Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, Septemba 15, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
JamiiForums na Haki Mawasiliano wameshirikiana kuandaa mjadala katika kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani.

Kauli Mbiu katika mjadala huu ni “Kuwezesha Kizazi Kijacho”, ambapo Mada husika ni “Demokrasia ya Kidijitali kama Kichocheo cha Utawala Bora”

Mjadala unafanyika kwenye Ukumbi ndani ya Seashells Hotel, Millenium Towers Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo
Nilianza kuwa raia ‘active’ Mwaka 1992, ni wakati huo ndipo nilipoanza kuisoma vizuri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni rahisi haki yako kupokwa ikiwa hauijui Katiba, nakushauri utakuwa raia mzuri ikiwa utaijua Katiba na itakufanya ujue haki zako

Maxence.PNG

Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo akizungumza na washiriki

Dkt. Muhidin Shangwe, Mhadhiri - UDSM
Uongozi wa Kisiasa huwa Una Ngazi (Hierrachy) kwamba Kiongozi yuko juu na Mananchi chini lakini uwepo wa majukwaa ya dijitali unasawazisha uwanja huu na kila Mtu sasa anaweza kumhoji yeyote, kuuliza swali lolote bila kujali Umri, Cheo wala Hadhi

Rodrick.jpg

Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Muhidin Shangwe (kushoto) akichangia mada ukumbini. Kushoto kwake ni Dkt. Rodrick Henry.

Dkt. Rodrick Henry, Mhadhiri - UDSM
Demokrasia ya Dijitali inaondoa ile dhana ya kusubiri hadi uchaguzi ujao yaani miaka mitano kwa Tanzania ili kumuwajibisha Kiongozi wa Kisiasa

Teknolojia ya dijitali inachochea dhana ya Mwananchi kuwa sehemu ya Utawala wa kila siku

Uongozi wa Kisiasa huwa Una Ngazi (Hierrachy) kwamba Kiongozi yuko juu na Mananchi chini lakini uwepo wa majukwaa ya dijitali unasawazisha uwanja huu na kila Mtu sasa anaweza kumhoji yeyote, kuuliza swali lolote bila kujali Umri, Cheo wala Hadhi

Demokrasia ya Dijitali bado ina changamoto kutokana na “Digital Divide”. Kuna Watu hususan wa Vijijini bado hawana namna ya kufikia au kumudu huduma za dijitali

Ni wajibu wetu wenye uwezo wa kushiriki kwenye majukwaa ya kidijitali kuhakikisha tunawajumuisha na wenzetu wasioweza ili iwe Demokrasia kweli

Stephen Aloys, Mkurugenzi Mtendaji - Haki Mawasiliano
Kuwa na Siku maalum ya Demokrasia Duniani ni muhimu sana, kila Mwaka imekuwa na ujumbe tofauti, Haki Elimu na Jamii Forums tumeamua kutumia mjadala wa Majukwaa ya Kidigitali kutoa elimu na kukumbusha jamii juu ya umuhimu wa kutumia Digitali katika kuimarisha Demokrasia

Tunatakiwa kuwa na Sheria ambazo hazibani uhuru wa kujieleza, tunataka Sheria na Kanuni ambazo ni rafiki zinazoweza kumfanya Binadamu aweze kujieleza, kiasili Binadamu anatabia ya kutaka kujua zaidi na kujieleza zaidi

Hali ya Demokrasia kwa sasa Nchini, kuna Sheria nyingi zinazotoa uhuru na zipo zinazobana uhuru wa kujieleza, tunachoshauri ni kuwa kusiwe na mipaka inayoumiza watu kutoa na kupata taarifa

Dunia ya Kidigitali ilivyo kwa sasa unaweza kupata taarifa ambayo haujaiomba na ukapokea taarifa ambayo hujaombwa

Taarifa ni Maendeleo, uwe kiongozi au raia wa kawaida, bila kuwa na taarifa huwezi kufanya kitu cha maendeleo

Pamoja na kuwa kwa sasa kuna uhuru wa kutoa maoni lakini bado kuna Sheria kadhaa ambazo zinamisha uhuru wa kutoa maoni na hivyo kuminya Demokrasia

Abdul-Aziz Ally Carter, Mwanafunzi - UDSM
Mifumo iliyopo katika Vyuo Vikuu inakatisha tamaa kwenye suala la Demokrasia, kuna vifungu vya Sheria vinazuia Wanafunzi kushiriki moja kwa moja kuleta Demokrasia Nchini tofauti na baadhi ya vyuo vya Nchi nyingine ambapo Wanafunzi wanatumika kama tabaka la kushawishi mabadiliko katika Taifa

Hali ni tofauti, mifumo iliyopo Tanzania inatengeneza Wanafunzi watiifu ambao hawana uwezo wa kuhoji, kupigania jamii, mwisho wake inatengeneza ‘Chawa’

Carter.PNG

Abdul-Aziz Carter, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada

Kuna Sheria ya Vyuo Vikuu (University Act 346) inakataza Wanafunzi kujihusisha na Siasa awapo chuo au katika mazingira ya chuo, pia kuna Sheria ndogondogo nazo zinasimamia msimamo huohuo

Kuna mambo tunatamani kuyazungumza lakini ukizungumza unachukuliwa hatua kwa kuonekana kukiuka Sheria, unaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kufukuzwa chuo

Kuna kipindi Wanafunzi walicheleweshewa fedha za ada za mkopo kutoka Bodi ya Mikopo, tukakubaliana tulipe ada kisha Bodi itarejesha hizo fedha Julai 2023, lakini hii ni Septemba hizo fedha hatujapata licha ya kufuatilia kwenye Mamlaka

Jopo letu.PNG

Wanajopo walioshiriki katika mazungumzo katika Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani wakisikiliza michango ya wahudhuriaji. Kutoka kushoto ni Bi. Dorice Mgetta, Dkt. Muhidin Shangwe (UDSM) na Dkt. Rodrick Henry (UDSM).

