Nchi zetu hizi ukichEka na Nyani Utavuna Mabua.
Kama wananchi hahitaji demokrasia anahitaji maendeleo, basi hatukuwa na sababu ya kuomba uhuru.
 
Maendeleo ni tawi la demokrasia!
Wakati mwingine ukiwaza Sana unaweza kumkufuru Mungu. Watu wengine kawapa miili mikuuubwa akili kiduchu. Kama demokrasia si hitaji la wananchi Kwa nini wanakwenda kupiga Kura? Nani Yuko tayari kupiga Kura kumchagua Johnthebaptist halafu Kura yake akaona imehesabiwa Kwa Bila bila?
 
Itamsaidia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu, Hospitali, Miundo Mbinu, Umeme na Maji?

Umelitazamia swala hilo katika upande huo tuu,
ambao nimchache kuliko upande wapili ambao unamengi yafaida kwa wananchi na kwa maendeleo ya nchi.
 
Itamsaidia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu, Hospitali, Miundo Mbinu, Umeme na Maji?

Yaani kuwa mwanasiasa wa Chama cha Upinzani atakuwa huru kufanya na kusema atakayo then mwananchi anakosa huduma muhimu ndo iwe issue ya kitaifa?

Ni Bora sana kwa Nchi kama Tanzania apatikane Rais Dikteta mwenye maono ya Kimaendeleo nchi iende mchaka mchaka kuliko kuwa na Rais mwanademokrasia na kuruhusu uhuni ufanyike.

Libya walitaka Demokrasia. Leo wanasemaje? Mimi nadhani nchi zetu za kiafrika hazihitaji Demokrasia. Zinahitaji maendeleo ya nguvu na nguvu ya maendeleo kwa pamoja.

Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.

Nchi zetu hizi ukichEka na Nyani Utavuna Mabua.
Umechanganya mambo hata demokrasia hairuhusu kumchora Rais au mtu yeyeto kwa nia ya kumdhalilisha.
 
Sasa kutukanwa kwa raisi au kuchorwa kwa raisi kunausiana nn na maendeleo kama kiongozi umeomba uongoze watu ukatoa ahadi zako umo umo kuna watu hawajakuunga mkono lkn ukishinda unaongoza wote kwaiyo lazma kuwepo na upinzan wa maneno kukosolewa na mengine wanaovuka mipaka sheria zipo na yani nchi ishindwe kuendelea kwa sababu ya kikundi au watu fulan kumtukana raisi au kumkosoa
 
Kazi ya Raisi ni kupambana na umaskini na kero za wananchi. Sio ufisadi wala mambo ya kupeana vyeo vya hisani!
 
Sasa kutukanwa kwa raisi au kuchorwa kwa raisi kunausiana nn na maendeleo kama kiongozi umeomba uongoze watu ukatoa ahadi zako umo umo kuna watu hawajakuunga mkono lkn ukishinda unaongoza wote kwaiyo lazma kuwepo na upinzan wa maneno kukosolewa na mengine wanaovuka mipaka sheria zipo na yani nchi ishindwe kuendelea kwa sababu ya kikundi au watu fulan kumtukana raisi au kumkosoa
Ukiwa na uwezo Mdogo wa kufikiri ndo utapambana na watu kwa kiongozi civilized ashughuliki na kelele za chura kwenye maji
 
Nlidhani ungekuja na hoja. But pia Demokrasia ni kutoa uhuru kwa kila mtu atoe ya moyoni mwake. Wewe ukiona aliyetoa wazo hili ni taahira na hapo huna madaraka ukiwa na madaraka si utasema anayeamini kinyume nawe auawe? Nlikuwa nataka kupima uwezo wa uelewa wa demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo. Nimegundua hata wanaozungumzia demokrasia au uhuru wa mawazo hawataki wenzao watoe mawazo yao. 😁😁😁😁

Wazazi tuna changamoto sana, yani ukiulizwa una watoto wangapi na taahira kama huyu utamuhesabu?

Wewe umeandika takataka tu, miaka 60 ya uhuru watanzania ni maskini zaidi ya walivyokuwa wakati nchi inapata uhuru, hayo maendeleo yako wapi kama hadi kujenga tu choo cha shule hadi hao hao wakoloni wawasaidie.

Maendeleo ya maana hamna pamoja na kwamba hakuna rais aliye tukanwa wala anayetukanwa kila siku ni visingizio kibao ndio vinaibuliwa. Zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wanaishi chini ya dola moja ya Marekani kwa siku. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom