Demokrasia ni hitaji la Wanasiasa tu. Wananchi Hitaji lao kubwa ni Maendeleo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,347
11,447
Itamsaidia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu, Hospitali, Miundo Mbinu, Umeme na Maji?

Yaani kuwa mwanasiasa wa Chama cha Upinzani atakuwa huru kufanya na kusema atakayo then mwananchi anakosa huduma muhimu ndo iwe issue ya kitaifa?

Ni Bora sana kwa Nchi kama Tanzania apatikane Rais Dikteta mwenye maono ya Kimaendeleo nchi iende mchaka mchaka kuliko kuwa na Rais mwanademokrasia na kuruhusu uhuni ufanyike.

Libya walitaka Demokrasia. Leo wanasemaje? Mimi nadhani nchi zetu za kiafrika hazihitaji Demokrasia. Zinahitaji maendeleo ya nguvu na nguvu ya maendeleo kwa pamoja.

Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.

Nchi zetu hizi ukichEka na Nyani Utavuna Mabua.
 
Uelewa wako ni mdogo sana na hapo hapo unajikanganya.Hitler alileta maendeleo makubwa Ujerumani lakin mwisho wa U dikteta wake aliafanya nini?

Gadafi uliemtaja alitoa mpaka pesa ya kuolea,jiulize kwa nini wananchi wake waje wamuue?

Ukimchora Rais na kama kwenye sheria inakatazwa unashtakiwa lakini sio kuwekwa kwenye kiroba.
 
wanasiasa wapumbavu ndo wanaifanya demokrasia ionekane haifai, ikiwa dini pia imeletwa kwetu kama demokrasia bt tunaitekeleza kuliko hata waloileta why tusifanye hivo pia kwenye demokrasia?

mi nadhani tatizo kubwa lipo kwenye katiba zetu ambazo haziendani na utawala wa kidemokrasia hivo tukirekebisha katiba zikaendana na demokrasia hizi reason za kijinga tunazozijenga wala hazitakuwepo.
 
Wewe umeandika takataka tu, miaka 60 ya uhuru watanzania ni maskini zaidi ya walivyokuwa wakati nchi inapata uhuru, hayo maendeleo yako wapi kama hadi kujenga tu choo cha shule hadi hao hao wakoloni wawasaidie.

Maendeleo ya maana hamna pamoja na kwamba hakuna rais aliye tukanwa wala anayetukanwa kila siku ni visingizio kibao ndio vinaibuliwa. Zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wanaishi chini ya dola moja ya Marekani kwa siku. Bure kabisa.
 
1: Kasome ni nini maana ya demokrasia?

2: Angalia nini ndani ya demokrasia kinapinga maendeleo ya watu husika?

3: Matumizi mabaya ya watu kwa kitu fulani chenye haki si sababu ya kukiondoa au kukizuia bali kuweka utaratibu unaokubalika na jamii husika jinsi ya utekelezaji wake.
 
Kwakuwa nchi nyingi za kiafrika hazina demokrasia zilitakiwa ziwe na maendeleo. Lakini ni kinyume chake kabisa. Mmeshindwa kutawala kwa kutumia akili na maarifa, mnataka kuhalalisha kutawala kwa mabavu kwa kisingizio cha kuleta maendeleo.

Maendeleo gani mtaleta nyie watu wenye mitazamo ya kimaskini?
 
Itamfadia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu,Hospitali,Miundo Mbinu,Umeme na Maji?

Yaani kuwa mwanasiasa wa Chama cha Upinzani atakuwa huru kufanya na kusema atakayo then mwananchi anakosa huduma muhimu ndo iwe issue ya kitaifa?

Ni Bora sana kwa Nchi kama Tanzania apatikane Rais Dikteta mwenye maono ya Kimaendeleo nchi iende mchaka mchaka kuliko kuwa na Rais mwanademokrasia na kuruhusu uhuni ufanyike.

Libya walitaka Demokrasia. Leo wanasemaje? Mimi nadhani nchi zetu za kiafrika hazihitaji Demokrasia. Zinahitaji maendeleo ya nguvu na nguvu ya maendeleo kwa pamoja.

Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.

Nchi zetu hizi ukichEka na Nyani Utavuna Mabua.
Sasa mbona vimewashinda vyote Maendeleo mashaka,demokrasia mashaka,,Familia zenu mambo safiiiiiii
 
Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.
Ndugu yangu,
Rais wa kupandikizwa hawezi kuwa mzalendo. Anatekeleza ayatakayo 'kwao' na kwa 'kundi' lake. Tumeshayaona hayo hapa sasa yanatosha.
Democracy NDIO pekee yaweza kuleta matakwa na mahitaji ya wananchi na hivyo kujenga msingi imara ya HAKI na AMANI ndani ya taifa.
Wananchi waachwe wapige kura na ndio wachague viongozi ili hatimae pia kuwezesha kupata mfumo thabiti wa uongozi unaowajibika. Maendeleo ya kweli yanatakiwa kulenga vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi kwa muda mfupi na muda mrefu. AMEN
 
Demokrasia ni hitaji la Wanasiasa tu. Wananchi Hitaji lao kubwa ni Maendeleo

Wanasiasa wa upinzani wasitutanie. Sisi hatuhitaji katiba. Lakini na wanasiasa wa chama tawala wasitutanie. Sisi tunadai umeme na maji, pamoja na kupungua kwa bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kula na yale ya kuendeshea mitambo. Sasa katika hao wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala, anayejua anadaiwa hivyo vitu ajiandae kuwajibishwa
 
Unawawajibisha vipi ilihali hawaitaji kupigiwa kura yako kukakaa madarakani?

Hivi huwa mnaelewa mnayoyaandika?
 
Itamsaidia nini mwananchi kuwa na Uhuru wa kumchora Rais na Kumtukana atakavyo na huku hakuna Huduma za muhimu kama Elimu, Hospitali, Miundo Mbinu, Umeme na Maji?

Yaani kuwa mwanasiasa wa Chama cha Upinzani atakuwa huru kufanya na kusema atakayo then mwananchi anakosa huduma muhimu ndo iwe issue ya kitaifa?

Ni Bora sana kwa Nchi kama Tanzania apatikane Rais Dikteta mwenye maono ya Kimaendeleo nchi iende mchaka mchaka kuliko kuwa na Rais mwanademokrasia na kuruhusu uhuni ufanyike.

Libya walitaka Demokrasia. Leo wanasemaje? Mimi nadhani nchi zetu za kiafrika hazihitaji Demokrasia. Zinahitaji maendeleo ya nguvu na nguvu ya maendeleo kwa pamoja.

Ili mradi Rais awe Mzalendo na mwenye malengo.ambaye atasema tunaelekea mbele na wote wakatakiwa kufuata kwenda mbele. Akisema kulia geuka wote tunageuka katika harakati za maendeleo.

Nchi zetu hizi ukichEka na Nyani Utavuna Mabua.
Kwani demokrasia siyo maendeleo? Baba wa Taifa alituasa kwamba msingi wa maendeleo ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Huwezi kuitenga demokrasia kwenye vyote hivyo.
 
Back
Top Bottom