Kuna Mwanafunzi akataka yafanyike maandamano kwa kuwa ni haki ya Kidemokrasia lakini akaitwa na Kiongozi wa Wanafunzi (Dean of Student), kinachoendelea hapo ni vitisho ili kutoendelea na alichokipanga, hivyo tunatengenezewa hofu na Demokrasia inaminywa hapo

Athari ya mifumo ya kutokuwa na Demokrasia imara inawafanya wanapohitimu masomo wanaingia uraia na kutengeneza Taifa lisilokuwa na nguvu ya kuhoji na kutambua haki zao za msingi

Shukurieli Laizer, Mwanafunzi - UDSM
Kwenye jaii kuna watu ambao wanafahamu kuhusu Demokrasia lakini wanakaa kimya, wapo wanaofahamu na hawataki kushughulia, wapo ambao wanafahamu na wajishughulisha, hao ndio ambao jamii inawaita ‘active citizen’

Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji -JamiiForums
Kuna watu wanasema Watanzania wanakurupuka au wanatumia vibaya Mtandao wa Intaneti, kama ni Asilimia basi inawezekana ni 3% ya wanatumia Mtandao vibaya, wengine 97% wanatumia vizuri

Kuna watu wanadhani mtandao unamfanya mtu abadilike, ni yuleyule ila amepata nafasi ya kujieleza katika njia mbadala. Hivyo, Wanachokiandika ndicho wanachokipenda na ndicho kinachotokea mtaani, mtandao ni uwakilishi wa uhalisia wa kinachoendelea mtaani

Moja ya majukumu ambayo yapo katika usajili wa JamiiForums ni kuimarisha Demokrasia na kuchochea uwajibikaji Nchini

Ukiwagusa Wanasiasa unaweza kuambiwa unaandika uongo au unachochea watu na unaweza kubambikiwa kesi. Tunaibua taarifa sahihi ambazo tunajua zinaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi pia

Katika kuchocheza #Demokrasia Nchini JamiiForums ina Shindano la #StoriesOfChange ambalo limetengenezwa maalum kwa Wananchi waache kulalamika badala yake wawe sehemu ya kuimarisha Demokrasia na maendeleo kwa kuandika maudhui yenye tija

Pia katika kutambua mchango wao, walioandika vizuri tunawatuza, Oktoba 7, 2023 tutawapa tuzo waliofanya vizuri katika Shindano kwa kuwa tunaamini waliyoyaandika yanaweza kubadilisha Taifa kwa namna moja ama nyingine

Dkt. Elisha Magolanga, Mhadhiri - UDSM-SJMC
Dunia ipo kiganjani, wakati nasoma chuo, asubuhi nilikuwa naona mijadala mingi mikubwa na mizito kupitia JamiiForums, lakini sasa hivi vijana wengi wanashindwa kubishana kwa hoja, wanabishana au kujenga hoja kwa hisia badala ya uhalisi

Miaka ya nyuma Siasa ilikuwa inajadiliwa zaidi kuliko mpira, lakini miaka ya hivi karibuni mpira umekuwa na nguvu kubwa mitandaoni kuliko hoja kama za Siasa au Maisha

Elisha Magolanga.PNG

Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (SJMC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Elisha Magolanga akichangia mada ukumbini.

Hiyo haijatokea bahati mbaya, ni ajenda ambayo imetengenezwa na kutufanya watu tusahau baadhi ya vitu muhimu vya kujadili ikiwemo Demokrasia

Mtandaoni uki ‘like’ kurasa saba au zaidi basi baada ya hapo utaanza kuletewa ‘posts’ ya kile ambacho ume ‘ki-like’, sasa hivi tunapoanza Ulimwengu wa Akili Bandia itafikia sehemu hata ukiwa na hela basi unaletewa vitu vinavyoendana na mazingira yako, hivyo tunapokuwa huru basi tunatakiwa kutambua ukuaji wa Digitali pia

Mwanafunzi wa Chuo kutojua Demokrasia ni nini, hii ni aibu

Wakisikiliza.PNG

Washiriki wakifuatilia uwasilishaji,

Mabadiliko ni maamuzi ya wewe mwenyewe, tumia Digitali kufanya mabadiliko na unaweza kujipanga kwa kujua nini unatakiwa kukifanya. Tunaruhusu watu wasio na weledi watengeneze ajenda badala ya kuzingatia nini ambacho sisi tunaweza kukifanya

Pia soma: Septemba 15, Maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Demokrasia
 
Naomba kuwasilisha....🤗
 

Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    10 KB · Views: 3
Ni michango mizuri Sana Kwa kweli yenye kutamani iwe demokrasia ya kiutendaji na siyo katika makaratasi tu.
 
Back
Top Bottom